Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

Umeshawahi kufika Sumbawanga? Kutokea Mbeya ?

Muache ubishi usio kuwa na kichwa Wala miguu, ujuaji wa kipumbavu

Ni hivi ukitoka Mbeya unafika Tunduma border then unakata Magharibi unaelekea Sumbawanga

Mwandishi Yuko sahihi sana

Umeshawahi kufika hata zambia mkuu ama unashabikia tu ujinga?
 
Huyu ndiye mfano wa huyo koloekole baada kichunwa ngozi,nyama yake ikabanikwa na kichomwa kisha kuliwa na wale jamaa walioitafuta,kisha ngozi yake ikaanikwa juani ilipokauka ikatengenezwa ndipo tukaambiwa itakuwa inaenda kuiba pesa benki inatuletea.

Kamugisha alivyokuwa na hamu na pesa ya wizi akawa amesema pesa ya kwanza tutakayomtuma huyo kolekole itakuwa milioni 100 ili tugawane pasu kwa pasu [emoji23][emoji23].

Kilichotukuta sitokaa nisahau.

Myama mwenyewe anakwato sijui vidole vitatu sa ayo mamilion angebebea kwenye nini!!
 
Umeshawahi kufika Sumbawanga? Kutokea Mbeya ?

Muache ubishi usio kuwa na kichwa Wala miguu, ujuaji wa kipumbavu

Ni hivi ukitoka Mbeya unafika Tunduma border then unakata Magharibi unaelekea Sumbawanga

Mwandishi Yuko sahihi sana
Watanzania wengi elimu zetu hazina msada wowote,mfano mnzuri kama huyo
 
Yaani ufike Tunduma boda kisha uende tena sumbawanga [emoji276]chai hii sio poa,Ikifika Tunduma ndio boda ya nakonde ilipo then unaingia zambia hadi kapiri mposhi ndio unaingia congo
Yaan kama baba Yako alikusomesha unapaswa kumlipa fedha zake haraka sana,màana kile ulichosomea hakina msaada wowote kwako
 
Huo wa ndagu matokeo yake si ndio kuambiwa utoe kafara mkuu, au wenyewe uko tofauti kidogo
Wenyewe ni tofauti kidogo , unapewa mtihani sio wa kuua ni mtihani tu mdogo ukifanikiwa unakuwa tajiri

Mfano, unaambiwa kuwa utakutana na KAMBA njiani uichukue Urudi nayo kwa Mganga lakini unaenda unakutana na Nyoka mkubwa ukiwa jasiri na ukakumbuka mkamate ukimshika tu anakuwa KAMBA

Wengi wanashindwa sababu mazingira ya jaribio ni ngumu kuhimili au kukumbuka ,

Bariadi wengi wametajirika kwa Ndagu

Sent from my CPH2217 using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA TISA




Ilikuwa njia yenye misukosuko hadi kufanikiwa mji wa Manono,haikuwa shughuli nyepesi hata kidogo.Tulivyofika hapo kijijini kazi ya kumtafuta Mwanamke mwenye titi moja aliyefahamika kama Nionso ilichukua nfasi.Tuliuliza kila mahali na hatimae tukaelekezwa nje kidogo upande wa mashariki mwa mji ule ndipo alikuwa akipatikana.

Nilitamani na mimi sikuhiyo nikamuone huyo mwanamke ambaye walidai alikuwa na titi moja anavyofanana,nilikuwa ninashauku sana.

Kweli tulifanikiwa kufika hadi kwake lakini muda tulioenda ilikuwa ni kipindi cha msimu wa upikaji wa pombe,hivyo alikuwa bize sana na tuliambiwa na msaidizi wake yapasa kumsubiri hadi atakapomaliza.Tulikaa pale kwenye mji wa huyo mama kwa muda wa siku 3 ndipo alituita akahitaji tufanye naye mazungumzo.Yule mwanamke ingawa walisema alikuwa na titi moja lakini mimi nilijaribu sana kumchunguza sikufanikiwa kuona chochote,unajua mwanamke maumbile yake ya kifuani huwa yanaonesha tu hata kama akivaa nguo kiasi gani,mimi nilipokuwa nikimtizama nilikuwa nikiona sehemu ya miinuko ya matiti yote mawili.

