Namna Wachungaji waovu wanavyoiharibu amani ya Waumini Duniani

Namna Wachungaji waovu wanavyoiharibu amani ya Waumini Duniani

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Duniani kuna Wachungaji wa aina mbili, wema na wabaya

Wachungaji wema mara zote wanahubiri habari njema za Mungu, mara zote wanaeneza Upendo, Amani, Mshikamao na kupigania utulivu ndani ya mioyo ya Wanadamu wote

Wachungaji Wema sifa zao kubwa wanakuwa ni wasomi wa hali ya juu na wanaoendesha mambo kwa kutumia falsafa

Wamejawa elimu kubwa, maarifa, hekima na utashi

Hawa mahubiri yao yote wanayofanya huwa yanazungumzia habari njema za Mungu, kueneza Amani na Upendo na huwa waumini wote wanapopata mafundisho yao nyoyo zao zinapona majeraha

Aina ya pili ni Wachungaji waovu (Wehu)

Hawa ndio wanatengeneza mipasuko ndani ya nyoyo, familia, ndoa na jamii za waumini

Mahubiri yao makubwa yanalenga kuzungumzia Shetani, Ubaya, Visasi, Kuzimu, Kafara, Laana, Vifo, Uchawi, Mauwaji, Vita

Mahubiri yao yote yamejaa panga, masime, visu, sumu, bunduki na silaha za mauwaji

Vinywa vyao vinatema sumu, machafuko, vita, mauwaji
Matokeo yake nyoyo, familia, ndoa, jamii za Waumini zinajeruhika vibaya sana

Watakwambia ardhi yako ina laana, unakaribia kufa, kuna mtu anataka kukutoa kafara

Baba, mama au ndugu yako ni mchawi ndiye anayekumaliza

Ndugu zangu ardhi yenye laana haiwezi kuzalisha mazao wala haitafaa kuishi
Fulani anataka kukuua ni upotoshaji wa hali ya juu kwasababu siri ya kifo aijuae peke yake ni Mungu

Hawa Wachungaji wehu wana uungu au utakatifu gani mpaka wafahamu siri za Mungu hasa za kifo

Baba au mama mchawi angeua mwanaye hata kabla ya kumzaa

Ndugu mchawi asingemsomesha nduguye au kumpa kazi au mtaji bali angemwacha ili aanguke

Sifa kubwa za Wachungaji waovu (wehu) idadi yao kubwa hawana elimu hata ya darasani, wala ya kiroho mfano elimu ya Seminary wala hawana wamekurupuka tu mtaani

Pengine walikua mitaani kwa maana nyingine wamekurupuka au wendawazimu

Swala la elimu kwa Makasisi, Wachungaji, Wamisionari, Mashehe na viongozi wote wa dini ni la muhimu sana ndiyo maana sisi Wakatoliki viongozi wetu kuanzia Baba Mtakatifu, Kadinali, Maaskofu, Mapadre wamekulia darasani yaani wamesoma miaka mingi kwa maana fupi wamezeekea darasani kabla ya kupewa kibali cha kuhubiri au kuongoza Waumini

Lengo kubwa nikuhakikisha Mhubiri ni mtu mwenye akili timamu na Mwanafalsafa na sio mwendawazimu au kichaa atakayetengeneza vita, mipasuko, machafuko ndani ya nyoyo za watu

Ndugu zangu hata raisi wa nchi akikosa elimu ya hali ya juu ataingiza nchi katika vita na matatizo ya kila aina

Sisi binadamu tangu tumehudhuria makanisa ya Kikatoliki yanayoongozwa na wasomi wa hali ya juu Mapadre, Maaskofu, Kadinali, Baba Mtakatifu sisi sote ni mashahidi hakuna siku wali egemea kwenye Uchawi, Shetani, Kafara bali mara zote wamekuwa wakihubiri Amani, Upendo na Mshikamao matunda yake nyoyo zetu zinapona majeraha kila tunapopata mahubiri yao

Lakini Wachungaji waovu sisi ni Mashahidi tangu wahubiri tumekuwa watu wa kukabana koo, kupigana, kutukanana, kudhuriana kwa namna tofauti na kuitana Wachawi

Tazama kiasi gani madhara ya kuongozwa na Wachungaji waovu wasio na elimu, hekima yamekuwa makubwa na kuleta mipasuko katika nyoyo, familia,ndoa na jamii za Waumini

Wachungaji waovu ni wapotoshaji wakubwa na wasiofaa kukubalika katika jamii

Kwanza kabisa upotoshaji wao ni wa aina tofauti nianze na Kafara

Kafara inaaminika ni kitendo cha kuua mtu au kumtoa sadaka

Turudi kwa Mungu na swala la kifo

Swala la kifo haliwezi kutokea kama Mungu hajatoa kibali kwa Malaika mtoa Roho

Anayeua ni Malaika mtoa Roho lakini ni baada ya Mungu kumruhusu, ikiwa hajaruhusiwa, binadamu atakaposhambuliwa ataumia tu mwili lakini Roho haitatoka mpaka pale Malaika mtoa Roho atakapokuja kuichukua Roho yake baada ya kuruhusiwa na Mungu

