CLONEY
Senior Member
- Apr 3, 2012
- 104
- 29
Natumai wazima ndugu zangu,naomba mnielekeze namna ya kutumia rice coocker.
----
----Hivi pilau waweza pika kwenye rice cooker maana mimi nimezoea sufuria mengine kwangu ni mashikolo mageni
Wakuu naombeni msaada wenu wataalam wa mapishi
Hivi karibuni nimenunua rice cooker nimejitahidi kusoma ila kuna baadhi ya vitu sijavielewa vizuri hivyo
Naombeni msaada wenu wa nini ninatakiwa nizingatie cha muhimu sana nitumiapo hicho kifaa
![]()
Ufafanuzi kuhusu matumizi mbalimbali ya rice cooker
Kila kitu unachotumia jikoni mwako kinaweza kufanya kazi zaidi ya moja inategemea na ubunifu wako na kitu husika pia na muda wa kukitumia maana kadili unavyotumia kifaa husika ndivyo unavyogundua kuwa kina weza kufanya kazi nyingine .Hii inaweza kudhihirika zaidi pale unapoweza kuandaa vyakula vya aina mbalimbali kwa kutumia rice cooker.
Baadhi ya vyakula vinanyoweza kupikwa kwenye rice cooker na jinsi ya kuvipika
Kuoka Keki au mkate
Kupika keki au mkate kwa kutumia rice cooker badala ya oven, kama ilivyo mazowea.
Kuoka keki au mkate kutumia rice cooker badala ya kutumia oven. Kama una oven ni rahisi zaidi, lakini kama huna oven, hata rice cooker inaweza kufanya kazi vizuri kabisa.
Kumbuka, ukitumia rice cooker, kuna vitu vichache inabidi kuvitilia maanani. Navyo ni :
Joto la rice cooker halifanani na lile la oven. Oven huweka moto ulio sawa pande zote za keki yako, hivyo huiva vizuri na kwa muda uliopangwa. Ukitumia rice cooker si lazima utumie muda sawa utakaotumia kwenye rice cooker, hivyo basi ni lazima uwe makini.
Ziba tundu la kutolea mvuke. Rice cooker ikitumika kupika keki ni lazima uzibe tundu la kutolea mvuke, hii itafanya joto lisipotee na kuifanya keki iive vizuri zaidi.
Jinsi ya kupika kwa rice cooker:
Haya ni maelezo ya ujumla jinsi ya kuoka keki kwa kutumia rice cooker, ila inawezekana rice cooker yako iko tofauti, cha muhimu zingatia haya:
1. Fuata maelekezo
Fuata maelekezo yote kama yalivyo kwenye kuandaa unachotaka kuoka, iwe cake au mkate. Maana maelezo huwa hayategemei unapika wapi.
2. Andaa kwenye rice cooker
Ikifika hatua ya kuweka mchanganyiko kwenye sufuria ya kupikia, weka mchanganyiko wako kwenye rice cooker. Fanya kama unavyopika wali na kisha washa jiko liwe kwenye "On Mode".
3. Usiruhusu joto litoke
Ili kupate matokeo bora, hakikisha hupotezi joto litakalokuwa kwenye rice cooker, hivyo funika na mfuniko usio na tundu, au ziba tundu la mfuniko wa rice cooker ili kuweza kuwa na joto linalotakiwa.
4. Muda wa mapishi
Kama ilivyoelezwa, joto la rice cooker halifanani na lile la oven. Hivyo basi, kupika na rice cooker inatakiwa muda mrefu kiasi tofauti na oven (mara nyingi si chini ya saa 1), maana moto unakuwa siyo mkali na hautokuwa sawa kwa pande zote.
Jinsi ya kuhakikisha muda:
Kama rice cooker yako inajizima yenyewe, inabidi uwe unaiwasha hadi keki itakapoiva. Hapa inamaanisha usicheze mbali. Ukiona switch ya rice cooker inagoma kukaa kwenye cook mode huku subiria kwa dakika 5 halafu washa tena, fanya hivi hadi keki itakapoiva.