Mama Nioso "Karibu sana wanangu"

Sisi "Ahsante sana mama"

Mama Nioso "Mumetoka Tanzanie mpaka hapa kwangu,nimewaona wakati mumekuwa kwa njia"

Aliendelea "Mimi kusasa niko kupika pombe"

Aliendelea kusema "Nimeona shida yenyu nyinyi mmekuya nayo"

Aliendelea kusema "Nyinyi mmko wachafu sana kumwili paka nibhaoshe muwe bien ndiyo mtapata mapesa mingi"

Yule mama aliendelea kuzungumza tukiwa tunasmikiliza,sasa alichokuwa ametuambia ni kwamba,wakati tunaenda hapo kwake alikuwa akifahamu na alituona,alisema tumefata kufanikiwa ili tupate pesa.Alituambia hatuwezi kufanikiwa kwasababu miili yetu ilikuwa michafu ni mpaka tuoshwe kwa dawa ndipo atufanyie kilichokuwa kimetupeleka.

Kumbe kila mtu aliyekuwa akifika hapo kwake kunywa pombe na vyakula wanavyokula wao halikuwa ombi bali ilikuwa ni lazima.

Alimwambia msaidizi wake achimbe mashimo mawili akishamaliza amwambie,yule msaidizi wake alimchukua mtu mwingine wakawa wameenda kando ya ile nyumba kulikokuwa na mashamba ya mihogo,ilikuwa kama mita mia kutoka kwenye ule mji.Baada ya kuchimba yale mashimo mawili yenye kimo cha futi tatu kila moja alirudi akamwambia yamekamilika!.

Mama Nioso " Mtalala kwenye mashimo kwa muda wa siku tatu nyinyi nyote bawili"

Aliendelea kusema "Ikashakamilika nitafanya dawa ndiyo mtapata pesa"

Usiku ule ilichemshwa dawa kwenye sufuria kubwa ambalo kila mtu alipaswa kukaa ndani ya sufuria hilo na kuanza kuoshwa dawa huku ukitandikwa na majani ya mti.Kiukweli haikuwa kazi ndogo hata kidogo kuvumilia vile viboko vya yale matawi kwasababu tuliambiwa dawa hiyo ndivyo ilipaswa kufanywa,tofauti na hapo kusingefanyika chochote.Sasa baada ya zamu yangu akafuatia na Kamugisha.

Hatukupaswa kuvaa nguo kabisa baada ya kutoka kwenye lile sufuria kubwa lililokuwa na dawa;Baada ya hapo alituongoza yeye mwenyewe yule mama hadi kwenye yale mashimo yaliyokuwa yamechimbwa mchana,yale mashimo yalikuwa kama makaburi.Alituambia kila mmoja aingie kwenye shimo lake na tulale chali,hatukupaswa kabisa kuchungulia nje wala kuamka hadi kutakapo pambazuka.

Ndugu zangu ile hali haikuwa ya kawaida na ndiyo maana nipo hapa kuwasanua watanzania wenzangu kuepukana na waganga matapeli wa nchini Congo.Kuna watu huwa hawasikii wala hawaelewi mpaka waone kwa macho yao,sasa msiposikia na kuelewa shauri yenu,mimi kazi yangu ni kuwaambia tu.

Asikwambie mtu ule usiku ulikuwa mrefu kama mwaka,nilikuwa najiuliza endapo kama tukifanyiwa kitu kibaya ni nani atakayefahamu huko Tanzania?,Kwakuwa ilikuwa ni urafi wangu na tamaa ya pesa niliamua litakalokuwa ngoja liwe.Tulilifanya lile zoezi kwa muda wa siku tatu mfululizo tena tukiwa uchi kama tulivyozaliwa,kulikuwa na baridi kali sana lakini hatukuwa na namna,nakumbuka nilipotoka huko Congo nilikuwa mweusi mithili ya mchoma mkaa,nilikaa ndani wiki 2 nzima angalau joto la dar linitakatishe kidogo.

Basi bana,Baada ya kukamilisha lile zoezi la kulala kwenye yale mashimo ikiwemo na kupigwa chale za kufa mtu,yule mama alituambia tumeshafuzu mtihani wa mafanikio na tujiandae kutajirika.

Mama Nionso "Kesho nahitaji kuwatuma watu huko mashambani wakawatafutie kolekole,huyo kolekole atakuwa anawaletea mbongo mingi,ila mkishapata hela mnikumbuke sana wanangu"

Kamugisha "Mama kolekole ni nani?"

Mama Nionso "Kolekole ni mnyama mdogo,huyu kazi yake itakuwa kuiba hela kwenye benki na kuwaletea nyinyi"

Aliendelea kusema "Mtanipa elfu 20 niwape vijana wakamtafute"

Kamugisha "Sawa mama"

Baada ya maelekezo yale,Kamugisha alichomoa hela akampatia yule mwanamke kisha akawatuma vijana kwenda kumtafuta yule Mnyama.Mimi kiukweli moyo wangu ulikuwa unakataa na niliona kabisa tunaibiwa kwasababu,kama mtu alikuwa na uwezo wa kutengeneza mnyama wa kwenda benki kuiba kwanini yeye anaishi kwenye lindi la umasikini?,Kuna vitu nilikuwa najiuliza sana lakini kwasababu Kamugisha alikuwa na imani kubwa sana kwa yule mama sikutaka kumtahadharisha,nilikaa kimya ili ajionee mwenyewe.

Wale jamaa walifanikiwa kuleta ka mnyama ka moja hivi kalikofanana na Pimbi (Hyrax) kakiwa kwenye Ndoo kubwa,kalikuwa na meno mawili makubwa mdomoni kama Sungura.Yule mama alituambia mambo mengi sana kanakofanya kale ka mnyama.

Walianza kukachuna kukatoa ngozi na walipomaliza ile ngozi ilianikwa juani kwa muda wa siku 2 ikawa imekauka kabisa,ile nyama waliila wale jamaa kwa kuichoma na kuibanika.

Ile ngozi ya yule mnyama ilipokauka ilifungwa vijiti fulani hivi mbele,katikati na nyuma vilivyokuwa vimekaa kama sigara,yule mama alitupatia maelekezo ya kwamba tutafute nyumba itakayokuwa karibu na benki yeyote na tukishaipata tutachimba Shimo lenye urefu wa kiganja cha mkono na kisha tutawasha vile vijiti vitatu kwenye ngozi ya yule mnyama,tutatamka maneno aliyokuwa ametuambia na kisha ile ngozi itaondoka itaingia shimoni na ikishafika shimoni itabadirika katakuwa kale ka mnyama kataenda kwenye benki tuliyomtuma katachukua kiasi tulichoagiza kisha kataleta.

Kwakuwa pesa katakayoleta itakuwa ya moto,yule mama alituambia tutakuwa tunaimwagia dawa aliyokuwa ametupatia kisha tutaanza kuzichukua na kuzitia kwenye mabegi.

Kiukweli kwa namna alivyokuwa ametuambia tulikuwa tunajiona ni matajiri ingawa hatukuwa na pesa bado,tulikubaliana na Kamugisha ya kwamba,zoezi hilo tungeenda kulianzia kwenye benki za pale Sumbawanga ili hadi kufika Dar tushakuwa madoni wa kufa mtu hata Bakhresa akasome 😂😂😂😂

Basi bana,yule mama alituomba tumpatie shilingi laki tatu kwa kutufanyia lile zoezi;Kamugisha alitoa pesa akawa amempatia huku sisi tukijawa na shauku ya kuwa matajiri kwa wizi wa fedha za watu kupitia ushirikina wa kolekole huko kwenye mabenki.