Mfano ni Mh Tundu Lissu
Mh Tundu Lissu alishambuliwa na risasi nyingi lakini hakufariki ni mwili uliumia Roho haikutoka kwasababu Malaika mtoa Roho hakutumwa na Mungu akaichukue Roho yake

Kwahiyo kitendo cha kusema fulani akamtoa kafara fulani ni kitendo cha upotofu ni sawa na kusema binadamu anauwezo mkubwa kuliko Mungu hata akaweza kutoa Roho ya mwanadamu mwenzie kabla ya Mungu kutoa kibali kwa Malaika mtoa Roho

Kwa maana nyingine ni sawa na kusema Mungu ni dhaifu kwasababu binadamu anaweza kutoa Roho ya mwenzie kabla hata Mungu hajatoa kibali kwa Malaika mtoa Roho

Ushahidi wa Quran

According to Islamic belief, a "soul cannot die before God allows," meaning that death only occurs when permitted by Allah at a predetermined time, as stated in the Quran (Surah Al-Imran, 3:145).

Wataalamu wa dini tusaidieni kutafuta Ushahidi wa Biblia, sijakumbuka ni somo lipi ili tuambatanishe hapa...

Kwahiyo anayepingana na alichosema Mungu kuhusu Roho katika kifungu hiki cha Quran na kuendelea kusema fulani amemtoa kafara fulani ni mtu wa kuelimisha na kama hataki kuelimishwa basi ni wa kukemea kwa nguvu zote kwasababu anamaanisha Mungu ni muongo

Hapa tunapata funzo kuwa tusishutumu watu kuwa wamewatoa kafara watu wengine kama Wachungaji hawa waovu wanavyohubiri huu ni sawa na uuwaji, shutuma hizi ni chafu, mbaya, hatari na za kutishia uhai wa wanaoshutumiwa

Wachungaji waouvu (wehu) wanayatoa wapi maneno machafu kama haya mbona Wachungaji wema na wasomi wa hali ya juu Mapadre, Maaskofu, Kadinali, Baba Mtakatifu wamekuwa wakiyapuuza na kutokuyazungumzia makanisani

Tazama madhara ya kuongozwa na Wachungaji waovu namna yanaharibu dunia yetu

Hapa Afrika tuhuma na fikra za uchawi zimeshamiri nchi za Magharibi na Mashariki mwa Afrika lakini Afrika Kusini wamejitahidi sana kule habari za Shetani hazipo kuna utulivu wa hali ya juu

Nilipata taarifa kwamba hata nchi ya Rwanda tayari ilishaingiza mfumo wa kuchuja viongozi wa dini

Wanaoruhusiwa tu kuhubiri ni wale wenye elimu ya hali ya juu na sii vinginevyo

Shutuma za Watu kuitwa wachawi zinatokana na nini

Shutuma hizi zinatokana na watu kuonekana wakiwa na maendeleo au uwezo wa fedha lakini vyanzo vyao vya mapato vikiwa fumbo vilevile watu hawa kupata misiba ndani ya familia zao

Kwanini vyanzo vya mapato vinakuwa havionekani hii ni kwasababu ya uamuzi wa watu kuamua kufanya kazi kwa juhudi na kutokuwa na tabia ya kuonesha kazi wanazofanya

Sasa wale wasiofahamu kazi wanazofanya wanapotoka nakudhani watu hao wanajiokotea fedha kirahisi pasipo kufanya kazi jambo ambalo sio kweli

Hata inapotokea watu hao wamechafuliwa wale wanaofanya nao kazi wanaishia kupuuza taarifa zao na kusema kuwa hawa watu wanakuwaje wachawi wakati tunafanya nao kazi tena kwa kujituma sana

Swala la misiba katika familia zao hili ndilo janga la Taifa

Mungu ameshasema katika Quran kuwa Roho ya Mwanadamu haitatoka kabla ya yeye kumtuma Malaika mtoa Roho

Sasa tunawezaje kusema kuwa wao wameua familia zao kama hawa wehu wanavyohubiri kwenye vichochoro vya nchi zetu maana yake ni kuwa kibali cha kutoa Roho wamepata wapi? Wakati Mungu anasema yeye ndiye anayetoa kwa Malaika mto Roho

Au tunamaanisha Mungu ni Muongo aliposema bila kibali chake Roho haitatoka

Hatuwezi kulaumiana kuwa tunasema hivi na vile bali walioleta upotoshaji huu mkubwa katika fikra zetu ni Wachangiaji waovu

Kwahiyo tunapata elimu kuwa tunapoona maendeleo au mali za watu au misiba tusikimbilie kuwashutumu watu wengine Wachawi kama Wachungaji hawa Waovu wanavyotupotosha bali tutakuja kufahamu juhudi zao za kufanya kazi lakini kuhusu misiba tuungane na Mungu kuwa Roho haitaweza kutoka pasipo yeye kutoa Kibali kwa Malaika mtoa Roho kama anavyotuasa

Kazi tuliyo nayo sasa sisi Waumini ni ya kuponya majeraha ya Wahanga walioumizwa na Wachungaji waovu na pili kuendelea kuwakataa katika maisha yetu

Tunapokutana na Wachungaji tujitahidi kutazama hata viwango vyao vya elimu tusikubali kuhubiriwa na Wendawazimu
 
Back
Top Bottom