Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

Ila ndugu yangu UMUGHAKA unatakiwa uje upatiwe tuzo ya mtesekaji bora. Yaani simulizi zako zote huwa ni majanga hadi najikuta nawaza huyu jamaa alikosea wapi. Nadhani katika watanzania wanaoteseka wewe utakuwepo kwenye kumi bora; shttpema hukubali kukata tamaa. One day YES utakuja na simulizi ya ushindi hapa. Endelea kupambana mwamba
itoshe kusema mali kwa njia ya uganga vimemkataa jamaa,
 
SEHEMU YA TANO



Hali ilizidi kuwa mbaya sana kwasababu maji yaliendelea kujaa kwa wingi,Baada ya yule Ustadhi aliyekuwa akiendesha kile chombo kuona mambo yanazidi kwenda mlama,alijaribu kuwasiliana na watu wa nchi kavu kule bandari ya Kirando kuona kama tutapata msaada,Mungu alisaidia mpaka wakati huo mawasiliano kwa hiyo sehemu ya katikati ya ziwa yenye mkondo mkali mawasiliano yalikuwa yakipatikana.

Alimpigia yule Seif usiku huo na bahati nzuri akapatikana,sasa ishu ikawa na kutufikia kwasababu tulikuwa mbali mno,sasa kumbe Seif alimwambia Ustadhi tuanze kutupa mizigo ziwani.

Utaratibu huwa ni kwamba,mnapopata matatizo ya msukosuko mkiwa ziwani huwa hakuna namna,mnaambiwa muanze kutupa mizigo kwenye maji,hapa huwa kuna imani za aina mbili.

1.Huamini mkitupa mizigo ziwani basi hali ya hewa itakuwa shwari.

2.Ni kupunguza uzito kwenye boti angalau kuweka uwiano sawa ili mpone.

Ustadhi "Anzeni kutupa mizigooooooo!"

Aliendelea "Tupeni mizigoooooo hiyoooo!"

Kila mtu aliyekuwa kwenye ile boti alianza kushika mzigo anaohumudu na kuurusha kwenye maji,mimi wakati huo kwakweli sikujua nifanyeje kwasababu hali yangu ilikuwa mbaya sana na nilidhani uenda siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa maisha yangu hapa duniani.Nilikuwa nawaza itakuwaje kwasababu niliondoka bila mtu yeyote kufahamu naenda wapi.

Pamoja na kutupa mizigo kwenye maji,bado hali ikazidi kuwa mbaya sana,Yule ustadhi niliona amechua boya akavaa akachukua na kamba akakamata dumu akaifunga kwenye dumu akawa tayari kwa lolote.

Wasaidizi wake nao nikaona kila mmoja amejiandaa kisaikolojia;Sisi ambao tulikuwa abiria kila mtu alikuwa akilia na kusali kivyake,wakati wenzangu kila mtu alikumbatia dumu lake,mimi kuna dumu lilikuwa na mafuta ambalo lilikuwa kando yangu,nikalichukua nikamwaga yale mafuta ziwani kisha nikafunga mfuniko nikaliweka chini ya miguu yangu.

Ustadhi na wasaidizi wake kumbe wao wote walikuwa wamejifunga kamba kiunoni kisha wakazifunga kwenye yale madumu, baadae nilipokuja kuuliza nikaambiwa madumu huwa yanakawaida ya kuponyoka mkononi ukiwa kwenye maji,hivyo ukifunga kama itakusaidia katika purukushani za mawimbi ya maji lisikimbie kwenda mbali ukafa maji.

Nakumbuka ilibidi nimuombe Mungu anisamehe dhambi zangu kwakuwa nilikuwa nimekosea sana.

Mimi "Eeeh Mungu nimekutenda dhambi,naomba unisamehe,Ikikupendeza nikalala mauti naomba unikumbuke katika ufalme wako utakaokuja"

Hayo ndiyo maombi nilimuomba Mungu wangu kwa wakati huo,kiukweli nilikuwa nimeshakata tamaa na nilijua sitoiona tena nchi kavu.

Sasa kumbe Seif aliwapigia simu kikosi cha uokoaji cha JWTZ ambao wapo jirani na Kirando kwenye mji wa Kipili,baada ya kikosi kazi cha Uokoaji cha JWTZ kupewa taarifa ile waliwasha Boti zao aina ya Fiber ambazo zinakimbia hatari,sasa kwakuwa Seif aliwaambia tupo Gezini jamaa waliondoka hadi Kirando kumchukua Seif waje nae maeneo ambayo tulikuwepo,walipofika Kirando Seif aliwapa mashine 2 za kuvuta maji kwenye boti kisha wao wakaondoka kutufuatilia tulipokuwa na Seif yeye akawasha boti yake akawa anakuja na watu wengine kwa ajili ya ukoaji.

Zile Boti za Jeshi zilifika eneo tulilokuwepo mida ya 8 usiku,walivyofika wakaanza kutuokoa kutoka kwenye ile Boti iliyokuwa inazama taratibu kwa kuzidiwa na maji,baada kuhakikisha watu wote tumeokolewa,walichukua zile mashine za kuvuta maji wakazihamishia kwenye ile boti kisha wanajeshi wengine wakabaki pale na ile fiber yao wakawa wanasaidia.Sisi tuliondolewa pale na kurudishwa hadi Kipili zilipo Kambi ya jeshi pamoja na kituo cha polisi.

Pamoja na zile Fiber kukimbia kwa spidi kali lakini tulitumia masaa 3 hadi kufika Kipili,kumbuka walifika kutuokoa ilikuwa saa 8 usiku,sasa kuondoka hapo Gezini hadi kufika Kipili ilikuwa saa 11 Afajiri.

Aisee sitokaa nisahau lile dhoruba na hata Wanajeshi walituambia Mungu alikuwa upande wetu siku hiyo kwasababu walidai huwa ni nadra kufika sehemu ya tukio wakakuta watu bado wapo hai,walisema ajali nyingi za hapo Gezini huwa wanafika kuokoa wanakuta watu walishakufa kitambo.

Bado hadi leo namshukuru Mungu sana kwasababu naamini bado anamakusudi na mimi,sema mimi ndiye muda mwingine najizima data na kuendelea kufanya maovu.

Baada ya kufika Bandarini nakumbuka simu zilipigwa sana siku hiyo kutoka kwa wakubwa,baada ya kuhesabiwa idadi yetu tulikabidhiwa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano wakitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.

Kamanda wa Jeshi "Poleni sana ndugu zetu,Mungu amewasaidia na mmenusurika,msiwe na hofu hapa ni sehemu salama na mtahudumiwa hadi pale mtakapopata usafiri mwingine au hadi dhoruba zitakapotulia"

Aliendelea "Sisi kama Jeshi lenu tumeshakamilisha kazi yetu,tunawakabidhi sasa kwa Jeshi la polisi nao waendelee na utaratibu wao,ila muwe na amani kabisa hapa mtaishi kama mpo kwenu vile"

Sasa kumbe kesho yake mkuu wa Mkoa alimwambia mkuu wa wilaya aje atuone na kutupatia Pole,kiukweli Polisi na Jeshi la wananchi(JWTZ) Kwa upande wa kule wanajali sana wananchi wa Tanzania kuliko nilivyokuwa nikidhani,nadhani ni kwasababu ya mipakani na mavurugu vurugu ya waasi wa Kongo.

Mtanzania upande ule wa Sumbawanga hadi Kigoma wanathaminiwa sana majeshi yao.


Basi,baada ya kuwa kila kitu kimekamilika,tulitafutiwa boti nyingine ambayo ilikuwa ikielekea Congo siku iliyokuwa ikifuatiwa na tukaombewa nafasi na kiongozi wa pale bandari ya kipili,boti ile ilikuwa inaelekea Congo sehemu moja inaitwa Fungo,sasa tukifika hapo kuna mizigo ishushwe kisha ndiyo turudishwe Moba.Ile safari kiukweli kutokea Kirando hadi Moba ilituchukua siku 5 kwasababu kadhaa wa kadhaa.

Sasa tukafanikiwa kufika Moba,tulipokamilisha taratibu zote za uhamiaji upande wa Congo tukaondoka zetu kuelekea mji mmoja ambao haukuwa mbali na hapo Moba unaitwa Kirungu.Sasa hapo Moba ni Jimbo au Mkoa na makao makuu yake ndiyo hapo Kirungu.

Naendelea...................
Umenikumbusha siku moja nilikua naenda uvira kongo kupitia ziwa Tanganyika kutokea kigoma,nika panda boti.

Tulipo vuka upande wa Burundi pana itwa rumonge kwa mbele yake ziwa lika chafuka hatari sana,na mimi nilitubu mazambi yangu yote,kila mtu aliomba kivyake ila Mungu ni mwema,hali ikatulia.
 
Umenikumbusha siku moja nilikua naenda uvira kongo kupitia ziwa Tanganyika kutokea kigoma,nika panda boti.

