Poleni na changamoto za hapa na pale, wanajamii wenzangu.
Naomba kupewa mwongozo kwenye hili suala (ruksa kunifokea).
Ukiachana na changamoto nyingine, suala la ngono nalo linaongoza kuharibu akili na maisha kiujumla hasa kwa vijana wa kiume wa miaka 18-29. Huu sio utafiti rasmi ila naongelea nilichokiona kwenye jamii sehemu mbalimbali nilizoishi.
1: Chaputa
Mara tu baada ya kuingia kwenye balehe, nilijikuta nimeingia kwenye uraibu wa masturbation. Hii tabia nimekaa nayo kwa miaka 5-6 mpaka nilipokuja kujichunguza na kugundua inaniathiri kisaikolojia. Sasa hivi ninautafuta mwezi wa tatu tangu nilipoacha huu mchezo na sina mpango wa kurudi huko haijalishi nini kitatokea.
2: Kulipia Ngono
Wiki za mwanzo baada ya kuacha masturbation, nilijikuta hamu ya ngono inaongezeka kupita maelezo na ubaya ni kwamba sikuwa na mahusiano yoyote. Hali ilizidi kuwa mbaya, ikafika hatua siwezi kufanya kazi vizuri. Nia ya kutafuta mtu wa kuwa naye kwenye mahusiano ikawa ngumu kidogo kulingana na namna nilivyojizoesha.
Ndipo nikapata wazo la kufanya ngono za kulipia wakati nikiendelea kumtafuta atakayenifaa kwenye safari ya maisha. Tinder, Badoo, na Tagged ndiyo zikawa sehemu zangu kubwa. Karibu kila wikiendi, naita mtu anakuja nyumbani namaliza nachohitaji, anasepa.
Hii tabia imenifanya niutelekeze hata ule mpango wa kutafuta wa kudumu, kwa sababu niliona kipengele cha kujuana kinanipotezea muda.
Nimelileta hili kwenu kwa sababu nataka kuachana na hizo tabia. Nimeona zina madhara kiuchumi, kisaikolojia na kijamii kiujumla.
Naomba mnipe mbinu ya kutumia kupambana na hamu ya ngono wakati nikiendelea kutafuta ubavu wangu wa pili tuoane.
Naamini ushauri wenu utanisaidia mimi na vijana wengine wengi walionasa kwenye hili tatizo.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.