Namibia: Waziri wa kilimo afukuzwa kazi kwa tuhuma za ubakaji msichana wa miaka 16

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Waziri wa Kilimo wa Namibia, Mac-Albert Hengari, amefukuzwa kazi baada ya kutuhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 miaka mitano iliyopita. Kwa mujibu wa polisi, Hengari alikamatwa siku ya Jumamosi baada ya kudaiwa kujaribu kumhonga mlalamikaji, ambaye sasa ana umri wa miaka 21, ili aondoe kesi hiyo.

Hengari, mwenye umri wa miaka 59, amekanusha kufanya kosa lolote. Alifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu na kunyimwa dhamana. Hii inakuwa kashfa kubwa ya kwanza kwa Rais wa kwanza mwanamke wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, tangu alipoapishwa kushika madaraka mwezi uliopita.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais haikueleza sababu rasmi za kumfuta kazi Hengari, lakini ilieleza kuwa pia amevuliwa nafasi yake katika Bunge la Taifa. Hengari alikuwa ametajwa na rais kuwa mbunge kwa tiketi ya chama tawala cha Swapo.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, Hengari anachunguzwa kwa makosa kadhaa yanayohusiana na tukio hilo, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara, ubakaji na kushambulia. Siku ya Jumatatu, alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu katika mji mkuu wa Windhoek akikabiliwa na shtaka la kuzuia mchakato wa haki kuchukua mkondo wake.

Hengari na washitakiwa wenzake wataendelea kushikiliwa rumande hadi tarehe 3 Juni, kesi yao itakapopelekwa tena mahakamani. Walinyimwa dhamana kwa sababu mahakama iliona kuna hatari ya wao kutoroka au kuwasiliana na mashahidi.

Chama cha upinzani cha Independent Patriots for Change (IPC) kililaani tukio hilo na kusema kuwa kukamatwa kwa Hengari "kwa tuhuma za ubakaji, utekaji na utoaji mimba wa kulazimishwa" ni dalili ya "kushindwa kwa uongozi" na kunadhihirisha unafiki wa serikali kuhusu mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Chama hicho kiliongeza kuwa kesi hiyo inajiri wakati ambapo kuna ongezeko la ukatili wa kijinsia nchini humo, ambapo jumla ya kesi 4,814 za ukatili wa kijinsia ziliripotiwa mwaka jana. Namibia ina idadi ya watu wapatao milioni tatu. IPC pia ilikosoa mchakato wa uchunguzi kabla ya uteuzi wa viongozi, ikieleza kuwa Hengari aliteuliwa licha ya uchunguzi wa jinai kudaiwa kufunguliwa tangu Novemba 2024.

Rais Nandi-Ndaitwah alitangaza baraza la mawaziri mwezi uliopita ambalo lilielezwa kuwa la kihistoria kwa kuhusisha uwakilishi mkubwa wa wanawake – wanawake tisa kati ya mawaziri 14 walioteuliwa, akiwemo makamu wa rais, ni wanawake. Rais huyo mwenye umri wa miaka 72 alishinda uchaguzi wa Novemba kwa kupata asilimia 58 ya kura.

Nandi-Ndaitwah ni mwanachama wa muda mrefu wa chama cha Swapo, ambacho kimekuwa madarakani tangu Namibia ilipopata uhuru wake mwaka 1990 baada ya mapambano ya muda mrefu dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini.
1745843988133.png

Chanzo BBC News
 
Serikali mpya ishaanza cracks

Vetting

View attachment 3318740

Chanzo BBC News
Vetting haikufanyika?

Cracks looming
 
Hata ukilala na mwanamke yuko uchi na wewe uko uchi kama hataki usimlazimishe wala kumbaka. It is not worth it fellas; and rape can never be justified. Utamaliza ; na kama wewe ni binadamu wa kawaida nafsi itaanza kukusuta, kukuhukumu na kukutafuna. Ni zile scenario za "I hurt myself more by hurting you" na kamwe hautakaa uwe sawa kisaikolojia - kwako na vizazi vyako!

Ubinadamu wetu hupimwa kwa kujizuia kutenda matendo ya kihayawani hata kama uwezo wa kuyatenda tunao. Na furaha ya dakika mbili inaweza kuharibu maisha yako yote. It is not worth it! 📌📌📌📌📌📌
 
Kuna nchi huyu waziri angeonekana shujaa. Angeendelea kula mshahara. Nimekumbuka kesi ya babati.
 
Back
Top Bottom