Tulipo vuka upande wa Burundi pana itwa rumonge kwa mbele yake ziwa lika chafuka hatari sana,na mimi nilitubu mazambi yangu yote,kila mtu aliomba kivyake ila Mungu ni mwema,hali ikatulia.
Mara nyingi napataga srori za ziwa tanganyika ya kuwa ina mauza uza kibao ila dizain kama siamini vile any way sikumoja nipate route ya kwenda walau kuvuka ili nisi simuliwe tena
 
Yule kijana aliyechoka ndio aliyekuwa anachukua ndoto kwenye stori bila shaka😂
SEHEMU YA SITA



Tulichukua pikipiki zikatubeba hadi Kirungu ambapo baada ya kufika kwa kuwa Jentre yeye alikuwa mwenyeji,alitutafutia Guest House ambayo tulipaswa kila chumba kulipa elfu 15.Guest za pale Kirungu karibia zote ni choka mbaya sana,tuliamua kukaa hivyo hivyo kwasababu hakukuwa na namna.

Ilipofika Jioni Jentre alienda kumleta mtu ambaye kwa mujibu wake ndiye aliyepaswa kutupatia kilichokuwa kimetupeleka, baada ya yule mtu kufika akajifanya kutusalimia na kuongea kifaransa akidhani tunakielewa,sielewi kama Jentre hakumwambia sisi ni watanzania au alifanya makusudi ili tumuone anaweza!.

Kamugisha "Sisi hatujui French "

Yeye "Oooh,kumbe nyinyi mko ba Tanzanie eee!"

Kamugisha "Ndiyo"

Yeye "Juu huyu Jentre ameniambia sikujua! nilijua tu anafanya muchezo!"

Aliendelea "Sasa nielezeni ile kitu ambayo nyie mmekuja nayo huku Congo"

Jentre "Anasema mumueleze kile kilichowaleta huku Congo"

Kamugisha "Mimi na ndugu yangu tumekuja kutafuta utajiri,hivyo tulikutana na huyu bwana Jentre akawa ametuambia wewe unaweza kutusaidia,tunaomba utusaidie"

Yeye "Ooh wala msijali,Hapa mmefika kwa mwenyewe,mimi wananiintanga makasu,ukisikia Makasu ndiyo mimi Hapa Kirungu muzima"

Aliendelea "Je nyie mmekuya na Makuta sababu ili niifanye kazi za kwenu inatakiwa muwe na makuta?"

Jentre "Anasema mmekuja na hela?,kwasababu ili kazi zenu ziende inapaswa muwe na hela?"

Kamugisha "Pesa tunayo"

Yeye "Moto nyonso asengeli kofuta troisi senti senkante mili"

Jentre "Anasema mnapaswa kulipa kila mtu shilingi laki tatu na nusu"

Kamugisha "Hilo halina tatizo tutalipa kwakuwa nina hamu sana hilo jambo lifanikiwe"

Yeye "Musiwe na wasiwasi hilo jambo lenyu ni ndogo sana"

Mimi kiukweli si kuwa na hela zaidi ya nauli na kiasi kidogo nilichokuwa nacho kama dharura,kumbuka niliamua kwenda huko Congo kwasababu ya jamaa ili asije akaona nilikuwa namchora na hata gharama zingine zote yeye ndiye alisema atanilipia,hivyo hata jamaa alipoomba hicho kiasi mimi sikuwa nacho,yeye ndiye aliyelipa hizo hela.

Baada ya kupewa kile kiasi,jamaa alisema hapo Guest tunapaswa kuhama kwasababu mizimu haitokubaliana na sisi kukaa kwenye Guest ambazo huwa zinalaza wazinzi;Hivyo alituambia tutahamia kwenye nyumba ya mdogo wake ambaye kwa muda huo hakuwepo alikuwa amesafiri.

Ilipofika Jioni Jentre alirudi na funguo za nyumba za huyo ndugu yake na akawa ametuambia tunapaswa kuhamia huko.Ile nyumba ilikuwa niya nyasi kama kawaida na hakukuwa na godoro bali tulikuta kuna vidude fulani vimesukwa kwa ustadi kwa kutumia mabua vimekuwa kama vijamvi,hivyo ndiyo jamaa alisema yatakuwa magodoro yetu kwa siku tutakazo kuwa hapo.

Jentre "Kama kaniorodhoshea mahitaji ambayo inapaswa mnunue ili shughuli ianze na shughuli itafanyika nyumbani kwake,si mbali sana na hapa"

Aliendelea "Mahitaji ni kama yafuatavyo"

Jamaa akaanza kuyataja mahitaji moja baada ya nyingine.

1.Ulezi & Ulezi - Hivi vitatumika kutengeneza pombe kidogo ya kwenda nayo porini kwa ajili ya mizimu,siyo ombi ni lazima.

