OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,701
- 11,920
Mamelod 69% YANGA 31%..... Je umewahi kujiuliza hizi possesion hupatikanaje? Ipo hivi kinacho angaliwa ni muda wa kumiliki mpira kwa timu husika ndani ya dakika flani mfano dakika 30, 45 au 90. kinachofanyika unaanza kuhesabu sekunde timu ikiwa na mpira mfano MAMELOD kipa wiliams kampasia mudau, mudau kampasia kekana, kekana kampasia kipa wiliams, wiliams kampasia tena mudau, mudau kapiga pasi mbele inazuiwa na mpira unachukuliwa na mudathir wa YANGA, unahesabu sekunde walizo kaa na mpira mguuni mamelodi yaani ktk kupasiana mfano ndani ya dakika 45 wamekaa na mpira dakika 40. Unachukua 40/45 × 100 = 88.9% kwahiyo kipindi cha kwanza mamelod ubao utasoma possesion ya 88.9% yanga 11.1%. . Hapo haijalishi mamelod amemiliki mpira akiwa kwenye boksi lake katikati au kwenye kumi na nane za yanga ubao utasoma hivyo hivyo 88.9% haijalishi wiliams katumia muda gani kupasiana na mabeki wake huku mpira ukiwa haufiki kwenye lango la mpinzani (YANGA). INAENDELEA