SoC04 Namna ya kudhibiti matumizi holela ya dawa za binadamu mtaani

SoC04 Namna ya kudhibiti matumizi holela ya dawa za binadamu mtaani

Tanzania Tuitakayo competition threads

jemzzle

New Member
Joined
Aug 12, 2016
Posts
4
Reaction score
3
Dhana ya kufanya biashara kwenye maduka ya dawa Muhimu (DLDM) inahatarisha maisha ya wananchi wanao kimbilia kupata huduma kwenye maduka haya .Maduka ya dawa yamerahisisha huduma ya upatikanaji wa dawa za binadamu wakati huohuo yameongeza hatari ya kupata madhara yatokanayo na dawa hizo.Hii inatokana na Mosi, uhitaji wa faida kubwa kutoka kwenye mauzo ya dawa kwa wamiliki, pili, kukosekana kwa wanataaluma wabobezi wenye kuishi viapo vyao kwenye maduka haya.

Hata hivyo dawa za binadamu zinaendelea kutokua salama hata katika baadhi ya taasisi za serikali ambapo majukumu ya usimamizi wa dawa yamekaimishwa kwa wanataaluma wasio wabobezi.Madharani, si ajabu kukuta katika Hospitali, zahanati au vituo vya afya Manesi,matabibu au wasaidizi wengine wa afya wakitoa dawa kwa wagojwa huku sheria za Nchi zikiwa zinawalinda.

Katika andiko hili haimaanishi kuwa wagojwa hawatopona ikiwa watapewa dawa na Manesi,matabibu au wasaidizi wengine wa afya, rahasha bali ni kuonyesha jamii kuwa utoaji wa dawa kwa mgojwa ni hatua ndogo sana na ya mwisho ambayo nyuma yake imetanguliwa na mlolongo mrefu wa udhibiti na usimamizi wa ubora wa dawa lengo likiwa kwamba ile hatua ya mwisho ya kumpatia dawa mgojwa inapofikia, dawa iwe imeendelea kubaki salama tangu ilipozalishwa.

Kwa muktadha huu dawa za binadamu zinabaki kuwa salama endapo zitakua chini ya mikono ya wanataaluma wa dawa ambao wameandaliwa kushughulika na dawa tangu zinapotengenezwa hadi zinapomfikia Mgojwa.

Miongozo ya utoaji dawa kwenye maduka ya dawa imeainisha orodha ya dawa ambazo mgojwa anaweza kupata dawa kwenye duka la dawa bila kua na cheti cha daktari ambapo atanunua dawa kulingana na ushauri tu wa muuza dawa .Dawa za kifua kama Mucolyn, Zecuf, Menthodex, Benylin hazihitaji cheti cha daktari na mgonjwa anaweza kununua kama anavyo nunua peremende kwa Mangi.Hii inatokana na athari ndongo zinazoweza kuhatarisha maisha.Zingine ni dawa za mzio(allergy), maumivu na homa kama vile cetirizine, loratadine, toff plus, Paracetanol ,hyoscine n.k ambazo zinatumika kama msaada wa haraka kwa mgonjwa.

Orodha ya Dawa hizi ni fupi na faida yake ni ndogo kuendana na gharama za uendeshaji wa maduka ya dawa muhimu. Hali hii inapelekea Wafanyabiashara wengi kuamua kuuza dawa zilizo kwenye orodha ambayo utoaji wake unahitaji cheti cha Daktari. Hapa ndipo shida kubwa inaanzia kwani baadhi ya dawa zinazohitaji vipimo vya maabara na historia ya matibabu ya mgojwa kumwezesha Daktari kuandika cheti cha dawa zinafaida kubwa kwa Wauzaji.

Dawa zilizoainishwa kwenye orodha hii ni kama (nitatumia majina yaliyozoeleka mtaani) Azuma, Njoi, Vega, Pen v, ciprofloxacilin, Duo cotexin, ALU, Primolut N, P2, Misoprostol, Powercef injection n.k ambapo dawa hizi zinafaida kubwa na Wauzaji wa dawa watamshawishi mgojwa kwa kila namna uweze kununua ili watengeneze faida huku wakihatarisha afya ya mtumiaji.

