SoC02 Namna wimbo wa taifa tunavyouchukulia ni kukosa uzalendo au ni aibu ya kutokujua?

SoC02 Namna wimbo wa taifa tunavyouchukulia ni kukosa uzalendo au ni aibu ya kutokujua?

Stories of Change - 2022 Competition

Wenger_tz

New Member
Joined
Aug 1, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Wimbo wa taifa ni moja ya nguzo muhimu sana katika kuimarisha uzalendo na umoja wa taifa lolote duniani,
Kwetu Tanzania wimbo huu huimbwa mara nyingi sana kwenye mikusanyiko ya kitaifa pamoja na sehem maarufu zaidi ikiwa ni uwanjani inapocheza time yetu yeyote ya Taifa.

Ukweli ukiangalia mataifa mengine yanavyoupa heshima wimbo wao wa taifa unaona uzalendo wa hali ya juu mno, jinsi wanavyoimba kwa hisia, kwa sauti na kwa ushirikiano.

Lakini taifa letu mara zote nilizoona wakiimba (Tukiimba), sisi huwa kwanza hatuna mkao mzuri wa kuimba yaani hakuna tofaut ya kusimama ukiwa unaimba wimbo wa taifa na ukiwa unapiga story na rafiki, pili huwa hatutoi sauti wala kinywa hakiendani na kinachoimbwa, yaan tunakuwa kama wagonjwa hivi,

Sasa mimi najiuliza hiv ni kwamba hatujui huo wimbo au ni kwamba level zetu za kujiamini ni ndogo kiasi kwamba hata kuimba tunaogopa kukosea?

Cha ajabu sana ni kwamba hata viongozi wa serikali tena wa ngazi za juu na wenyew ndo hata mdomo hawafungui. (Uzalendo which?)

Ebu tazama wachezaji wetu wa timu ya taifa wanavyoimba wimbo wa taifa , utaishia kuskia mlio wa bendi tuu na wenyew hata mkao wao haukuonyeshi heshima kwa wimbo wenyewe.

Jaribu kupitia mchezo wa Chan tulipocheza na somalia utadhani sis ni wagonjwa yaani , Somalia waliimba wimbo wao kwa heshima sana.

1. ni wimbo wetu umepooza kiasi kwamba hauimbiki kwa hisia ?

2. Ni wananchi wenyewe hatujui kuimba wimbo huo vizuri ndo mana tunakuwa tunaufuatisha kimya kimya?

3. Au ni lile tatizo letu watanzania tulio wengi tunakosa kujiamini kwenye hadhara mana kwa maoni yangu nadhani Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo raia wake hawajiamini kwanye hadhara ( lack of confidence in public speaking) kwa kiwango cha juu sana.

4. Au ni hatujui maana yake?

Heshima kwa alama za taifa letu ni ya msingi sana, na wimbo ukiwa moja ya alama za taifa pamoja na alama nyingine kama bendera na nembo ya taifa, tukivipa heshima ya juu itstusaidia kupunguza baadhi ya mambo kama rushwa na kuongeza thamani ya huduma za kiserikali/kitaifa, mana imefika sehem ambayo mtu kuitumikia serikali ni kwasababu tuu America kazi nzuri zaid private,uzalendo uko wapi hapa?

Kwanini hatuoni fahari kutumikia taifa letu, ? Yote hii ni kukosa uzalendo ambao hujionyesha wazi katika kiwango cha heshima tunayozipa alama zetu za taifa.

NM.( ndoto za mchana)
Mimi ningekua rahisi,
1. Ningehakikisha kila kusanyiko ninalokuwepo au analokuwepo waziri yeyote au mkuu wa mkoa nahakikisha alama hizi za taifa zote zipo na tunazitumia nikiwa mimi kama mfano.

2. Ningehakikisha moja ya kigezo cha mchezaji kuitwa time ya taifa ni kuujua na kuweza kuimba vizuri wimbo wa taifa. Maana ukiwaangalia wachezaji wetu huu mda wa kuimba daaah hadi unajiuliza wametekwa au wamelazimishwa?( Serikali hairuhusiwi kuiingilia TFF lakini huwezi kutenganisha hivi vitu)

Au tunatumia aman tuliyonayo vibaya mana sis ni Don care kwenye mambo ta kitaifa mpaka sio vizuri.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom