Namna mwanamke anavyonunuliwa kupitia 'mahari'

Namna mwanamke anavyonunuliwa kupitia 'mahari'

ASIWAJU

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
1,938
Reaction score
1,632
Karibu katika somo hili la leo linalohusu biashara maarufu ya kununua wanawake "mahari".

Mchanganuo au namna inavyo fanya kazi;

Bidhaa
Mwanamke [ Nyanya ]

Wauzaji
Wazazi upande wa mwanamke

Wanunuzi
Wazazi upande wa mwanamme.

Dalali
Mshenga

Mazungumzo ya biashara:

Mzazi upande wa mwanamke [ muuzaji bidhaa mwanamke/nyanya ]
Karibu ndani kuwa huru

Mnuuzi; Nimekaribia
Muuzaji; wazima utokako ?
Mnuuzi; wote wazima wa afya
Muuzaji; Ni jambo jema

Kikao rasmi cha kuuziana bidhaa kina itishwa baada ya mazungumzo mafupi ya awali kutamatika.

Ndugu baadhi wa upande wa kiume [ wanunuzi wana jumuika kwa pamoja ] na ndugu baadhi wa upande wa kike [ wauzaji ].

Biashara ina anza;

Mzazi/muuzaji wa mtoto wa kike [ muuzaji ]; Awali ya yote nipende kuwa shukuru wote kwa kuitikia wito huu, hili ni jambo jema linalo onesha muelekeo mwema wa kikao hiki.

Wote kwa pamoja tume jumuika hapa kwa dhumuni moja tu la kumuoza[ kumuuza ] binti yetu kwenda koo nyingine hii iliyopo hapa.

Makubaliano yetu sisi kama wana ukoo wa binti mtoto wetu ata ondoka hapa nyumbani kwa mahari ya shilling million tatu na ng'ombe wawili.

Hiyo ndiyo pesa na mali itakayo mtoa binti [ bidhaa ] hapa

Wanunuzi [ upande wa kiume ]; Kwanza tunapenda kushukuru kwa haya mapokezi na huu ukarimu mlio tuonesha toka tumefika mpaka sasa.

Tumepata kuya sikia mazungumzo, masharti na maelekezo ya mzazi mwenzetu kwa kuhusu suala la mahari.

Tunasema asante kwa maelekezo haya tumeya pokea lakini kabla suala halija fika mbali sana sisi kama wazazi tuna omba kulizungumza hili suala kiutu uzima zaidi ili pande mbili zote tupate kuhafikiana vyema.

Maombi yetu ni kuwa suala hili la mahari tunapaswa kulitazama upya tena kutokana na hari ya sasa ilivyo tuna omba tufanyiwe punguzo kutokana na gharama za kifedha na mali zilizo tajwa.


Mzazi/muuzaji[ upande wa kike ]; Maombi yenu nime ya pokea na kuya kubali na hii imechagizwa na heshima na busara mlizo onesha kwangu na ndugu zangu mpaka sasa hivyo nita waondolea laki tano mtapaswa kutoa million mbili na nusu na ng'ombe wawili. hapo ndipo mwisho kukokana na heshima mlizo onesha.

Wanunuzi; tumepokea punguzo lenu kwa mikono miwili na kwa shukurani kubwa, makubaliano tuliyo afikiana kwa upande wetu tunge omba kuanza na million moja zengine tutakamilisha kwa wakati wengine kama mtajali.

Mzazi/muuzaji; Kwa kuwa sote sasa tume kwisha kuwa ndugu ombi lenu na liafiki lakini ni kwa sharti la muda usio vuka mwaka lazima taratibu za mahari zipate kukamilika zote.

Ni hayo tu maelekezo yetu upande wa binti kwenda kwenu.

Mnunuzi; Tunasema asante kwa kupokea ombi letu, siku zote uugwana ni vitendo hakika tutatimiza ahadi tulizo ahidi hapa leo.

Muuzaji; Basi ningependa kuhitimisha kikao na taratibu nyingine za kupata chakula ziendele.

Jamani au kuna shida yoyote ?

Wote kwa pamoja [ upande wa kike na kiume ]; Hapana

Muuzaji; Basi taratibu zengine ziendele.

MWISHO:

Kauli za wanawake/bidhaa/nyanya.


Siweze kuolewa kwa hela ndogo, Siwezi kuchukuliwa bure, mahari ina niheshimisha, mwanaume aliye serious lazima atoe pesa nyumbani, mwanamke anaye chukuliwa bure ana dharauliwa na mwanaume, ukichukuliwa bure utateswa na mwanaume n.k
Maswali:
Je, hizi kauli za wanawake zina kweli yoyote au uongo?

Je, kuna nafasi ya jamii kubadilika juu ya biashara hii na kuweka mbele utu wa mtu?
 


Nawa karibisha wanunuzi na wauzwaji wote walio pitia katika biashara hii ya kununua mtu kama nyanya" mahari " kwa maoni yenu na majibu ya maswali yangu.
 
Karibu katika somo hili la leo linalohusu biashara maarufu ya kununua wanawake "mahari".
Mada yako umekosea kidogo, hii biashara haijawahi kukosa dalali(mshenga) hata siku moja.Na sikuizi wanalipwa kama madalali wengineo.
 
Kataa Ununuzi wa Binaadamu

Kataa Biashara ya Utumwa

Kataa Ndoa ❌
❌❌❌❌❌❌❌
 
Mada yako umekosea kidogo, hii biashara haijawahi kukosa dalali(mshenga) hata siku moja.Na sikuizi wanalipwa kama madalali wengineo.
Kweli, wacha nimuongeze
 
Back
Top Bottom