Namna mwili unavyokuwa gereza la mwanadamu

Namna mwili unavyokuwa gereza la mwanadamu

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Katika vitu vinavyomkwamisha mwanadamu kujielewa yeye ni nani? Yupo kwa kusudi gani?, ana uwezo gani? na ni kwa nini anafanya anayoyafanya ni mipaka ya mwili wake inayotegemea na milango ya fahamu.

Tukiulizwa maswali aghalabu tunajibu ndani ya mpaka wa muda na mahali "space and time" mpaka ambao ni gereza la mwili. Ikitokea mtu anaongea jambo linalovuka mpaka huo unaweza kuonekana kama una hitilafu fulani hivi au kuna nguvu nyingine inakutawala.

Imefikia hatua ambayo watu tunashindwa kabisa kuisikiliza asili yetu "formless and timeless" na kubakiza yanayokubalika na milango ya fahamu tu ambayo inadhibitiwa na mpaka wa muda na mahali.

Tumekuwa watumwa wa mpaka wa mwili kiasi cha kushindwa kabisa kuelewa chochote kilicho asili yetu. Kushindwa huku kujielewa kunatufanya ushindwa kuelewa hata viashiria vya masuala mengi yanyotokea Duniani ambayo asili yake ni nje ya mipaka ya milango ya fahamu.

Wakati mwingine kutokana na kushindwa kuelewa kinachotendeka nje ya mpaka wa mwili tunakuwa tukifanya maigizo ambayo ukifuatilia ni uhalisia utakaojidhihirisha .Mathalani ukifuatilia suala la ugonjwa wa Korona unaweza ukaona viashiria vyake vilishawahi kuigizwa mapema sana mwaka 2008 kabla ya kujidhihirisha kwa ugonjwa wenyewe Duniani.

Mwalimu wangu wa falsafa aliwahi kunisisitiza kuelewa kuwa yanayotokea katika ulimwengu wa kifizikali ni taswira za vitu halisi katika ulimwengu wa kifikra sikumuelewa sana ila kadiri muda ulivyoendekea nilikuja kuelewa.

Ulimwengu uliopo nje ya mipaka ya muda na mahali una nguvu sana na mara nyingi unatukumbusha lakini hatujiweki tayari kupokea kile tunachokisikia au kukiona kutokana na mazoea ya kuwa gerezani (mwili).

Tafakari hivi unapokuwa umelala usingizi unafikiri ni nini kinaendelea? Je unaona mpaka wa muda na mahali? Au ukishaamka unarudi gerezani mwako na kuanza kujifanya tena?..nakumbuka nilishawahi kuota ninajua juu sana kiasi cha kuona wanaonikimbiza ni kama wanajisumbua lakini nilipoamka nilijikuta kitandani katika gereza langu la mwili na siwezi kuruka hata futi tano.

Ulishawahi kuchezwa na machale dhidi ya kitu, jambo au mtu fulani na jambo hilo likatokea hata kama ni baada ya muda mrefu kupita?Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini machale hayo yalikucheza au ulipata majibu baada ya matokeo? Gereza la mwili linatusahaulisha uwezo wetu mkubwa tulioumbiwa na kutufanya tusubiri matokeo"reactive being" badala ya kuwa waandaaji wa matokeo "proactive being".

Kutokana na mipaka hiyo ya mwili kuwa kama gereza la Mwanadamu mara nyingi tunapojiuliza maswali juu ya sisi ni akina nani? tupo kwa kusudi gani tuna uwezo gani huwa hatupaswi majibu fasaha jambo linalotufanya wengi wetu kukosa kabisa maana ya maana ya maisha na uwepo wetu.Jambo hili la kushindwa kujielewa limesababisha machafuko na vurugu nyingi mno katika Dunia.

Itaendelea
 
Ninakupata mkuu.

Watu wengi zaidi ya asilimia 90 huwa wanaishi maisha yao yote duniani bila kujitambua wao ni nani.

Bila kuujua vema ulimwengu wa roho (spiritual realm) maisha yanakosa maana.

Shida kubwa ni kuwa watu wako gerezani na wameridhika kukaa gerezani.

YESU NI KRISTO
 
Bandiko zuri ila gereza la mwili haliruhusu kuelewa kwani tumeshafungwa akili.
 
Tusije kwenda kwa pupa tukawa kama Afande Sele. Subra, uvumilivu na saburi, upole na unyenyekevu, wema na upendo na kujifunza ya rohoni pasipo kikomo kutatupeleka mbali zaidi
Basi sawa
 
Back
Top Bottom