Namna Rostam Aziz alivyotoa hoja Kenya, ni kielelezo cha utajiri bila maarifa

Namna Rostam Aziz alivyotoa hoja Kenya, ni kielelezo cha utajiri bila maarifa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Rostam Aziz ameshambuliwa na makundi mbalimbali nchini Kenya baada ya kutoa maoni yake kuhusu mfumo wa biashara wa nchi hiyo huku akieleza kutotekelezwa ahadi ya Mhe. Rais ya Kenya aliyompa miaka kadhaa yakuwekeza kwenye gesi.

Rostam hajawahi kuishambulia Wala kuzungumza chochote kibaya kuhusu utawala wa Tanzania, amepataje courage yakukosoa mfumo wa Kenya?

Je, alitegemea wafanyakazi waliomkwamisha wachukuliwe hatua? Alitaka mfumo wa Kenya umkumbatie na kumdekeza Kama anavyofanuiwa na mfumo wa Tanzania? Kwanini ajisemee yeye badala yakusemea wafanyabiashara wote?

Next time inabidi wafanyabiashara wachague maneno yakusema wanapoambatana na Rais, lazima hoja zao zikaguliwe.
 
Walituaminisha wamekimbia nchi na kwenda kulelewa na wanaume wa kizungu kama wakimbizi kwa sababu hapa nchini walikuwa wanatishiwa maisha na mwendazake.

Sasa hivi mwendazake hayupo je ni lini mtaacha kuishi kwa kulelewa na wazungu Ulaya mrudi Tanzania kujenga nchi na kula kwa jasho lenu? Tunahoji haya kwa sababu tunaona mko kimyaaa.

Mkiendelea kukaa kimya watu watajua mlikimbia nchi kwa masilahi yenu na siyo kwa kutishiwa maisha na mwendazake. Kwanza wewe Lema ulilipa lile deni lako la million 400 lililosomwa na spika Ndugai bungeni?

Rudi ulipe madeni ya watu.

Na wewe mzee wa MIGA Lisu rudi hutawakuta Acacia uliokuwa unawatetea sana utakuta kampuni mpya ya madini inayoitwa TWIGA
 
Kwa hiyo ulitaka asiseme kilichomkwamisha! Wewe nani mpk umchagulie cha kusema? Mtu huongea kikwazo kinachomkwamisha katika jambo fulani sasa ulitaka anyamaze wakati ameshafanya hatua 1,2,3 ikashindikana na tatizo analiona lipo sehemu fulani, alifumbie macho wakati wa upande wa pili kero zao zinasikilizwa na kutatuliwa yeye abaki kimya? Kesho tunalalamika wakenya wanatupiga bao, tumia akili yuko vizuri.
 
Mkuu wewe utakua unachagua watu wa kuwasilikiliza. Kama huwezi appreciate hata kile alichoongea ambacho ni KWA manufaa ya nchi basi ubaki na siasa tu, jukwaa la jana lilikua ni kuona changamoto za kiuwekezaji kati ya Tanzania na Kenya na kama mtanzania nilifurahishwa na aliyoongea ukweli. Kama unataka aikosoe Tanzania basi tafuta jukwaa hilo.
 
Mkuu wewe utakua unachagua watu wa kuwasilikiliza. Kama huwezi appreciate hata kile alichoongea ambacho ni KWA manufaa ya nchi basi ubaki na siasa tu, jukwaa la jana lilikua ni kuona changamoto za kiuwekezaji kati ya Tanzania na Kenya na kama mtanzania nilifurahishwa na aliyoongea ukweli. Kama unataka aikosoe Tanzania basi tafuta jukwaa hilo.
Wewe ni Mtanzania halisi
 
Rotsam kama Mfanya. Biashara na Mtanzania yuko sahihi, kwani alichokisema ndio ukweli wakenya wana vision na wivu na nchi yao na jamii zao, hata mkenya wa kawaida, wanataka kunufaika wao tu, na hio sio zambi ni uzalendo na nchi Yao, Hata yale Kenyata aliyoongea ni ya jukwaani tu, nenda kwenye utendaji watataka kupata zaidi, kwa hio Watanzania lazima wawe imara kushindana kutetea maslahi, nchi ikipote na wao wamepoteza pia, kwani watakuja kuwa wanyonge kwenye nchi yao.

Na hii inatokea kwa sababu Tanzania imekumbatia Ujamaa, ujamaa unaua ushindani wa mtu na mtu hadi tasisi na taasisi, inatoa kujiamini na inaleta utegemezi, na uvivu, wizi, akili zinarara,

Kenya wamekumbatia Ubebari, ubepari lazima ushindane, lazima uwe agresive, lazime utetee maslahi yako, lazima utambue unataka nini. lazima uwe mbunifu.

Ni lazima Tanzania itoke kwenye mfumo wa ujamaa kama inataka kuendelea.
 
Kwani kasema nini KIbaya?Mimi nafikiriametoa mfano hai kwamba hata Kenya nako kuna mambo yanakwama kwa hio ni lazima tuelezane ukweli.Ukweli ambao Hata Rais anaujua kwamba nchi inapaswa kupata faida pia.Any ways ni mtazamo wako
 
Ninachojiuliza ni kwa nini katika hiyo miaka ya kuzungushwa hakurudi kwa Mheshimiwa Rais? Kwa jinsi alivyoongea ni Kenyatta ndie aliyemuomba awekeze kwa hiyo access alikuwa nayo. Alishindwa nini kumfuata na kumwambia kuwa jamaa zake wanamzungusha? Au tatizo ni Kenyatta mwenyewe?

Amandla...
 
Back
Top Bottom