SoC01 Namna fikra bora na uhuru wa kusema vitavyochochea mapinduzi ya kiuchumi kwa jamii ya Watanzania

SoC01 Namna fikra bora na uhuru wa kusema vitavyochochea mapinduzi ya kiuchumi kwa jamii ya Watanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Chief Ortambo Ikumenye

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2017
Posts
247
Reaction score
503
Mada yangu itajikita zaidi kuonesha namna uhuru wa fikra na kusema unaweza kuwa ni chachu ya kuleta mapinduzi ya maendeleo ya kiuchumi kwa jamii, hususani ya watanzania. Hivo, natoa pia fursa kwa mada nyingine katika uwanda huu wa ‘uhuru wa fikra na kusema’ na namna zinavoweza kuleta mapinduzi kwenye nyanja nyingine za maendeleo ya jamii kama; elimu, siasa, michezo, dini, n.k.

Awali ya yote, nilipata ‘mgagasiko’ kidogo wakati naandaa mada yangu. Nilijiwa na vichwa vya mada takribani vinne, na hivo kunilazimu kufanya chaguo la kichwa kimoja. Ila bado sina uhakika kama nilifanya chaguo sahihi. Labda wasomaji wangu mtanisaidia pia kutoa maoni yenu kati ya hivi vichwa vingine ambavyo ni:

  • Uhuru wa fikra na kusema, ni tanuru la maendeleo ya jamii kiuchumi”,
  • Uhuru wa fikra na kusema, ni chachu ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwenye jamii”, na
  • Mapinduzi ya kiuchumi kwa jamii ya watanzania, yatachochewa Zaidi na uhuru wa fikra na kusema
Ukitizama vichwa vyote hivo vya mada ambavo vilinijia, utagundua ya kwamba vyote vinalenga kuonesha uhusiano uliopo kati ya ‘uhuru wa fikra na kusema’ na ‘maendeleo ya jamii kiuchumi’.

Fikra!
Wikipedia inatuambia kwamba ‘Fikra au Fikira ni ujumbe uliotumwa kutoka akilini kwa ajili ya viumbe hai ili kujua kutenda jambo bila kukosea’. Hivyo ni fikra ambazo zinafanya binadamu kutenda mambo kwa ustaarabu tofauti na wanyama, kwasababu bongo za wanadamu tayari zina taarifa fulani ya ni namna gani zinatakiwa kutenda na kufanya maamuzi na pia zinauwezo wa kutengeneza taarifa mpya ili kuweza kupambana na changamoto za mazingira yanayowazunguka.

Fikra pekee hazitoshi kumkamilisha mwanadamu, kinachofanya fikra kuonekana bora, ni endapo, aliyezibeba ‘fikra hizo’ atazisema, ataziwasilisha, na kuzitekeleza kwa jamii yake. Ni hapa ndipo inapoibuka hoja ya umuhimu wa ‘uhuru wa kusema’. Nimetumia neno ‘kusema’ nikiwakilisha namna ambavyo mtu anaweza kuzitoa fikra zilizopo kichwani mwake na kuziweka katika matendo au kuziweka zionekane na jamii na kunufaisha wengine katika jamii yake.

Kunapokosekana uhuru wa kusema ama ‘uhuru wa kutoa fikra kichwani na kuzileta kwa jamii’, matokeo yake ni kwamba, fursa nyingi ambazo zingeweza kuletwa na kutekelezwa kwenye jamii zinaishia kufia ndani ya bongo za watu kwa sababu ya vikwazo au kukosekana uhuru wa ‘kuzizungumza’ na ‘kuzitoa’.

Chukulia mfano: Nchi ya Tanzania ilifika mahali ambapo wale walioamua kutoa fikra zao za ukosoaji kwa mambo ambayo walikuwa wanayaona hayapo sawa, lakini tukashuhudia watu wale wakipata madhila mabaya na wengine hata kupotea kwenye uso wa dunia. Sasa, madhara ya jambo kama hili maana yake ni kwamba, linakuwa linaweka kizuizi kwa jamii na watu wenye fikra bora kuweza kutoa fikra zao kuboresha pale penye mapungufu, kwasababu kunakosekana uhuru wa kufanya hivo.

Matokeo yake sasa, changamoto za kiuchumi ambazo zingeweza kupatiwa ufumbuzi basi zinaendelea kutokupatiwa ufumbuzi, kwasababu, wenye maoni na fikra za kutatua changamoto hizo hawapo huru kufanya hivo.

Kwa muktadha huo nilifanya tafiti, kwa kujaribu kuangalia kama kuna uhusiano kati ya ‘per capita GDP ya nchi (pato la kichwa)’ dhidi ya ‘World Press Freedom Index’ ambayo inatolewa na taasisi ya reporters without borders. Nikagundua ya kwamba, kuna uhusiano chanya ‘positive correlation’, kati ya nchi ambazo zina uhuru mkubwa ‘press’ na kipato cha mtu mmoja mmoja.

PRESS.JPG

Data source: Write’s calculations, World bank (GDP Per Capita), na reporters without borders (press freedom index score).

So ukiangalia vizuri hiyo chati hapo, utaona kwamba, kuna uwezekano mkubwa kwa nchi kukuza uchumi wake kwa kuanza kuruhusu uhuru wa watu kuzielezea wazi fikra zao. Utaona kwamba ‘per capita GDP za nchi zinaongezeka Zaidi pale ambapo press freedom index ina improve ambayo naiweka kwenye mizania ya ‘uhuru wa kujieleza au kusema’.

Nikaenda tena mbali kuangalia takwimu za ‘Human Freedom Index’ ambazo kutolewa kila mwaka na taasisi ya Cato Institute kwa kushirikiana na taasisi ya Fraser Institute na Liberal Institute – Friedrich Naumann Foundation. Kwa kifupi, ‘Human Freedom Index’ ni ujumla wa ‘Personal Freedom au uhuru wa watu’, na ‘Economic Freedom au uhuru wa kiuchumi’.

Baada ya kuweka hizi takwimu kwenye chati, kuna kitu kilinijia cha haraka, utaona ya kwamba nchi nyingi zilizoendelea duniani kiuchumi kama; Australia, New Zealand, Ulaya, na America ya Kaskazini wapo ‘rated high’ kwenye ‘human freedom index’ wakati nchi nyingi ambazo ni masikini Zaidi ama zina hali ngumu ya kimaisha wapo ‘rated lower’ kwenye ‘Human Freedom Index’. Maana rahisi ni kwamba, ikiwa kama nchi itataka kupiga hatua ki uchumi na kuboresha hali ya maisha ya jamii, ni lazima kwanza ipige hatua kuhakikisha kuna uhuru wa kutosha kwa wananchi wake.

Human Freedom.JPG

Data source: Write’s calculations, The Human Freedom Index report by Cato Institute.

Hivo basi, tunazidi kuthibitsha ya kwamba, ubora wa maisha ya mwanadamu, haswa kiuchumi daima utabaki kuwa ni jambo linaloamuliwa Zaidi na ‘ubora wa fikra zake na uhuru wa kuzisema/kufanya/kuzizungumza’. Lakini fikra haziwezi kuwa bora ikiwa mtu mwenyewe aliyezibeba hizo fikra anaishi kwenye mazingira yasiyo huru na yenye vikwazo.

Ni uhuru wa fikra na kuzisema ambao ndio haswa chachu ya nchi nyingi zilizo na ‘high level of liberty kama za magharibi’ kuweza kufanikiwa kwa kuweza kuwa na ‘high level of innovations’. Kwa sababu ‘innovations’ au ugunduzi ni mjumuisho wa ubora wa mtu kufikiri na uhuru wa yeye kutoa mawazo yake ya kigunduzi kwa jamii.

Kwa maana hiyo, endapo kama jamii nzima ya watanzania ikiweka juhudi za kuboresha na kukomboa fikra zao halafu pia kuboresha mazingira ya watu kuwa na uhuru wa kuzisema fikra zao, nina Imani kabisa kwamba, nchi hii, tutaanza kushuhudia mwamko wa maendeleo ya kiuchumi, kwasababu raia na watu wenye fikra za kujenga watajiamini Zaidi na watajituma Zaidi kuzitoa fikra na mawazo yao ya kujenga kwa jamii nzima ya watanzania. Na matokeo yake ni kwamba, tutaona biashara mpya zenye muundo wa kisasa zikiibuka kwa kasi kwa sababu itakuwa ni kama hizi fikra ambazo zilikuwa kifungoni sasa zimeachiwa zitapakae mtaani.

