Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Tovuti za wizara ya elimu zimekua na muundo ule ule tangu awali zilipotengenezwa hadi leo, hakuna vyumba vipya ambavyo vinabeba maudhui mapya ya kutoa msaada kwa wanafunzi.
Wote tunajua teknolojia inakua kwa kasi sana na kutokana na kasi hii ya teknolojia sekta nyingi zinakwenda kupitia mabadiliko makubwa sana ya uendeshwaji wake, na moja ya sekta ambayo inaenda kupitia haya mabadiliko ni hii ya elimu.
Nashangaa kuona watu wakihubiri kuhusu mambo ya paperless economy huku wakiwa wameacha huu mjadala wa teknolojia ya elimu upite hivi hivi kirahisi, wakati huu mjadala sisi ndio unatuhusu sana huku kwenye mataifa yetu yanayoendelea na ni rahisi kwenda nao sawa kama tu tutakua na ufahamu nao vizuri.
Tunajua…
Elimu ipo kwenye mabadiliko kutoka kwenye ule mfumo tuliouzoea wa kukaa darasani kusoma na kufanya mitihani, kuhitimu na kutunukiwa cheti. Na sasa tunakwenda katika mfumo mpya ambao hautomlazimisha mtu kukaa darasani na wenzake ili aweze kuhitimu bali sasaivi unaweza ukakaa nyumbani na ukaanza kusoma kupitia kompyuta yako na ukahitimu katika kiwango chochote unachohitaji.
Jambo hili linachagizwa sana na mfumo wa ajira, sasaivi maeneo mengi duniani waajiri hawaulizi kuhusu cheti ila wanauliza kuhusu unachoweza kufanya, kwahiyo hawakupimi kwa cheti ila wanakupima kwa ujuzi ulionao katika eneo ambalo umeombea kazi, hii inafanya watu wasijali kuhusu shule uliyosoma na ndio maana hizi shule za mitandaoni zinapata nguvu sana skuizi.
Kwahiyo na sisi kama taifa si vyema kubaki nyuma ila ni vyema kuangalia namna tutakwenda sambamba na haya mabadiliko ambayo yataenda kuibadili mazima sekta hii ya elimu, hasa kwa kuwaandaa vijana wetu taratibu taratibu ili waweze kujifunza namna ya kujisomea kwa kutumia simu janja au kompyuta na serikali inatakiwa iwe katika mstari wa mbele kwenye kufanya hili jambo lifanikiwe.
Wacha tuanzie hapa…
Wizara ya elimu iko na tovuti zake maalumu ambazo huwa inazitumia kutoa taarifa muhimu. Tovuti hizi huwa zinakuaga bize kipindi cha matokeo ya watainiwa katika ngazi fulani zinapotangazwa na kipindi ambacho watu hujaza nafasi za kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini na baada ya hapo tovuti hizi huwa zinakua hazina jambo lingine la maana linaloendelea.
Sasa kuliko kuziacha hizi tovuti ziwe bize katika vipindi viwili pekee kila mwaka ni heri wangefanya namna hizi tovuti ziweze kuwa bize vipindi vyote vya mwaka.
Sasa ni namna gani hizi tovuti zinaweza kuwa bize na zikatupeleka kwenye haya mabadiliko ya kielimu kwa hatua…
Skia hii sasa...
Kwa Tanzania Dar es Salaam ndio sehemu yenye tuition nyingi sana zinazoaminika na wanafunzi wengi walioko kila mkoa, ndio maana kipindi cha likizo vijana wengi wanasafiri kutoka mikoani kuja Dar es salaam kwaajiri ya kwenda kwenye tuition mbalimbali.
Na hii ni rahisi kwa wale ambao wako na ndugu katika jiji la Dar es salaam ila kwa wale ambao hawana ndugu inawawia vigumu kufanya hivyo richa ya kwamba wanatamani kuhudhuria kwenye hizo tuition.
Lakini pia...
Licha ya kwamba tuition ni nyingi ila vile vile tuition nyingi zinazo aminika na wanafunzi wengi zipo katika maeneo ambayo sio rafiki kwa watoto kwenda kupata elimu hii ya ziada.
Maeneo kama mchikinini, yamejaa waraibu wa madawa ya kulevya, na pia yanajaa maji mvua zinapo nyesha, wanafunzi wengi wanaokwenda kwenye haya maeneo ni wale wakiume ambao sio waoga ila wengi wao wanatamani kwenda maeneo haya ila wanashindwa kutokana na mazingira hasa watoto wa kike.
Sasa basi…
Serikali yetu inaweza kuanzia hapa kuenenda sawa na haya mabadiliko ya teknoloji katika sekta hii ya elimu, kwasababu walimu wengi wanaofundisha katika maeneo haya yenye usalama mdogo ni wazuri kweli ila sasa wako kwenye hayo maeneo kwasababu wanalipa kodi kidogo.
Kwahiyo serilali ingetumia tovuti zake kuongeza eneo ambalo litawakusanya walimu mbalimbali waweze kujisajiri na kuanza kutoa elimu kwa wanafunzi kwa bei iliyo rafiki ili wao wapate faida na serikali ipate pesa kidogo kwaajiri ya kuendeshea mfumo.
Namna mfumo utakavyofanya kazi...
Mwalimu atajisajiri na baada ya kujisajiri atakua na ukurasa wake ambao utampa mamlaka ya kufanya vitu mbalimbali, ikiwemo kuweka video za masomo, na kutengeneza majukwaa ya kujadili yeye pamoja na wanafunzi wake pekee.
Video za masomo akituma haziendi moja kwa moja kwenye ukurasa wake ila zitapitia kwenye upande wa kiongozi wa mfumo nae atapitia kuona maudhui yanayopatikana katika video hiyo akiona yanafaa atairuhusu na watu wengine watakua na uwezo wa kuiangalia.
Wanafunzi nao watajisajiri kwa kuweka taarifa zao muhimu ikiwemo daraja walilopo ili iwe rahisi kuwapeleka kwenye maudhui yanayolingana na daraja lao, na akishapelekwa huko basi atakutana na walimu mbalimbali na yeye atachagua mwalimu ambae atamuhitaji na hapa atalipia pesa kidogo ambayo hii itakwenda moja kwa moja kwa mwalimu na serikali nayo itapata asilimia kidogo kwaajiri ya kuendeshea mfumo.
Pia kwenye huu mfumo mitihani ya nyuma na majibu yake itawekwa wanafunzi waendelee kujikumbushia na kipendegele cha mitihani ya kila wiki pamoja na ile ya kila mwezi ambapo wanafunzi watakua wanalipia pesa kidogo kwaajiri ya gharama za watunga mitihani na pia kuandaa zawadi kwa wale ambao watakua wanafanya vizuri zaidi.
Hii ingesaidia kuwapa elimu iliyo salama vijana kwakua watakua wanafanya mambo yote haya wakiwa nyumbani.
Pia usawa ungekuwepo kwa kiasi fulani kwa maana watu wengi sasaivi wako na simu janja kwahiyo hawawezi kushindwa kuweka bando kuwapatia watoto wao waweze kujifunza wakiwa wako nyumbani na ile hali ya kushindwa kwenda Dar kisa hauna ndugu ingeisha..
Itaongeza chachu ya vijana kupenda kujifunza kwasababu wanajua kila wakijifunza mwisho wa wiki watajipima na wakifanya vizuri majina yao yanawekwa kwenye ukurasa rasmi wa wizara na kutangazwa na wasemaji wa wizara ya elimu pamoja na zawadi.
Pia itawaandaa vijana kuwa tayari kuelekea kwenye haya mabadiliko ya kielimu yanayokuja kwa kasi, kwahiyo hata yatakavyofika asilimia mia moja sisi kama taifa hatutoshangaa kwakua tayari tulishakua huko zamani sana.
Itapunguza wimbi la ukosaji ajira kwa walimu, kwa maana wakimaliza watajisajiri kwenye mfumo na kuanza kufundisha ili waendelee kupata pesa za ziada waendeshe maisha yao.
Najua changamoto zitakua nyingi sana kwenye huu mfumo wakati tutakapoanza ila kadri siku zitakavyokwenda tutauboresha na kuwa na mfumo ambao utasaidia vijana wengi kutokupoteza muda mwingi kwenye magari wakisafiri umbali mrefu kutafuta vituo vya kufanya mitihani na kusoma yale masomo ya ziada na badala yake watakua wanafanya hivi vyote wakiwa katika mazingira ya nyumbani kwao.

Upvote
2