Namna Vyombo vya Habari vya Kimataifa vilivyoingia mtegoni kueneza uvumi wa kifo cha Kim Jong Un

Namna Vyombo vya Habari vya Kimataifa vilivyoingia mtegoni kueneza uvumi wa kifo cha Kim Jong Un

Rahma Salum

Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
30
Reaction score
59
Rais wa Korea Kaskazini alionekana akiwa hai mara baada ya vyombo vya habari vya Kimataifa kama CNN kuripoti kuwa amefariki dunia. Je, ni kitu gani kilipelekea vyombo hivyo vya habari kutoa taarifa kuhusu kifo chake?

Mwaka 2020 kulitokea uvumi kuhusu kifo cha Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un. Ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari zilieleza kuwa amefariki dunia, vingine vikieleza kuwa yupo katika hatari ya kufa na vingine vikiripoti kuwa yupo kwenye hali ya ‘coma’.

Kitendo hicho kiligeuka kuwa aibu kwa CNN na vyombo vya habari vingine duniani, pamoja na vyombo vya habari vya kijasusi mara baada ya Kim kuonekana wiki moja baada ya kutangazwa kifo chake, akiwa anakata utepe wa moja ya kiwanda cha mbolea nje ya Pyongyang, Mji Mkuu wa Korea Kaskazini.

Ingawa ni vigumu sana kujua mambo yanayoendelea ndani ya Korea Kaskazini, picha hiyo ilidhihirisha mkanganyiko wa habari potofu na uvumi kwa Vyombo vya Habari.

Uvumi huo ulionekana kuanzia ndani ya nchi ya Korea Kusini, kutoka katika tovuti ambayo ilitoa taarifa kuhusu hali ya afya ya Kim. Tovuti hiyo kwa jina la Daily NK inahusiana na kutoa taarifa na uvumi kutoka Korea Kaskazini.

Ripoti ya Daily NK ya Aprili 20, 2020 ilisema kuwa Kim yupo hospitali kwa matibabu ya utaratibu wa moyo na mifupa ikidaiwa kuwa ni matokeo ya uvutaji wa sigara kupita kiasi na unene kupita kiasi, na kwamba inasemekana kuwa yupo katika hali nzuri. Daily NK ya lugha ya Kingereza ilieleza kuwa hali ile ilipelekea kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Uvumi huo ulipata uzito zaidi kwa kuwa Kim hakuonekana kuanzia Aprili 11, 2020 hususan kwenye sherehe ya kila mwaka inayofanyika Aprili 15 ya Maadhimisho ya siku ya jua, ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Kim II Sung ambaye ni babu yake Kim Jong-un.

Aprili 21, 2020 CNN iliripoti kuwa Kim baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo hali yake imekuwa mbaya na yupo mahututi katika hali ya nusu umauti. Taarifa hiyo ilitolewa huku ikitaja vyanzo vya taarifa kama ofisi za ujasusi kutoka Marekani ambayo haikutaja moja kwa moja ni nani.

Mtangazaji wa televisheni ya Marekani ya MSNBC, Katy Tur, aliandika katika ukurasa wake wa Twiiter kuwa Kim ubongo wake umekufa, baadae alifuta na kuomba radhi kwa kutoa ujumbe huo.

Rais wa kipindi hicho Donald Trump ambaye mara nyingi amekuwa akiviita vyombo vya habari vya Marekani ‘Taasisi za habari za uongo’, alisema kuwa taarifa iliyotolewa na CNN ni ya uongo. Aliongeza kuwa, yeye ana mahusiano mazuri na Kim Jong-Un hivyo ana imani kuwa yupo salama. Siku kadhaa baadae Trump alisema kuwa anafahamu vizuri kuhusu afya ya Kim lakini hatolizungumzia kwa muda huo.

Majibu yote yalijibiwa mara baada ya Korea Kaskazini kutoa picha za Kim akiwa na afya njema na mwenye tabasamu murua.

“Usiamini kabla ya kuhakiki taarifa. Ikiwa ni vigumu kupata taarifa kutoka Korea Kaskazini hata katika kipindi kizuri, inawezekana vipi kupata taarifa za afya ya Kim bila nchi kusika kutoa taarifa? Nchi ilikuwa katika hali ya kificho kwa sababu ya mlipuko wa Corona”, Alisema Jean H. Lee, Mkurugenzi wa Programu wa Korea katika kituo cha Wilson huko Washington.

Aliongeza kuwa, Korea Kusini sio chanzo kizuri cha taarifa. Ni lazima utafute vithibitisho na kuhakiki taarifa yoyote inayotokea katika vyanzo vya habari vya Korea Kusini.

20210312_173116.jpg
 
Alipotea mwezi mzima, hakuonekana kabisa, vyombo vyote vya habari vikaripoti ana corona na vingine vikaripoti alishafariki ila Serikali inaogopa kusema. Siku anaonekana alikua mzima wa afya kabisa, hakua na dalili hata kidogo kama alikua anaumwa.

Nahisi Magu atawapa funzo la pili kama lile halikutosha. Tatizo letu waTanzania ni wavivu, wambea, kufuata mkumbo + unafiki. Na tutatazidi kuwa maskini mpaka tuone cha moto.
 
Ukichagua kuwa Rais, umechagua kuwa muuza sura.

Ukipotea huonekani wakati kazi yako moja ni kuuza sura, lazima watu waulize, wewe umechagua kazi ya kuuza sura, mbona unazembea kuuza sura huonekani?
 
Lakini kwanini watu wakuombea mabaya? Tujifunze kuishi vizuri na watu vyeo ni vya kupita lakini ubinadamu utabaki.
Sio wote tunao muombea vibaya na isitoshe Magufuli sio hela apendwe na kila mtu. Kama Yesu na Mtume Muhammad walipendwa na wengi na walichukiwa na wengi ije kuwa Magufuli?
 
Halafu jamaa akiibuka analitest moja la masafa marefu, anawaacha waongee halafu anatulia.
 
Ni kweli, lakini kwanini iwe awamu yangu tu ndiyo inaombewa mabaya na wakati na awamu zingine nazo zilikuwa na binadamu mkuu?
Umetumia kipimo gani kujua awamu iliyo pita inaombewa mazuri na hii ina ombewa mabaya.

Ila kama hujui awamu iliyo pita Rais alitukanwa na kuambiwa yeye na serikali yake ni dhaifu,akaambiwa tena nchi haina kiongozi ipo ktk auto-pilot.

So huwezi kumzuia mtu kuongea na huwezi kupendwa na kila mtu.
 
Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanafiki wa mkuu watakua wamejifunza kitu. Ndugu wa Lissu, Azory, Erick Kaflag, Clock8, wanafunzi wale wa UDOM waliofukuzwa ghafla kwa kigezo cha kutokukidhi vigezo vya kusomea ualimu, baadhi ya waliokua na vyeti feki, WAHANGA WA AJIRA na wengine nadhani nao wamejifunza kitu kupitia tetesi zilizopo.
 
Lakini kwanini watu wakuombea mabaya? Tujifunze kuishi vizuri na watu vyeo ni vya kupita lakini ubinadamu utabaki.
Kama unafanya kinachotakiwa kufanyika hakuna kuwaza au kuonea haya wanayosema/kukuombea watu fata malengo yako......hii hasa kwa maisha ya kibongo ukitaka kuua nyani usimuangalie usoni.
 
Back
Top Bottom