Hivo, maoni yangu ni kwamba ili jamii ya watanzania ifanye mapinduzi ya kiuchumi, ni lazima kuwe na jitihada za kuhakikisha watu katika jamii wanakuwa na ‘fikra zilizobora’ na pia ‘wanakuwa na uhuru wa kusema/kujieleza/kufanya/kutekeleza bila kuwa na vikwazo’. Kufanikisha hii hatua, napendekeza jamii na watunga sera wafanya mambo yafuatayo:
  1. Mfumo wa elimu unaolenga kujenga zaidi uwezo wa mtu kutengeneza fikra za kigunduzi: Huwezi kuwa na uwezo wa kutengeneza fikra bora bila kuwa na elimu iliyo bora. Bado Tanzania ipo kwenye changamoto ya kielimu, kwasababu jamii ni kama imeshaamini kwamba kusoma ni kuruka vidato na sio kumpima mtu anafahamu nini kwa elimu aliyokuwa nayo. Ndo maana utashangaa kuona kuna wahitimu wengi wa elimu ya juu lakini huoni idadi hiyo ikishabihiana na kiwango cha ugunduzi ama kuibuka kwa mawazo mapya katika jamii.
  2. Jamii iachane na mienendo inayodumaza uwezo wa kufikiri: Hii inagusa mwenendo mzima wa jamii ya kitanzania kwasasa, kumekuwa kuna wimbi kubwa la jamii kujikuta kwenye kifungo cha kutaka kusoma, kusikia, na kufuatilia habari ambazo hazina tija katika mustakabali mzima wa kuleta mabadiliko chanya katika fikra zao. Jamii inatakiwa sasa ianza kufuatilia Zaidi mambo yenye tija na yanayojenga uwezo wao wa kufikiri. Kwa mfano tu, ukiangalia vyombo vya habari vya TV vya Tanzania, ni nadra sana kupata maudhui ya kufundisha, utakuta asilimia kubwa ya maudhui ni ya kuburudisha Zaidi na ambayo hayaongezi thamani kwenye fikra za jamii.
  3. Kuondoa vikwazo vyote ambavyo vinazuia aina fulani fulani ya shughuli za kiuchumi kwa kigezo kwamba ni haramu: Hili ni jambo pia natamani kuliona linabadilika katika jamii ya watanzania kwa sababu nakiona kama kitu ambacho kinatatiza ‘uhuru wa mtu kutekeleza fikra ama wazo ambalo lina tija kiuchumi’. Mfano rahisi tu, sasa hivi duniani kuna nchi nyingi sana ambazo zimepitisha sheria ya kuruhusu kilimo cha bangi na matumizi ya bangi katika tafiti za madawa. Kwa kupitisha sheria kama hizi tu imepelekea sasahivi kidunia, industry ya bangi kufika Zaidi ya US Dollar 100 Billion. Huko Marekani, jimbo la Colorado kwa mwaka, wanapata kodi takribani US Dollar 400 Million (sawa sawa na TZS 1.6 Trillioni) ambayo inatokana na shughuli za bangi. Mifano hii inatuambia nini kama jamii ya watanzania, ni kwamba hata huku Tanzania kungeweza kuwa na utaratibu wa kuruhusu shughuli hizi za kiuchumi ambazo bado watunga sera wetu wanazidi kuzikataa kwa kutokuelewa. Matokeo yake serikali inashindwa kuongeza mapato ya kodi kutoka kwenye shughuli kama hizi za kiuchumu na kuendeleza mawazo ya kizamani kukandamiza walalahoi kwa kuja na kila aina ya kodi kila mwaka.
  4. Kuondoa sheria kandamizi zinazominya aina yoyote ile ya uhuru wa watu kutoa maoni/mawazo/hisia. Jamii inavoachiwa kupiga kelele kuhusu jambo fulani ambalo sio sahihi i.e. kodi. Itawapa angalizo na serikali yenyewe kuhusu kufanyia kazi hizo changamoto. Kuruhusu watu kusema ni mfumo ambao nchi nyingi zilizopiga hatua zinatumia kama kielelezo cha kufanya mabadiliko au mageuzi fulani. Lakini kuwa na jamii ambayo imefungwa mdomo wa kuongea, maana yake ni kwamba serikali itabaki kuamini kwamba sera zake ni nzuri kwa jamii wakati uhalisia haupo hivo.
Hitimisho
Daima imekuwa kiu yangu kuona jamii ya watanzania inakuwa ni jamii ambayo inajali Zaidi misingi ya ‘uhuru wa watu kusema/kutenda’ kwa sababu ni uhuru huu ambao ndio utaoweza kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa nchi ya Tanzania. Uhuru huu wa watu kusema/kutenda ni mbolea ya kuibua ‘fikra’ za kimapinduzi ambazo daima zipo kwenye vichwa vya wananchi.
 
Upvote 4
Nimependa hoja yako ya kuruhusu shughuli kama ya kulima bangi. Serikali ingeweza kutengeneza pesa kwenye kodi na kuachana na haya makodi ya kipuuzi kunyanyasa masikini.
 
Back
Top Bottom