Kama rice cooker yako inaweza kutega muda, basi tega saa moja ili keki ipate kuiva vizuri. Hakikisha huchungulii kwenye rice cooker hadi baada ya saa moja kuisha. Funua funua huharibu mapishi ya keki yako.
5. Kujaribu keki
Njia nzuri ya kujua kama keki imeiva ni kuingiza kijiti cha meno au kitu chembamba kwenye keki. Kikitoka kikavu, keki yako imeiva na isubirie kwa muda kabla ya kuanza kujiramba, vinginevyo irudishie kwenye moto kwa dakika nyingine 10, rudia hadi keki iive.
Kupika pilau nyama
Moja kati ya njia ninayoonaa ni rahisi na ya haraka kupika pilau ni kutumia rice cooker , leo nitaelezea jinsi ya kuipika na njia zinazofanya iwe rahisi zaidi.
Mahitaji
- Mchele nusu kg
- Kuku mlaini nusu kg
- Viazi mviringo (mbatata) 2 vimenye na vikate
- Kitunguu saum kijiko 1 cha supu (garlic)
- Tangawizi mbichi kijiko 1 cha supu(ginger)
- Bizari nyembamba (uzile) kijiko 1 cha supu (cumin)
- Mdalasini vipande 3 vya kiasi au kijiko 1 cha aupu(cinnamon)
- Pilipili manga kijiko 1 cha chai (black pepper )
- Kidonge cha supu cha kuku 1 (chicken maggi)
- Garam masala kijiko 1 cha chai (sio lazima)
- Iliki chembe 4(cardamom)
- Karafuu kava chembe 4(dried cloves)
- Vitunguu maji kilichokaangwa kikombe 1 (nimetumia vitunguu maji vya kunnua, vipo tayari kupikia ) (onion)
- Keroti (carrot ) 1 , imenye na ikate ndogo ndogo
- Mafuta ya kupikia robo kikombe (yakihitajika) (cooking oil)
- Chumvi (salt)
Maandalizi
- Kwenye rice cooker, tia kuku uliekwisha mtengeneza na kumkosha vizuri ,chumvi, kitunguu saum, tangawizi, viazi , carrot, kidonge cha supu na spaisi zote.
- Tia maji vikombe 3 au zaidi, inategemea na supu unayotaka kulingana na mchele wako,
- Funika ,washa rice cooker ,kuku achemke awive pamoja na viazi na ibaki na supu kiasi
- Tia vitunguu maji , mchele na mafuta yakihitajika, kama kuku atakua na mafuta ya kutosha usitie mafuta, koroga kidogo funika wacha mpaka wali uwive ,ukauke ,funua uchanganye na pilau itakua tayari kuliwa.
- Kipimo cha supu inategemea na mchele utakaotumia au unaweza kutumia kipimo cha kikombe cha rice cooker,
- Mara nyingi nakua nakisia maji au supu au nikitumia kipimo cha rice cooker naengeza kama kama nusu kikombe.
- unaweza kuengeza kiasi cha spaisi kama unataka pilau ikolee rangi.
- unapotumia kuku mlaini ndio unazidi kua rahisi sababu unatumia rice cooker kupikia na anawiva haraka.
- naweza kukaanga vitunguu mwenyewe vingi ukaweka kwenye fridge au freezer na kutumia unapovihitaji au unaweza kununua dukani vilivyokua tayari kutumia/vilivyokwisha kaangwa (fried onions ).
Baaadhi ya maoni ya wadau wa Jamiiforums kuhusu matumizi ya rice cooker
----Nifanyavyo mimi:
(a) Napima mchele kwa kikombe/vikombe kiasi ninachotaka na kuuosha;
(b) Nauweka katika sufuria la rice cooker;
(c) Naongeza maji (yasiyopashwa moto) pungufu kidogo ya mara 2 ya kipimo cha mchele. (Utazoea kipimo cha maji kadiri unavyotumia);
(d) Naongeza chumvi na mafuta kwa kadiri nipendavyo;
(e) Nafunika na kuweka vema hilo sufuria katika cooker, na kuweka on umeme. Switch inakuwa kwenye "cook"
(f) Hapo bila kukoroga wala nini upikaji hufanyika na ukiwa tayari switch inafyatuka kwa sauti toka "cook" hadi "warm"
(g) Naacha kwenye warm kwa dakika chache (4 - 6), nazima umeme na kuipua;
(e) Wali tayari kupakuliwa na kuliwa.
