Tychob
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 3,972
- 5,170
Hamna cha mjomba kuwa mama ujinga tuu, mama ni mama na mjomba ni mjomba.Mjomba ni mama, mtreat kama mama yaani muulize anataka kiasi gani ili ajitegemee mpe kiasi hicho halafu utemane nae.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamna cha mjomba kuwa mama ujinga tuu, mama ni mama na mjomba ni mjomba.Mjomba ni mama, mtreat kama mama yaani muulize anataka kiasi gani ili ajitegemee mpe kiasi hicho halafu utemane nae.
Huyo mjomba Mali siyo za ukoo wao amtimue tuu...Dah ndugu yangu hili nalo ni tatizo au wewe unataka liwe tatizo? Maana unavyoendelea kutumia makalio badala ya kichwa naona unaenda haribu mahusiano na ndugu zako kisa Mali ambazo Dingi alikufa akaziacha. Ni kweli hupendi kurudishwa nyuma na huyo anko ila najiuliza kama wewe uliaminika hadi kukabidhiwa Mali unashindwaje kula na kipofu??
We jamaa umeongea bonge la kitu.Bro nimesoma uzi wako ngoja nikushaur kitu.
Hapo kazi ilipofikia ni wakat wa wewe kufanya shughuli yako binafs. Hiyo ni ishara Mungu anakupa ya kufanya ile kitu inaitwa agano la asili. Shida ya hiyo kazi yako ni kuwa mbeba maono na watafsiri maono hamuendani so chakufanya. Itisha kikao cha familia nzima weka meza mpango mkakati wako na watu unaotaka kufanikisha nao huo mpango. Sasa unasema kuna mawili ni au waupitishe au wakugawie chako uanze fresh. Mzee usimuangalie Mama cjui mtu unavyotaka kuitafuta kesho ya watoto wako waachie wafu wazike wafu wao. Huwez kufungiwa nira na wasio amin mzee. Waache wafu wazike wafu wao. Baada ya hapo jitahd ufunge vioo na uwe na sura ngumu ukomae miaka 10 watakutafuta wote
Ameeleza kuhusu magari kuliko alichokusudia.Ungeandika kwa mpangilio nzuri basiii
Hahahaha umejuaje sinywi pombe. Huu utafit umeufanyia wapWatu kama nyinyi wameadimika hapa jamvini .
Hongera una kichwa kizuri bila shaka hunywi pombe
Weee kwani mama Ako ndo MUNGU,? Yaani mtu aharibu kazi uogope maneno ya mama?Huu ni mtihani wangu mkubwa, ipo hivi nina mjomba yangu ambaye ni mdogo wake mama yangu mzazi, kiumri ni mdogo kwangu kama miaka 5 hivi, huyu mjomba pamoja na wajomba wengine wawili na mama zangu wadogo, makuzi yao ni wamepita kwenye mikono ya mzee wangu.
Mzee wangu alikuwa ni mfanyabishara wa kati, katika uhai wake aliacha mashamba mengi, nyumba kadhaa, duka mbili na gari za biashara, hadi anafariki gari zilikuwa zimechoka, nilizifufua kwa mnaozijua scania ni chuma kisichoisha kishamba.
Katika uhai wake mzee alifanikiwa kuzaa na wanawake karibu sita, huyu wa sita mtoto alifariki alikuwa ni dada yetu* katika hawa watoto tuliobaki mimi ni mtoto wa mwisho na katika siku za mwisho za maisha ya mzee hapa duniani mimi nilikuwa karibu zaidi na mzee na mimi ndiye nilifundishwa kazi karibu zote za mzee, hata kuna mali nyingi kama mashamba ya miti mzee alinionyesha mimi tu, kiufupi alinipenda sana (huwa naumia sana kwa kumkosa mzee hii hali huwa inajirudia sana )
Tangu mzee anaumwa hadi alipofariki nilikuwa nasoma chuo, baada ya msiba tulikaa kikao cha familia na familia kuamua mali zote ambazo hazikugawanywa na mzee zibaki ni mali za familia na akibidhiwe mama kama msimamizi mkuu na mimi nimsaidie mama.
Kwa bahati mbaya baada ya mzee kufariki nilipanic sana, nilijingiza kwenye ulevi wa pombe hali iliyomfanya mama kunichukia sana na kunitaka nisiwe sehemu ya mali zake, hadi niliposoma postgraduate ya ualimu na kupata kazi ya aulimu bado mama alikuwa ananiona mimi chenga na kumlaumu mzee kuwa alinidekeza sasa nimeharibika.