Athari zinazoweza kumpata mgojwa kwa kutumia dawa hizi ni kama kupata usugu wa vimelea vya magojwa ambapo itapelekea kuhitaji dawa za madaraja ya juu zaidi kujitibu kwa maambukizi ya bacteria wa kawaida hadi atakapo yamaliza madaraja yote ya juu ya dawa ambayo bei ya dawa zake ni ghali na zikigoma atakufa, mataizo ya moyo, Figo, ini na viungo vingine vya mwili kwani mfumo wa uchakataji dawa mwilini unahusisha viungo nyeti mwilini.

Si ajabu kwa siku za karibuni kumuona kijana wa miaka 30 akiwa na kansa,presha,upungufu wa nguvu za kiume, ganzi, ugumba n.k ambapo kwa namna moja au nyingine takwimu zake zinaweza kua zimepandishwa na haya matumizi holela ya dawa. Muuza dawa hatakutahadharisha yote haya maana anataka pesa ya haraka haraka. Jamii inatakiwa itambue athari kubwa za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi holela ya aina mbalimbali za dawa bila kufata matakwa ya kitaalamu ya tiba.

Suluhisho;

Serikali ipitie miongozo inayoruhusu watoa dawa wasio wanataaluma wa dawa kusimamia maduka ya dawa hospitalini, kwenye zahanati na vituo vyote vya afya. Pia serikali iajili wahusika wa kutosha wenye taaluma yao ili wasimamie huduma za dawa na kupunguza madhara yatokanayo na matumizi ya dawa.

Biashara ya uuzaji wa dawa kwenye maduka ya dawa muhimu (kwa sababu haihusishi dawa moto) isimamiwe na Baraza la famasi chini ya uratibu wa ya serikali za mitaa ambapo mfanyabiashara awajibike kuwasilisha taarifa za kitaaluma za mtoa huduma zinazoaksi kufuzu mafunzo ya utoaji dawa. Maduka yote ya dawa yapate huduma za ugavi kutoka kwenye Famasi kwa namna ambayo kila famasi iliyosajiliwa itapewa maduka ya dawa ya mtaani itayoyahudumia. Pia Serikali za mitaa ziwezeshwe namna ya kuhakiki wanataaluma hawa kupitia mafunzo chini ya baraza la famasi.

Biashara ya uuzaji wa dawa kwenye maduka makubwa (Pharmacy business - inahusisha dawa moto), kama ilivyo kwenye sheria za baraza la famasi, biashara hii ni biashara ya Mfamasia, basi serikali itoe ruzuku kwa Wafamasia kama mitaji ya kuanzia Biashara na wananchi wote wenye nia ya kufanya biashara ya dawa za binadamu wawekeze kwenye uuzaji wa dawa kwa jumla kuwauzia wafamasia. Hii itaondoa ile dhana iliyopo kwasasa ya wafamasia kutundika vyeti. Pia, hii itasidia kuweka bei kikomo ya dawa kama ilivyo kwenye mafuta huku tukiokoa afya za watanzania.

Taratibu za vyeti vya dawa vya daktari na ugavi wa dawa kwenye maduka yote ya dawa ziende kidijitali kuwezesha ulalo wa taarifa za dawa kwenye kila duka.
 
Upvote 2
Kwa muktadha huu dawa za binadamu zinabaki kuwa salama endapo zitakua chini ya mikono ya wanataaluma wa dawa ambao wameandaliwa kushughulika na dawa tangu zinapotengenezwa hadi zinapomfikia Mgonjwa.
Mnyororo mzima, hakika.

biashara hii ni biashara ya Mfamasia, basi serikali itoe ruzuku kwa Wafamasia kama mitaji ya kuanzia Biashara na wananchi wote wenye nia ya kufanya biashara ya dawa za binadamu wawekeze kwenye uuzaji wa dawa kwa jumla kuwauzia wafamasia
Wazo zuri la public funding of a service of public interest. Na ndio maana maduka yenyewe yakaitwa community pharmacy. Sio bure bure tu.
 
Back
Top Bottom