Charamba
Member
- Aug 12, 2022
- 7
- 12
UTANGULIZI: Chuo kikuu ni ngazi ya juu zaidi ya elimu nchini tanzania na duniani kwa ujumla ambayo inamuwezesha mwanafunzi(Mwanachuo) kupata maarifa na ujuzi maalumu. Mfano;Udaktari, Ualimu, Sheria, Masuala ya uchumi na biashara, Masuala ya habari, na mengine mengi yatolewayo vyuoni.
MJADALA MKUU: Napenda kulipanda jukwaa hili la stori za mabadiliko kwa kuangazia juu ya suala la ELIMU na AJIRA NCHINI.
Kwa miaka ya hivi sasa kumekuwa na tatizo la ajira kwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu (Wahitimu wa kuanzia2015-2021 kwa kiasi kikubwa) ambapo wengi wao wamejikuta wakikaa mtaani bila ya kuwa na kazi za kuwaingizia kipato, jambo linalosababisha wahitimu hao wa vyuo kuilaumu serikali na kuiiona elimu walioipata si chochote kwao na walipoteza tu muda wao kuitafuta elimu hiyo.
Ni kweli kwamba kwa kawaida serikali inapaswa kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo, lakini ni ukweli uliodhahiri kwamba kuwaajili wahitimu wote wanaohitimu vyuo ni ngumu kwasababu idadi ya wanaohitimu ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa uchumi wa nchi yetu katika ulipaji wa mishahara ni mdogo hivyo serikali haiwezi kuwaajili wahitimu wote bali inaajili kulingana na ukubwa wa mfuko wake(uchumi).
Kutokana na ukweli kwamba kila mtu angependa awe na ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu ni vema sasa kila mwanafunzi wa chuo KUANGALIA NAMNA YA KUPATA AJIRA KUPITIA ELIMU ALIYONAYO kupitia mikakati mbalimbali kama ifuatayo.
Mikakati kwa wanachuo na wahitimu wa vyuokatika kupambana na tatizo la ajira.
1. Kuhusianisha elimu waliyoipata chuoni na mazingira halisia ya jamii. Hii inamaana ya kwamba kutafuta mahali panapohitaji maarifa aliyonayo muhitimu katika jamii na kuyatumia maarifa hayo kama fursa ya ajira.
2. Kutofautisha kati ya siasa na elimu. Ni ukweli kwamba siasa ipo kufichua maovu pekee hivyo suala la wanachuo kuchanganya siasa na elimu zao zinawafanya waamini kuwa serikali ndiyo inasababisha kwa100% wao kukosa ajira na ilihali wanapaswa kutumia elimu zao kutengeneza ajira.
3. Kusomea kozi wanazoziweza kwa ufanisi na siyo kusoma kwa mkumbo. Hii iko hivi.... wahitimu wengi wa elimu ya vyuo wanashindwa kubuni fursa za ajira kwa sababu maarifa waliyoyapata vyuoni hawana uwezo nayo bali wanauelewa tu hivyo wanapojaribu kubuni fursa wanafanya ovyo kabisa.
4. Kutumia pesa ya kujikimu maarufu kama( BOOM) kujenga msingi bora wa maisha baada ya kuhitimu chuo. Wanachuo wengi wanatumia Boom kuishi kwa starehe bila kukumbuka kwamba kuna maisha baada ya chuo hivyo wanapaswa kujenga msingi bora wa maisha yao ya baadae kwa kuanza kuwekeza katika fursa mbalimbali kama vile:
a .Kilimo
b. Ufugaji(kuku,bata, mbuzi n.k) c.ujasiriamali.
5. Tumia kipaji kujipatia ajira. Ni ukweli kwamba kila binadamu kabaliwa kipaji tofauti na mwingine bali ugumu uko tu kwenye mtu kujua kipaji chake. Kwa wahitimu wa vyuo pia wanaweza kutumia vipaji vyao kujikwamua kiuchumi kwa kuvifanya vipaji hivyo kuwa ajira.. mfano; kipaji cha
HITIMISHO: Mwisho japo kwa uchache nipende kutumia nafasi hii kuwakumbusha wanachuo na wahitimu wa vyuo kuwa "wasichague kazi kwa kuziona basdhi ya kazi siyo za hadhi yao bali wazifanye kazi hizo kuwa za hadhi yao kwa kuzifanya kwa ufanisi na weredi wa elimu zao......."
Nalishuka jukwaa hili la (stories of cha kwa kurudisha heshima na shukurani za dhati kwa uongozi wa JF kwa fursa hii adhimu kwetu sisi watanzani.......👍👍🙏🙏JF daima

. KUIMBA,
. KUCHEZA MZIKI au MPIRA,
. KUCHORA,
. KUHAMASISHA n.k. Ila kipaji hicho kinapaswa kutumika kikihusianishwa na maarifa ya elimu kama msomi.....

Upvote
7