Jaribu. Ni rahisi
----Napo hujakosa sana
Rice cooker zote sufuria zake zina vipimo vya kikombe cha kupimia mchele ambacho wanakupa
na wapi maji ya kupikia mchele yafikie
- vikombe vi-2 maji nayo yafikie ujazo wa sufuria wa alama 4 ambayo ni sawa 0.75 lt
- vikombe vi-3 ,, ,, ,, 6 ambayo ni sawa na lita moja
- ,, vi-10 ,, ,, ,,, 18 sawa na lita 3 ya maji
kwa wepesi zaidi chemsha maji yakishakuwa na joto weka mchele uliolowekwa baada ya kuupembua halafu washa button ya cooker ON ikishaiva ijajiswitch button ya warm koroga mchele ulio juu uende chini tayari ni WALI subiri hizo dk ili uchague kukauka kwake HIZO SUFURIA HAZIUNGUZI na kutokea ukoko mweusi
au anza kwa kuweka maji yaliyopoa na mchele mkavu kabisa na kuweka button cooker ON
ikishaiva ijajiswitch button ya warm koroga mchele ulio juu uende chini tayari ni WALI subiri hizo dk ili uchague kukauka kwake pakua ule
----Wakuu naombeni msaada wenu wataalam wa mapishi
Hivi karibuni nimenunua rice cooker nimejitahidi kusoma ila kuna baadhi ya vitu sijavielewa vizuri hivyo
Naombeni msaada wenu wa nini ninatakiwa nizingatie cha muhimu sana nitumiapo hicho kifaa
![]()
----Mimi yangu kila siku napikia wali, pilau biriani. Na kila maharage nachemshia humo.
Mchemsho wa nyama pia nachemshia humo ikiwa napika supu.
Kwa kweli naishukuru sana maana hata nikiwa sina sh mia ninapika kwanza maharage then naosha sufuria nabandika wali.
Ina miaka mitatu sasa.
----Nifanyavyo mimi:
(a) Napima mchele kwa kikombe/vikombe kiasi ninachotaka na kuuosha;
(b) Nauweka katika sufuria la rice cooker;
(c) Naongeza maji (yasiyopashwa moto) pungufu kidogo ya mara 2 ya kipimo cha mchele. (Utazoea kipimo cha maji kadiri unavyotumia);
(d) Naongeza chumvi na mafuta kwa kadiri nipendavyo;
(e) Nafunika na kuweka vema hilo sufuria katika cooker, na kuweka on umeme. Switch inakuwa kwenye "cook"
(f) Hapo bila kukoroga wala nini upikaji hufanyika na ukiwa tayari switch inafyatuka kwa sauti toka "cook" hadi "warm"
(g) Naacha kwenye warm kwa dakika chache (4 - 6), nazima umeme na kuipua;
(e) Wali tayari kupakuliwa na kuliwa.
Jaribu. Ni rahisi
Nifanyavyo mimi:
Nimepikia sana rice cooker hostel, Pika sana makande Tena nilikua napika maximum Mara mbili kwa wiki, wali, maharage, maandazi, chips, ugali, vegetables zote, nyama, pilau, uji na mazagazaga mengine.
Ili uweze kupika maandazi au ugali unaweka kikaratasi chembamba unachomeka chini ya kile kiswitch Cha cook ili rice cooker isijifyatue kutoka cook kwenda warm, so ukiweka kikaratasi utapika kitu chochote na hakitajifyatua. Tumepika Kila kitu kwa rice cooker