Namna pekee ya kujinasua kwenye aibu ya mkataba wa DP World ni hii hapa

Namna pekee ya kujinasua kwenye aibu ya mkataba wa DP World ni hii hapa

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
Wajumbe,

Mkataba huu wa kijambazi wa DP World na wajanja wachache ndani ya CCM na Serikali yake imekiacha CCM uchi mchana wa jua Kali. Kinachoendelea kwa sasa ni kujifaragua tu na the so called "tuendelee kutoa elimu" kwa wananchi.

Serikali ikisema unafutwa tuanze upya itakuwa ni aibu na fedheha kwa chama. Lakini pia ieleweke kwamba kushupalia kuendelea na Mkataba huu kunaweza kuiondosha CCM madarakani.

Ushauri wangu ni huu hapa. Yule yule dalali wa dili hili, Rostam Aziz arudi Dubai awaambie DP World wajifanye wamekasirika na kelele zetu ilhali walikuwa na "Nia njema" kutuletea maendeleo, Kwa hiyo wasuse mradi huo na kwenda kwingine ili watunange. Tubaki na bandari yetu.

Au mnaonaje wadau maana maji yameshajaa ruba weusi.
 
Hivi CCM mnaijua lkn? DP watapewa bandari pamoja na kelele zote

CCM haijali chochote na ushindi upo pale pale upige kura ama usipige
 
Ingekuwa ni rahisi hivyo wasingesambaa mitaani kutoa Elimu
Hivi CCM mnaijua lkn? DP watapewa bandari pamoja na kelele zote

CCM haijali chochote na ushindi upo pale pale upige kura ama usipige
 
Wezi wa bandarini wameshajaribu kuwatumia wanasiasa uchwara wameshindwa, viongozi wa dini hola, mawakili njaa nao wameangukia pua.

Sasa wanajaribu kutumia karata ya mwisho kwa kuokota mateja mitaani waje kuwasaidia kuandika ushuzi hapa, ila hao pia nina uhakika wataishiwa pumzi very soon.

Serikali haiwezi kuacha kuingia mikataba yenye faida kwa taifa, sababu ya kelele za wakwepa kodi wachache pale bandarini🤣🤣🤣
 
Aibu na fedheha kwa chama chenu ina maslahi gani kwa taifa?

Ule mkataba uvunjiliwe mbali, acheni kuleta siasa kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom