Namiliki blog ila sioni faida yake

Namiliki blog ila sioni faida yake

Blog ni kama ukurasa wa Instagram, Facebook,n.k.

Njia ya uhakika ya kufanikiwa uwe na watembeleaji wengi utaombwa utangazie watu bidhaa au huduma zao, Kwenye blogs unaweza kuomba utangazie watu biashara zao kwenye kampuni kama Google adsense, kwa watembeleaji elfu moja unaweza kuingiza dola 1 ( shilingi 2,600 ). blogs maarufu kama za ajira, muziki, n.k. wanapata watembeleaji mpaka laki kwa siku

Mbinu nyingine za kufaidika hasa kama una watembeleaji wachache jaribu kuuza bidhaa mfano andika vitabu vyako uza kwa pdf, unaweza kuuza bidhaa zako au za wengine, kutoa ushauri, n.k.

Cha muhimu zaidi lenga sehemu moja, jikite na sehemu moja usiwe mpana sana, mfano kama ni tiba jikite na tiba za vidonda vya tumbo tu, kama ni michezo jikite na timu moja tu, n.k. ukitoka nje ya hapo ni ngumu kwasababu ya ushindani mkubwa zaidi, ni ngumu kucompte na mablogs makubwa ya kitambo kama kina millard, deal na kitu kimoja kwanza
 
Umeeleza mambo mengi ya muhimu mkuu . Ila mtandao unaotembelewa na watu wengi kuliko yete ni Google.
Ni kweli na watu wengi ambao ni potential huwa wanapatikana huko google ila shida ni kwamba ukiwa na blog mpya huwa ni ngumu kuonekana pale google kwahiyo ili watu wengi waweze kuiona kwa urahisi ni Bora udeal na social media, utengeneze cycle fulani hivi ambayo it's drive traffic kwenda kule.

Na google watu hawaspend muda mwingi ila wao huwa wanakwenda kwenye search engine na kutype random words ya kile wanachokitaka then page ya kwanza or ya pili itakayojitokeza ndio hiyo wanadeal nayo.

Ila kwenye social ukipost followers wako wanaiona bila shida na ukiwa unacontents zinazomake sense basi kupata good engagement ni uhakika.
 
Blog ni kama ukurasa wa Instagram, Facebook,n.k.

Njia ya uhakika ya kufanikiwa uwe na watembeleaji wengi utaombwa utangazie watu bidhaa au huduma zao, Kwenye blogs unaweza kuomba utangazie watu biashara zao kwenye kampuni kama Google adsense, kwa watembeleaji elfu moja unaweza kuingiza dola 1 ( shilingi 2,600 ). blogs maarufu kama za ajira, muziki, n.k. wanapata watembeleaji mpaka laki kwa siku

Mbinu nyingine za kufaidika hasa kama una watembeleaji wachache jaribu kuuza bidhaa mfano andika vitabu vyako uza kwa pdf, unaweza kuuza bidhaa zako au za wengine, kutoa ushauri, n.k.

Cha muhimu zaidi lenga sehemu moja, jikite na sehemu moja usiwe mpana sana, mfano kama ni tiba jikite na tiba za vidonda vya tumbo tu, kama ni michezo jikite na timu moja tu, n.k. ukitoka nje ya hapo ni ngumu kwasababu ya ushindani mkubwa zaidi, mablogs makubwa ya kitambo
Hapo kwene kujikita sehemu moja ndo nahisi nafelia hapo
 
Hapo kwene kujikita sehemu moja ndo nahisi nafelia hapo
Watu wengi huingia kwenye blog kupitia matokeo ya google ya vitu wanavyosechi.

Mfano mtu anasechi habari za michezo. kuna ushindani mkubwa vibaya mno, blogs zipo nyingi sana.

Kwa ugeni wako inabidi uspecialize zaidi, blog ihusu kitu kimoja tu, mfano habari za team kama KMC, ukitaka kuingia team kubwa kama Yanga ushindani ni mkubwa inabidi uingie zaidi mfano maisha ya mchezaji flani tu, usianze kushindana na magwiji kuchanganya habari, na google wakiona blog inadeal na kitu kimoja kwa muda mrefu wanaanza kuipa points kwenye matokeo, unaweza kuiita blog teuzizetu kisha ukajaza teuzi tu, blog ikianza kupanda kwenye matokeo ndio unajipanua vitu vya ziada
 
Yangu ni getravelguard.blogspot.com naombeni kama kuna anayeweza nisaidia kuipamba iweze Piga pesa, domain ime expire duh
 
Back
Top Bottom