Baada ya kupata kazi na kaka zangu kuona mali zinaharibika na mimi naishi maisha magumu, walimjia juu mama na kunikabidhi mali zote nizisimamie kwa sababu walikuwa wanajua ukaribu wangu na mzee.
Baada ya kupewa mali nilianza na mashamba kuyafufua, nikaja na duka moja, duka lingine lilikuwa vizuri na lilikuwa linauzwa na mama na ndugu zake hadi leo sihusiki nalo, nakumbuka nilipewa kama 20m kama mtaji, so nikazipeleka shambani, kisha dukani, baada ya hapo nilikopa mimi kwa sababu nilikuwa najua mikopo ya mzee na kisha nikafufua gari moja, baada ya kukufua gari ilibidi nimtafute kaka yangu flani nimuombe apewe gari na gari anaijua na ana connection kubwa ya wafanyabishara, miaka mingi amefanya kazi na marehemu mzee kama dreva mkuu.
Baada ya kumpatia gari huyu kaka yangu ,tulipiga sana kazi, hela ya gari unaishika tukalipa vizuri mkopo, baada ya kulipa tukamua tufufue gari nyingine kweli nikaiweka nyingine sawa na nyingine ikauzwa nikatufa fuso, hapo ndipo shida ilianza, mama aliniomba nimpe gari moja mjomba kwa sababu ni dereva na anakaa home na mother kamaliza chuo ajira hakuna na dukani wapo wengine.
Nilivyompatia gari haikuwa shida mwanzoni, baadaye kidogo mjomba akaanza makeke ya kugombana na madreva wengine, kageuka boss, yule dreva wangu mkuu kaka yangu alikuja kunikabidhi gari kuwa hawezi fanya kazi kwenye mazingira magumu, nilimuomba sana na kumuita mjomba na kumweleza risk na tabia zake kuwa hazifai, nadhani hakunielewa, akaendelea na tabia zile zile, ilibidi niwaite wajomba wengine labda wamkanye, kweli tulikaa kikao.
Mimi, wajomba na mama, kweli mjomba alikiri atabadilika, cha ajabu baada ya kikao mama alinijia na kunilaumu sana, eti namtia mkosi mdogo wake kumuitia vikao na kuniambia nisirudie kukiwa na shida nimwambie yeye, ilibidi nimwambie kuwa akirudia kwa kweli namfukuza, nilipomwambia hivyo dah mama alikuja juu sana na kunitishia sana hata kudiriki kusema atakunywa sumu nikimfukuza mdogo wake.
Kweli tumefanya kazi kwa amani kama miaka miwili hadi sasa hapakuwa na shida, shida zimerudi upya gari zilikuwa njia ya Mbeya kubeba viazi, acha tu mjomba kawanyanyasa sana huko, tunapanga mafuta na dreva wangu mkuu, nampatia hela dah mjomba hataki nimpe dreva huyo, maneno kibao dah nashindwa kuelewa, nawaza nimfukuze nakumbuka kauli ya mama nikimwacha anaharibia kazi, kiufupi nipo njia panda naona kabisa mjomba hayupo kwenye maono yangu.
Huyu dereva mkuu namhitaji sana kwa sasa, kuna mahali nataka nifike kwenye biashara ya gari, fundi wangu hamtaki mjomba anadai wanapishana, kiufupi mjomba anaona hizi mali ni zao na dada yake, nimejaribu kumweleza umuhimu wa kuheshimu wengine, umempatia mtu pesa akusaidie kuzungusha halafu unampelekesha akizipiga chini haelewi, tayari naona nina kirusi kwenye kazi zangu kukitoa inanipa headache.
Moyo nimeusikiliza unasema fukuza shida mama, sasa mama atafanyaje, kajamaa kanajiona ni sehemu ya umiliki, mimi mwenyewe huwa nakaa na kaka zangu tunajadili wananipa malengo najiwekea malengo, kaka zangu hawa ni mama tofauti, ni utu wao tungegawana hali ingekuwa ngumu sana kwangu, nipo kwenye mtanziko mkubwa.
Kasema tatizo ni mjomba ake,mbona kaelezaAmeeleza kuhusu magari kuliko alichokusudia.
Mali za baba ake😅Mali si za dada ake lakin au zako
Mpige chini harafu mwambie mama yako anywe sumu kama alivyoahidi. Njia ya mafanikio inahitaji watu wenye maamuzi magumu pia chunguza kifo Cha mzee wakoHuu ni mtihani wangu mkubwa, ipo hivi nina mjomba yangu ambaye ni mdogo wake mama yangu mzazi, kiumri ni mdogo kwangu kama miaka 5 hivi, huyu mjomba pamoja na wajomba wengine wawili na mama zangu wadogo, makuzi yao ni wamepita kwenye mikono ya mzee wangu.
