Wakuu nina hii blog ambayo naimiliki lakini hamna inachoniingizia
Kama madhumuni ya kuanzisha hii thread ilikua upate namna blog yako itakavyoweza kukuingizia chochote kitu, unabidi upangilie baadhi ya mambo kwanza.
Japo hujashare blog yenyewe tukaiona, au inahusu nini(Ninche, Lugha, Na ipo kwa Muda gani)
Ushauri wa jumla jumla. Ni kama bado ujatafuta mada moja specific ya kuhusisha blog yako, basi zingatia hilo kwanza. Yaani blog inayojihusisha na topic moja tu iko na chances kubwa za kuonesha results kuliko ile ambayo unachanganya changanya mambo.
Kama target audience yako ni watanzania basi unaweza i monetize either kwa kutoa huduma/bidhaa inayoendana na mambo unayoongelea kwenye blog yako.
Kama ujuzi uko nao, na watu wanaona value, basi kuingiza pesa kwa namna hio iko given. Japo mpaka uenyeke mwanzoni kwanza kueka msingi na kuanza kutoa value ya kutosha(kubuild authority kwenye Ninche yako)
Kama target audience sio Bongo na maybe unataka ufocus na Adsense. Tafuta Ninche yenye CPC kubwa. Pangilia blog iwe na Responsive Design na Load time yake iwe Fast. Ipachikie ma content ya kutosha.
Baada ya kufanya hayo ni kufanya SEO Extensive, ili uweze pata Organic Traffic ya kutosha kutoka kwenye Search Engines. Na by "Traffic ya kutosha" namaanisha walau uwe unawatu wasio pungua 500 kwa siku na Views walau 2,000 kwa siku. Results unazoweza pata kama Ninche yako iko vizuri na SEO pamoja na vitu vitu vingine, umefanya vizuri.
Cha mwisho ni kusubiri tu, kuendela kuandika content zako. Then baada ya week kadhaa au mwezi unaomba Adsense.
Sasa wewe ndiye utaamua kama unaendelea kuandika, au content ulizoandika before Adsense zinatosha. Ila kufikia hapo blog itakua inakuingizia ingizia vi hela.
Wingi wa mapato kwa aina hio ya Monetization ina depend na quality ya traffic unayopata, Ninche yako na quality ya posts zako (On-Page SEO+ Readability ambayo ni mambo umaeza jifunza tu kwa ku Google na ku ya apply kwenye uandishi wako.)
(Hii blog ni ya Kiswahili, na nimeanzisha January. Nime apply baadhi ya izo vitu, na matokeo zinaonekana japo bado ni changa. Japo zipo za Adsense zenye Traffic kubwa ya hapo, ila strategy ni zile zile.)
Goodluck ✌️