Vichaka vya kujificha Simba vinafyekwa vyote. Ooohh Yanga wamefika fainali kombe la shirikisho waje huku kwenye club bingwa. Oohh Yanga hawezi kuingia makundi ya champions league, mara Yanga akaingia tena kwa kishindo. Oohh Yanga wataishia makundi hawawezi kuingia robo fainali, Yanga wakatinga robo kabla ya Simba tena wakiwa na mchezo mmoja mkononi. Ikaja draw ya robo, oohhh Yanga kwisha habari wamepangwa na Mamelodi. Kabla ya mechi ya jana, wakasema maneno yote kwamba mechi ya Yanga vs Mamelodi itaishia kwa Mkapa tena kwa Yanga kufungwa magoli mengi. Sasa baada ya mechi ya jana, wameanza kupiga ramli za mechi ya Pretoria. Hawa hawataishiwa maneno hadi siku Yanga atakapokua juu ya Simba kwenye CAF ranking, kwa sababu ndiyo kichaka pekee kilichobaki kufyekwa, ambacho hakina muda mrefu.