Mzee wangu alikuwa ni mfanyabishara wa kati, katika uhai wake aliacha mashamba mengi, nyumba kadhaa, duka mbili na gari za biashara, hadi anafariki gari zilikuwa zimechoka, nilizifufua kwa mnaozijua scania ni chuma kisichoisha kishamba.
Katika uhai wake mzee alifanikiwa kuzaa na wanawake karibu sita, huyu wa sita mtoto alifariki alikuwa ni dada yetu* katika hawa watoto tuliobaki mimi ni mtoto wa mwisho na katika siku za mwisho za maisha ya mzee hapa duniani mimi nilikuwa karibu zaidi na mzee na mimi ndiye nilifundishwa kazi karibu zote za mzee, hata kuna mali nyingi kama mashamba ya miti mzee alinionyesha mimi tu, kiufupi alinipenda sana (huwa naumia sana kwa kumkosa mzee hii hali huwa inajirudia sana )
Tangu mzee anaumwa hadi alipofariki nilikuwa nasoma chuo, baada ya msiba tulikaa kikao cha familia na familia kuamua mali zote ambazo hazikugawanywa na mzee zibaki ni mali za familia na akibidhiwe mama kama msimamizi mkuu na mimi nimsaidie mama.
Kwa bahati mbaya baada ya mzee kufariki nilipanic sana, nilijingiza kwenye ulevi wa pombe hali iliyomfanya mama kunichukia sana na kunitaka nisiwe sehemu ya mali zake, hadi niliposoma postgraduate ya ualimu na kupata kazi ya aulimu bado mama alikuwa ananiona mimi chenga na kumlaumu mzee kuwa alinidekeza sasa nimeharibika.
Baada ya kupata kazi na kaka zangu kuona mali zinaharibika na mimi naishi maisha magumu, walimjia juu mama na kunikabidhi mali zote nizisimamie kwa sababu walikuwa wanajua ukaribu wangu na mzee.
Baada ya kupewa mali nilianza na mashamba kuyafufua, nikaja na duka moja, duka lingine lilikuwa vizuri na lilikuwa linauzwa na mama na ndugu zake hadi leo sihusiki nalo, nakumbuka nilipewa kama 20m kama mtaji, so nikazipeleka shambani, kisha dukani, baada ya hapo nilikopa mimi kwa sababu nilikuwa najua mikopo ya mzee na kisha nikafufua gari moja, baada ya kukufua gari ilibidi nimtafute kaka yangu flani nimuombe apewe gari na gari anaijua na ana connection kubwa ya wafanyabishara, miaka mingi amefanya kazi na marehemu mzee kama dreva mkuu.
Baada ya kumpatia gari huyu kaka yangu ,tulipiga sana kazi, hela ya gari unaishika tukalipa vizuri mkopo, baada ya kulipa tukamua tufufue gari nyingine kweli nikaiweka nyingine sawa na nyingine ikauzwa nikatufa fuso, hapo ndipo shida ilianza, mama aliniomba nimpe gari moja mjomba kwa sababu ni dereva na anakaa home na mother kamaliza chuo ajira hakuna na dukani wapo wengine.
Nilivyompatia gari haikuwa shida mwanzoni, baadaye kidogo mjomba akaanza makeke ya kugombana na madreva wengine, kageuka boss, yule dreva wangu mkuu kaka yangu alikuja kunikabidhi gari kuwa hawezi fanya kazi kwenye mazingira magumu, nilimuomba sana na kumuita mjomba na kumweleza risk na tabia zake kuwa hazifai, nadhani hakunielewa, akaendelea na tabia zile zile, ilibidi niwaite wajomba wengine labda wamkanye, kweli tulikaa kikao.
Mimi, wajomba na mama, kweli mjomba alikiri atabadilika, cha ajabu baada ya kikao mama alinijia na kunilaumu sana, eti namtia mkosi mdogo wake kumuitia vikao na kuniambia nisirudie kukiwa na shida nimwambie yeye, ilibidi nimwambie kuwa akirudia kwa kweli namfukuza, nilipomwambia hivyo dah mama alikuja juu sana na kunitishia sana hata kudiriki kusema atakunywa sumu nikimfukuza mdogo wake.
Kweli tumefanya kazi kwa amani kama miaka miwili hadi sasa hapakuwa na shida, shida zimerudi upya gari zilikuwa njia ya Mbeya kubeba viazi, acha tu mjomba kawanyanyasa sana huko, tunapanga mafuta na dreva wangu mkuu, nampatia hela dah mjomba hataki nimpe dreva huyo, maneno kibao dah nashindwa kuelewa, nawaza nimfukuze nakumbuka kauli ya mama nikimwacha anaharibia kazi, kiufupi nipo njia panda naona kabisa mjomba hayupo kwenye maono yangu.
Huyu dereva mkuu namhitaji sana kwa sasa, kuna mahali nataka nifike kwenye biashara ya gari, fundi wangu hamtaki mjomba anadai wanapishana, kiufupi mjomba anaona hizi mali ni zao na dada yake, nimejaribu kumweleza umuhimu wa kuheshimu wengine, umempatia mtu pesa akusaidie kuzungusha halafu unampelekesha akizipiga chini haelewi, tayari naona nina kirusi kwenye kazi zangu kukitoa inanipa headache.
Moyo nimeusikiliza unasema fukuza shida mama, sasa mama atafanyaje, kajamaa kanajiona ni sehemu ya umiliki, mimi mwenyewe huwa nakaa na kaka zangu tunajadili wananipa malengo najiwekea malengo, kaka zangu hawa ni mama tofauti, ni utu wao tungegawana hali ingekuwa ngumu sana kwangu, nipo kwenye mtanziko mkubwa.
Hongera Kwa kilichoamuliwa ila endelea kuwa makini zaidi.nashukuru wote kwa ushauri, leo tulikaa kikao cha familia mimi, mama , wajomba na mjomba mhusika, tumeyamaliza kwa amani tu , kashuka kwenye gari na amekubali makosa yake, na tumekubaliana ataenda shamba akisamamie parachichi na mifugo huko, nako huko nimempa precautions kabisa kuwa nina vijana wangu nimefanya nao kazi miaka mingi kidogo hatakiwi kuwatingisha , akifeli huko anarudi kwao MAKETE
"pluto" 🤣Mama hawezi kujipeleka pluto kirahisi hivyo, huyo mjomba alichofanya ni kucheza na akili ya Dada yake tuuu,
Mtu mzima naye anakosea, na akikosea anatakiwa aonyeshwe njia, Oya Si nia yako ni nzuriii? Ongea na Mama na Mjomba mwenyewe na hata ndugu wengine, unampa Nafasi ya mwisho akizingua Piga Chini.
BTW Umeandika Maneno 677 na herufi 4418 bila kutupumzisha, yaani hata Aya moja? huu ni ujangili.
Mjomba shikilia hapo hapo kwanza mpaka a edit.
Kama mama kivipi wakati ukoo tofauti yani mfano wewe Dada yako kaolewa na mume kafariki halafu wewe uanze kusumbuana na watoto wa dada yako kuhusu Mali zao.Mjomba ni mama, mtreat kama mama yaani muulize anataka kiasi gani ili ajitegemee mpe kiasi hicho halafu utemane nae.
Kula na kipofu kivipi wakati mali za familia yao Mama na watoto sasa mjomba hapo anaingiaje mpaka unasema ale na kipofu?Dah ndugu yangu hili nalo ni tatizo au wewe unataka liwe tatizo? Maana unavyoendelea kutumia makalio badala ya kichwa naona unaenda haribu mahusiano na ndugu zako kisa Mali ambazo Dingi alikufa akaziacha. Ni kweli hupendi kurudishwa nyuma na huyo anko ila najiuliza kama wewe uliaminika hadi kukabidhiwa Mali unashindwaje kula na kipofu??
Huyo mjomba na yeye si ana wazazi wake kwanini ascended kurithi mali za wazazi wake.Mali za baba ake😅
Huyo mjomba akatafute vyake aache kuvizia vya shemeji
Mjomba ni mama wapi bwanaaa....FUKUZA AONDOKE HAPOMjomba ni mama, mtreat kama mama yaani muulize anataka kiasi gani ili ajitegemee mpe kiasi hicho halafu utemane nae.
Bosss,tuambie mjomba kakaa sawa au alizingua shambani pia?nashukuru wote kwa ushauri, leo tulikaa kikao cha familia mimi, mama , wajomba na mjomba mhusika, tumeyamaliza kwa amani tu , kashuka kwenye gari na amekubali makosa yake, na tumekubaliana ataenda shamba akisamamie parachichi na mifugo huko, nako huko nimempa precautions kabisa kuwa nina vijana wangu nimefanya nao kazi miaka mingi kidogo hatakiwi kuwatingisha , akifeli huko anarudi kwao MAKETE