Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bomoi [emoji38][emoji38] nimekumbuka ngoma Nzambe na Bomoi ya wale ndugu watatu Makoma.SEHEMU YA NANE
Jamaa alionekana kuishiwa nguvu kabisa baada ya kutuona;Mimi na Kamugisha tulibaki tunatazamana na tusijue cha kufanya.
Mtanzania "Haya jamaa waliyekuwa wakifanya nae kazi huyu hapa,muulizeni sasa maana pengine ningeonekana nawawekea kauzibe"
Kamugisha "Lakini kaka huyu jamaa ndiye mtu anayetusaidia sisi!"
Mtanzania "Acha utani !"
Kamugisha "Kaka sikutanii,huyu hapa mwenyewe aseme"
Mtaalamu "Kwani kuna shida gani hapa?"
Mtanzania "Aaah Bomoi wewe tangu lini ukawa mganga?,hawa ni ndugu zangu kutoka Tanzania usiwafanyie hivyo!"
Mtaalamu "Nilijua tu mtaharibu,ona sasa mmeshaharibu masharti ya wazee,haya mambo sikutaka watu wengine wayafahamu,mmeharibu wenyewe"
Yule mtaalamu kumbe alikuwa haitwi Makasu wala nini,jina lake halisi alifahamika kama Bomoi,sasa kitu kingine kilichonishangaza ni kwamba,mara ya kwanza tulipoonana nae alikuwa akifanya kuongea Lingala na French kwa kwenda mbele,ila alipoletwa hapo dukani na mtanzania mwenzetu alikuwa akizungumza kiswahili fasaha kabisa.
Mtanzania "Bomoi sikiliza,hawa ni ndugu zangu hebu hiyo hela uliyochukua tafadhali warudishie"
Mtaalamu "Hiyo hela ishaenda kwa wazee sasa mimi nitaitoa wapi?"
Mtanzania "Wazeee?,wazeee gani bhana wewe rudisha hela ya watu!"
Jamaa baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya aliondoka akasema anawahi kwenye ishu zake na yeye hana hela.Tulibaki tunashangaa tu kwasababu tulikuwa tushapoteza gharama na hatukuwa na cha kumfanya.Niliumia sana kwasababu laiti kama Kamugisha angenisikiliza tangu mwanzo nilipomshitua pengine kusingetokea hayo yote.
Mtanzania "Kama huyu jamaa ndiye mlidhani ni mganga ndugu zangu hapo mmetupa hela yenu,hapa Kirungu kuna matapeli wengi sana wanaojifanya waganga na wanawaibia sana watanzania,kitu kibaya ni kwamba,ukikutana na watanzania ukijaribu kuwashauri wanadhani unawazibia,haya sasa na nyie mjionee wenyewe!"
Aliendelea "Halafu wengi huwa wanajifanya kuongea lingala ili kuwachanganya kabisa,hapa Kirungu lugha ni mbili tu,kiswahili na French ukiona mtu anazungumza lingala ujue huyo ni tapeli kutokea huko Kisansha!"
Kamugisha "Kwahiyo kaka hapa Kirungu hatuwezi kupata mtaalamu mzuri akatusaidia?"
Mtanzania "Hapa wataalamu walikuwepo zamani ila sasa wengi walishahamia kwenye miji mingine,mi kiukweli ningekuwa namfahamu hata mmoja ningewaelekeza ila kiukweli siwajui!"
Baada ya mazungumzo yale tuliondoka zetu kurudi kule kwenye ile nyumba ya nyasi ya mdogo wake na yule tapeli kwenda kuchukua mabegi yetu ili turudi Guest kisha tuangalie nini cha kufanya;tulipofika wakati tukiwa tunafunga mlango tulimpigia simu Jentre aje achukue ufunguo amrudishie tapeli mwenzie.Tukiwa hatuna hili wala lile alikuja mwanamke mmoja na mwanaume ambao walipofika hapo tulipokuwa tumesimama tukimsubiri Jentre ili tumkabidhi funguo sisi tuondoke walitusalimia na wakajitambulisha.
Mwanamke "Mimi naitwa Mama Bojee,ndiye naangalia bantu bingi kuu huu mutaa na huyu anaitwa Dofili ni Presdaa wa localitee"
Sasa kwa mujibu wa yule mama ni kwamba,yeye alikuwa ni kama mjumbe wa mtaa na yule jamaa aliyeongozana nae alikuwa ni mwenyekiti wa mtaa tuliyokuwepo.Baada ya kupata taarifa kwamba kuna watanzania tupo pale kwenye ile nyumba kumbe walikuwa kututafuta mida fulani lakini tulipishana nao,sasa wakati tukiwa tunafunga mlango tuondoke ni kama waliitwa ili waje kabla hatujaondoka.
Walitutaka tuongozane hadi ofisini ambako tungeonyesha documents zetu na kuulizwa maswali kadhaa.
Mwanamke "Mnayo Madocumenshoo?"
Baada ya kutaka kuona documents zetu kila mmoja alitoa zake akawa zinakaguliwa;walipoona kila kitu kipo sawa walikuwa wanatuuliza documents zetu zinaonyesha tungekaa Guest hadi siku tunaondoka,sasa walitaka kufahamu ni kwanini tulienda kuishi kwenye mtaani kama wakongomani wakati hatukuwa na vibali.Kama nilivyosema hapo awali,wakongo na viongozi wao wanapenda sana fedha,ukijichanganya akapata upenyo wa kukukamua atakukamua kwelikweli.Baada ya kuona wanaweza kutuletea shida,Kamugisha ikabidi amueleze yule mama ukweli angalau kuepusha mambo mengi.
Mwanamke "Mimi niko kujua tu kwamba hawa Watanzanii bhamekuya kwa monganga "
Aliendelea "Mmesaidika"
Kamugisha "Hapana"
Mwanamke " Juu mimi ujuanga hapa Kirungu hakuna Monganga wa ukweli,bhanganga bhako huko mu villejoo"
Aliendelea "Nyie mko mtaka mufumu wa kazi gani?"
Kamugisha "Atusaidie mambo yetu"
Yule mwanamke kuna mtu alimpigia simu akawa amemwambia aje pale ofisini kwake,pamoja na yote hayo lakini yule mama alituambia tumpatie hela kidogo ya mboga,Kamugisha alimpatia elfu 10 ya Congo na alifurahi sana.
Yule jamaa aliyepigiwa simu alipokuja akawa anazungumza na yule mwanamke lugha ya French iliyochanganyikana na baadhi ya maneno ya kiswahili,kumbe yule jamaa aliitwa kama mtu atakayekuwa mfasiri wa lugha maana yule mama kiswahili fasaha ni kama kilimpiga chenga.
Jamaa "Mama leki anasema,kama nyie iko mtaka mganga nendeni Manono kule iko mama mmoya mwenye titi moya mtasaidika"
Aliendelea "Mama leki anasema msisaidike na waganga wanaume kwasababu wengi hawajui kitu,mkimpata huyo mama atawasaidia sana"
Kwa mujibu wa maelezo ya yule jamaa akiwa kama mfasiri wa yule mama ni kwamba,kuna mganga mmoja anapatikana kwenye Mji uitwao MANONO,ule mji kuna mwanamke mmoja ambaye alisema ana Titi moja na ni mganga kwelikweli,pia akasema waganga wa kweli wengi wa Congo ni wanawake,wanaume wengi wao ni matapeli.
Boss wangu Kamugisha alipopata hayo maelezo ni kana kwamba alipagawa na alitaka afike muda huo huo hapo Manono,nilikuwa nikimtazama usoni unamuona ni mtu ambaye alipata faraja mpya baada ya ile ya mwanzo kupotelea mikononi mwa matapeli.
Kamugisha "Muulize mama huko Manono kuna umbali gani na huyo mama anaitwa nani?"
Jamaa "Mama leki anasema,Manono ni mbali na mtagharamika kwa siku 2 njiani,juu unajuaga huku kwetu ni mamotaa tu,hakuna gari njia si mzuri"
Aliendelea "Mama huyo anaitwa Mama Nionso"
Kamugisha "Kwahiyo tukienda hapo Manono tukimuulizia mama Nionso tutampata"
Jamaa "Hapo anafahamika ku vilejoo muzima,hamuwezi potea"
Baada ya majadiliano ya muda mrefu pale ofisini,yule mwanamke alituambia kama tukitaka kwenda aje atuandikie barua ambayo itatusaidia kuepukana na usumbufu tuwapo kule.Tuliondoka tukaenda kumpelekea Jentre ule ufunguo kisha tukajikataa zetu kurudi Kule Guest,Jentre kwakuwa alikuwa anaelewa alichokifanya hakutaka kabisa kutusumbua,tulipompa ufunguo aliondoka kinyonge sana!.
Kamugisha "Mwanangu sasa unaonaje?,vipi tuelekee huko Manono tukamcheki huyo Maza?"
Mimi "Pesa bado unayo kaka?"
Kamugisha "Kuhusu pesa usiwaze mdogo wangu,nitabadili nyingine kama ikihitajika"
Mimi "Kama pesa ipo hakuna tatizo tunyooke tu kwa huyo Maza".
Kwakuwa usafiri wa kule huwa ni Bodaboda kwa kiasi kikubwa kwasababu ya Ubovu wa Barabara,tuliamua kumtafuta Bodaboda mmoja tukazungumza nae ili kumuuliza sisi kufika hapo Manono ingetugharimu bei gani?.
Bodaboda "Manono ni mbali,nyie mtanipatia laki 3"
Kamugisha "Laki 3 !?"
Aliendelea "Mbona pesa nyingi sana hiyo!"
Bodaboda "Ulizeni mamotaa wengine kama mnadhani nawadanganya!"
Tulijaribu kutembea na kuwauliza Bodaboda kadhaa wengi walituambia bei ni hiyohiyo,kuna mmoja yeye alituambia tumpatie laki 250 ili atupeleke huko Manono.Baada ya jamaa kukubaliana na ile Bei tulirudi pale kwa mtanzania tena kubadili Dollar kadhaa hivyo tukawa na hela ya kutosha.Tukawa tumekubaliana na yule Bodaboda Kesho yake tuianze safari.
Kabla ya kuondoka tulienda kwenye ofisi ya yule mwanamke akatuandikia documents akaigonga na muhuri ili tutakapofika hapo Manono tusipate usumbufu wa hapa na pale.
Tunamshukuru tukaamka salama na safari ya kuelekea kwenye Mji wa Manono ikachukua nafasi.
Inaendelea.................
Wanaenda kupigwa tenaBado Safari inaendelea tu...
[emoji23][emoji23] Kweli ujue au we unaielewa kipenzi[emoji23][emoji23][emoji23]
Ndio dizain ya DECI sijui D9 Mara KaryandaThey say short ways are the wrong ways. .
Yaan story za kwenda mbele kurudi nyuma huwa zinahitaji umakini mno na zinachosha kusoma[emoji23][emoji23] Kweli ujue au we unaielewa kipenzi
Hahaha 😆 naona watu hawajifunziNdio dizain ya DECI sijui D9 Mara Karyanda
[emoji23][emoji23] Sasa me na ubashite huu hapana unakuwa unazidi kunichosha yaani naomba kwa akinyi asiendelee ujue unasoma tu kitu ila huelewi kitu ndio mimi kuleYaan story za kwenda mbele kurudi nyuma huwa zinahitaji umakini mno na zinachosha kusoma
Huhuuu[emoji23][emoji23] Sasa me na ubashite huu hapana unakuwa unazidi kunichosha yaani naomba kwa akinyi asiendelee ujue unasoma tu kitu ila huelewi kitu ndio mimi kule
Usicheke, waonee huruma. 😄😀😆😅🤣😂