Mungu ni mkubwa tulifanikiwa kuvuka maji na tukafika Tanzania salama kabisa.Tulipofika Sumbawanga tulitafuta chumba tukapanga kwa muda wa mwezi mmoja ili kulifanikisha lile zoezi letu.

Yule mama alikuwa ametuambia kile kingozi kabla ya kukifanyia kazi tukinunulie mahindi pamoka na utumbo wa kuku kile ndipo kiingie shimoni kikifika shimoni ndipo kinabadrika kinakuwa ki mnyama kilicho hai.Wakati yule mama anatupatia yale masharti kiukweli nilikuwa najiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,Tangu lini ngozi ikala mahindi?,Tangu lini ngozi ikala utumbo wa kuku?,yaani ameshindwa kutupatia mnyama mwenye uhai ambaye ndiye angekula hivyo vitu yeye anatupatia ngozi anasema inakula,mimi kama kawaida nilikuwa nina mashaka sana ila mwenzangu alikuwa mwenye furaha sana kana kwamba alikuwa ametolewa akili,sasa kwakuwa mimi nilikuwa si mtoa hela sikutaka kumshauri chochote nikaamua nikae kimya.

Tuliponunua hayo mahitaji sasa zoezi la kuchimba shimo kwenye kile chumba likaanza,kumbuka tuliambiwa tuchimbe kishimo kidogo tu kilichokuwa na urefu wa kiganja cha mkono.Baada ya kukamilisha tukakipiga kiberiti kwenye vile vijiti kama tulivyoelekezwa na yule mama na kisha tukatamka maneno aliyokuwa ametuambia.

Ajabu ni kwamba hakuna chochote kilichotokea,tulifanya lile zoezi siku nzima laki holaaaaa,Jamaa yangu Kamugisha alichanganyikiwa kabisa.

Kamugisha "Una uhakika mdogo wangu hatujakosea ?"

Mimi "Kaka tulichoelekezwa ndicho tunakifanya,hapa hamna kitu kaka tumepigwa"

Kamugisha "Mi siamini,hebu ngoja tulale halafu kesho pia tuendelee na zoezi"

Palipokucha zoezi lile lilichukua nafasi lakini hali ilikuwa ileile,hakuna chochote kilichotokea.

Baada ya kuona tunapoteza muda tu kule Sumbawanga,tuliamua kurudi Dar es salaam na kile kingozi na jamaa kukichukua kwenda kuendelea na zoezi nyumbani kwake lakini hadi leo nikimuuliza huwa anabaki kufyonza na kusonya kana kwamba mimi ndiye niliyemuingiza chaka 😂😂

Jamaa hajakata tamaa anasema anajaribu kupepeleza ili tuelekee tena huko Zambia maana ameambiwa huko wapo wataalamu wa kumpatia utajiri.

Mimi kazi yangu nitakuwa ni kuwasimulia tu ndugu zangu.Safari ya Zambia ikiwa tayari nitawajulisha[emoji23].


KUWENI MAKINI NA WAGANGA WA KONGO KWANI WENGI MATAPELI.
Kwa niaba ya wasomaji wako nichukue nafasi hii kukushukuru kwa simulizi yenye mafunzo yenye kutukumbusha kwenye hatua za maisha!

Hapa kikubwa ni kuwa makini na WAGANGA WOTE TU SIO WA KONGO PEKE YAKE KWANI NAO WAPO KWENYE UTAFUTAJI
 
Huyu ndiye mfano wa huyo kolekole,baada ku
chunwa ngozi,nyama yake ikabanikwa na kuchomwa kisha kuliwa na wale jamaa walioitafuta,kisha ngozi yake ikaanikwa juani ilipokauka ikatengenezwa ndipo tukaambiwa itakuwa inaenda kuiba pesa benki inatuletea.

Kamugisha alivyokuwa na hamu na pesa ya wizi akawa amesema pesa ya kwanza tutakayomtuma huyo kolekole itakuwa milioni 100 ili tugawane pasu kwa pasu [emoji23][emoji23].

Kilichotukuta sitokaa nisahau.
Si umpleke kwa bibi ngende

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom