SoC02 Namna bora ya kutumia rasilimali watu kuchochea maendeleo kupitia rasilimali zilizopo eneo husika

SoC02 Namna bora ya kutumia rasilimali watu kuchochea maendeleo kupitia rasilimali zilizopo eneo husika

Stories of Change - 2022 Competition

Kikapuu

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
1,122
Reaction score
1,629
UTANGULIZI.
Rasilimali ni nyenzo ya muhimu ambayo huleta faida kwa kurahisisha maisha ya mwanadamu kulingana na mahitaji yake. Rasilimali inaweza kuwa ni ya asili au si ya asili kwa mfano vyanzo vya maji, misitu na hata vivutio vya kitalii kama mlima Kilimanjaro ni rasilimali ipatikanayo Tanzania. Kupitia tume ya rasilimali watu ya mwaka 2002 imehakikisha rasilimali watu inatimiza majukumu yake ipasavyo. Kwa kuangazia baadhi ya rasilimali zipatikanazo ndani ya Tanzania ni Kama vile ardhi, watu, milima, maziwa na mito pamoja na mbuga za wanyama.

Rasilimali watu ni nyenzo inayohusu binadamu ambaye anaweza kutumia rasilimali nyingine ili kuleta maendeleo yenye manufaa kwa kizazi cha sasa na cha baadae. Rasilimali hii inaweza kuibua wataalamu mbalimbali wenye uwezo wa kukuza na kulinda rasilimali zinazowazunguka.
download (7).jpeg

Rasilimali watu.
(Picha kutoka mtandaoni)

Katika mada hii nitaonesha jinsi gani tunaweza kutumia rasilimali watu kwa ufasaha kulingana na rasilimali zipatikanazo eneo husika, Umiliki Bora wa rasilimali, upatikanaji wa wataalamu, wataalamu wanaoweza kuwepo eneo lolote, cutawala bora kulingana na upatikanaji wa rasilimali, hii asaidia kuchochea maendeleo ya kijamii na hata kitaifa.Namna bora ya kutumia rasilimali watu kwa kuzingatia rasilimali zilizopo katika eneo husika ni Kama ifuatavyo :

Vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa ni muhimu sana kwa sababu huchochea maendeleo ya uvivu , kilimo na hata utalii kwa mfano ziwa Victoria , ziwa nyasa, mto manyara na mto wame. Namna bora ya matumizi ya watu katika eneo lenye rasilimali hii ni kuhakikisha tunapata wataalamu ambao watahusika na uvuvi, kilimo, utali pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji.
images.jpeg

Uvuvi.
(Picha kutoka mtandaoni)

Ardhi ni moja ya rasilimali ya asili ambayo kwa asilimia kubwa kila mmoja kabarikiwa kuwa nayo. Rasilimali hii ni muhimu kwa kazi mbalimbali Kama vile ujenzi, kilimo na hata biashara. Namna bora ya kutumia rasilimali watu kwenye rasilimali hii. Moja, kwa eneo lenye ardhi yenye rutuba kwa mfano mkoa wa kigoma, inapaswa kuandaa na kupeleka wataalamu wa masuala ya kilimo kwa kiasi kikubwa na kuwapatia huduma Bora za kijamii ikiwa ni pamoja na naji, umeme na matibabu. Pili, kwenye ardhi isiyo na rutuba ni nzuri kwa uwepo wa wataalamu wa masuala ya biashara, uhandisi wa masuala mbalimbali kama vila umeme na majengo.
download (6).jpeg

Kilimo.
(Picha kutoka mtandaoni)
download (1).jpeg

Biashara
(Picha kutoka mtandaoni)

Misitu, mbuga na wanyamapori rasilimali hizi hutupatia faida kama fedha za kigeni, chakula, madawa na ukuaji wa maendeleo ya kijamii. Kama taifa tunapaswa kuzingatia rasilimali watu inayohutajika katika eneo husika hivyo ili kutunza na kulinda maeneo haya tunahitaji kuwa wataalamu wa kutosha wa masuala ya utalii, ulindaji wa maeneo haya, madaktari wa wanyama pamoja na wajuzi wa lugha za kigeni. Mifano ya hizo ni Kama vile hifadhi ya katavi, mbuga ya Ngorongoro, wayama kama vile twiga, simba na tembo.
download (4).jpeg

Wanyama.
(Picha kutoka mtandaoni)

Vito vya thamani kwa mfano upatikanaji wa madini ya almasi, dhahabu pamoja na Tanzanite katika maeneo ya Mwadui, Geita na kahama. Ili tuweze kufaidika na upatikanaji wa rasilimali hizi ni muhimu kuandaa na kupeleka rasilimali watu itakayoweza kutunza na kuendesha shughuli za uchimbaji madini. Taifa linapaswa kuandaa wataalamu mbalimbali watakaoendesha uchimbaji huo wataalamu hao ni wanaohusika na masuala ya miamba pamoja na wahandisi wa mitambo na umeme.
download (3).jpeg

Almasi.
(Picha kutoka mtandaoni)

Umiliki Bora wa rasilimali.
Rasilimali zote humilikiwa na serikali husika, hivyo muamuzi wa mwisho ni serikali. Ili tuweze kuleta maendeleo miongoni mwa jamii hadi kitaifa rasilimali zinapaswa ziwe chini ya serikali za mtaa. Kufanya hivi kutawezesha wenyeji kunufaika na kuleta chachu ya maendeleo kitaifa.

Upatikanaji wa wataalamu.

Njia Bora ya kupata wataalamu ni kutumia rasilimali watu iliyopo eneo husika. Hi itasaidia jamii kutambua mahitaji yake na kupunguza utegemezi wa ajira, kwani itamhamasisha mwanafunzi kusoma kozi yenye kuleta tija kwa eneo alilopo.
images (3).jpeg

wanafunzi
(Picha kutoka mtandao)

Wataalamu wanaoweza kuwepo eneo lolote.
Rasilimali watu ambayo inaweza au ni muhimu katika kila eneo ni pamoja na watoa huduma ya elimu, afya na hata ufundi kwa mfano fundi umeme au mwashi.
images (1).jpeg

Wataalamu wa afya
(Picha kutoka mtandani)
download (5).jpeg

Wahandisi
(Picha kutoka mtandaoni)

Uongozi bora kulingana na rasilimali
Tunapaswa kuwa na kiongozi mwenye uweledi na eneo husika, ni bora viongozi wanapaswa kuwa wabobezi au wataalamu kwa mfano kama eneo lina rasilimali kama vile mito na maziwa basi yatupasa kuwa na mtu sahihi mwenye uelewa na masuala hayo na si vinginevyo. Hivyo kupitia uwepo wa kiongozi bora na Umiliki wa rasilimali kwa serikali za mtaa itachochea maendeleo na ukuaji wa kiuchumi.

Changamoto na sululisho la makazi ya rasilimali watu.

Ongezeko la idadi kubwa ya watu inaweza kuathiri maeneo muhimi. Hivyo wahusika na makazi na mipango miji wanapaswa kupangilia kwa kina. Kuwepo kwa eneo maalumu la makazi pamoja na eneo muhimu kwa ajili ya matumizi mazuri ya rasilimali hiyo. Kama ni kilimo au hufadhi basi inapaswa kutengwa eneo mahususi kwa ajili ya rasilimali hizo

Hitimisho.
Kupitia matumizi sahihi ya rasilimali watu kwenye rasilimali zimzungukazo ni Bora kuliko kutumia rasilimali watu bila kuzingatia upatikanaji wa rasilimali katika eneo husika. Kulingana na mtegemeano kimazingura tunapaswa kulinda na kuzitumia vizuri rasilimali ambazo zinatuzu guka. Pia, na elimu inapaswa kutolewa kwa jamii ili ijue umuhimu wa rasilimali hizo kwa sasa na kwa baadae.

Maswali ya kujiuliza
1. He, rasilimali watu inatumika ipasavyo ?
Na Kama ndiyo kivipi zinatumika ?
Na kama sivyo ni kwanini ?
2. Ni rasilimali zipi zipo katika eneo lako ?
3. Jamii inayokuzu guka inajua umuhimu wa rasilimali watu katika kuchochea maendeleo kupitia rasilimali asilia ?
 
Upvote 0
Karibu wasomaji ukipendezwa na mada hii usisahau kunipigia kura na kuchangia maoni yako.
 
Back
Top Bottom