Chuki za kipumba kando,ntatoa maoni yangu kama Mkenya,ni maoni tu kumbuka,tafadhali!Nina rafiki wengi watz,tulosoma nao.Cha kushangaza ni kuwa wanavowaona watz,wakenya yaani,ambao hawajamjua mtz yeyote moja kwa moja na mtazamo wangu mimi niliyesoma nao,tofauti hamna!Watz wanajulikana na wakenya kwa ustaarabu wao,heshima pia na kiswahili chao wanakipenda sana wakenya wa bara.Wakenya hawana issue na watz.Hata hivyo kama walivyo wakenya,sanasana kwenye biashara.Kila kitu kinafanywa kwa haraka na bila ukarimu wowote.Kwahivyo wakenya wengi huona watz kama wavivu na wasopenda kujituma.Mwanabiashara wa Kenya hata ukiagiza kitu kutoka kwake na maneno makali kama 'nipe kilo moja ya sukari' au hata 'leta mkate haraka!'haitakuwa ishu kwake.Kwake itakuwa kama lugha ya biashara tu!Hivo hivo kama mtz ukisema 'naomba bia mbili',huku Kenya na pesa ni zako!Wakenya vichwani mwao watakuwa wanajiuliza huyu ni zuzu nini?Waganda huku Kenya hawakubaliwi kabisa kujitambulisha kama wageni.Kwa wakenya wengi,mganda ni kama mkenya anayeishi nchi nyingine!Wanyarwanda itakuwa ngumu kwa mkenya kumwelewa vizuri kwani hatupakani nao.Wakenya wengi kuwaona wanyarwanda kama wenye ufahamu mwingi sana kwenye taaluma zao na kielimu pia.Warundi hatujui kabisa kama wakenya!