2.Mafuta ya Petroli - Haya yatatumika kututoa hapo kwa jamaa hadi huko maporini kwenye mizimu.

3.Mkuki - Huu ni lazima upelekwe kwa mizimu huko porini ili tukubaliwe.

4.Shuka jeusi na Jeupe kwa kila mtu - Haya yatatumika huko porini.

5.Nyembe moja kila mmoja kwajili ya kupigwa Chale.

Alipotupa Orodha ya vile vifaa ilibidi tumpe hela Jentre akaviandae hivyo vitu ili viwe tayari kwa kazi.

Usiku ulipoingia tulienda kutafuta sehemu tukapata chakula kisha tukarudi kulala kwenye tule tujamvi pale chini ya sakafu ya udongo,aisee sitokaa nisahau siku hiyo kwasababu sikupata kabisa usingizi kulikochagizwa na mbu wengi nawa kutosha pia mbavu zilikuwa zinauma sana kulala pale chini,ajabu ni kwamba Kamugisha yeye alikuwa ameuchapa usingizi hadi anakoroma.

Kiukweli nilisema hata kama ni kutafuta lakini kwa hali ile yalikuwa ni mateso makubwa mno.

Namshukuru Mungu kulipambazuka na vile vifaa vikawa vimenunuliwa,sasa kabla ya kuanza lile zoezi yule mtaalamu akawa ametuambia tumpatie elfu kumi kila mmoja pesa Congo ili alale usiku aoteshwe kuhusu mambo yetu kabla hajaanza kutukarabati.Tulimpatia hizo hela na siku hiyo tukalala tena kwa mateso mle ndani na hatimaye kukakucha;Kulipokucha tena jamaa akatuambia alijaribu kufanya zoezi la kuoteshwa usiku lakini hakuona kitu,sasa akasema usiku huo tena inabidi alale tena ili aoteshwe ili kazi iwe rahisi.

Sasa Siku ya Tatu yule Mdogo mtu alikuja kutoka huko alikokuwa ameenda,sasa tulikuwa tunapiga nae stori mbili tatu akawa anatuambia kuna sehemu alikuwa ameenda machimboni kuchimba madini,jamaa alikuwa amechoka sana.

Mimi nilipomuona tu jamaa nikajua atakuwa na maisha magumu mno,sasa nikawa najiuliza!,Kama kweli kaka yake ni Mganga kwanini asimsaidie mdogo wake akawa Tajiri?,Nilijaribu kumshirikisha hilo wazo Kamugisha lakini nikaona analipuuza kwakuwa alikuwa na imani kubwa sana kwa yule mtaalamu.Yule mdogo mtu alijua sisi ni marafiki zake na kaka yake na yeye ndivyo alivyo mwambia.Yule jamaa alilala usiku mmoja tu kesho yake akawa ameondoka kurudi huko machimboni kwake.

Mimi "Kaka mbona kama jamaa inaonyesha amechoka sana?,Kwanini kama jamaa yake ni mganga kweli asimsaidie?"

Kamugisha "Mdogo wangu waganga huwa wanamipaka,unaweza kukuta familia yake inapata taabu ila watu wengine wanasaidiwa vizuri tu,wala hilo lisikushitue mdogo wangu"

Aliendelea "Jamaa inaonekana anajua"


Niliamua kukaa kimya ila kichwani mwangu nilikuwa nina maswali mengi sana.

Sasa baada ya siku tatu jamaa akatuambia alioteshwa mambo yetu na hivyo usiku tulipaswa kwenda kwake ili atuambie alichokuwa ameoteshwa.Kweli,ilipofika usiku tukaelekea nyumbani kwake tukiongozana na Jentre,tulipofika hapo tulimkuta akiwepo yeye na mke wake na wakiwa kwenye nyumba ya nyasi kama kawaida.

Tulikaa sebuleni kama nusu saa kisha tukaanza kusikia huko ndani mtu anaguna kwa vishindo vikubwa kana kwamba amenyigwa na kiazi kooni.


Naendelea.................
 
Mdomo ni maliyako unaweza sema chochote kwasabu hulipii kodi pia una uhuru wakutoa maoni juu ya hii story ....lakini ngoja nikwambie kitu kimoja kuita srori za wenzako CHAi huu ni upumbavu ilihali hata hiyo chai yenyewe wew huna ..... kama ni chai unaonaye sisi tuna furahia ... jifunze kuheshimu mambo ya watu wengine na kama una kwZika hujalazimishwa kuisoma ... kaa kwakutuli au pita iviiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom