Namna ya kufanya ili nirejeshewe pesa ninazomdai mtu Shilingi milioni 105

Namna ya kufanya ili nirejeshewe pesa ninazomdai mtu Shilingi milioni 105

Crimea Bridge

Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
51
Reaction score
152
Kuna mdau alikuwa ni mteja wangu, hapa Kariakoo. Nilikua nampa mali kauli ili akauze, mara ya mwisho kabisa uyo mteja alinitapeli. Hakunilipa pesa yangu. Nikafuatilia kwa njia ya sheria na kutumia police wa pale Central ya posta Tukafanikiwa kumkamata lakini kama mnavyojua police hawahusiki na madeni na jamaa alikuwa na connection, hata ndani hakulala.

Kilichotokea tu ni kwamba police walishauri niende mahakamani au tuandikishane pale pale.

Tukaandikishana mkataba kwamba atakua ananilipa kwa awamu. Mpaka sasa hajalipa hata sumni na amekuwa mbishi sana. Ni kama aliwapa pesa wale police maana kila Nikimkumbusha deni langu anakataa anasema yeye amesha nilipa.

Nikimuuliza umenilipaje anasema alikua ananipa pesa cash kitu ambacho ni uongo.

Sasa wadau naombeni solution huyu mtu nimfanye nini? Kwanza kabisa amechangia katika kuanguka kwa biashara yangu.

Mwanzo nilifikiria kwenda mahakamani lakini najua nitapoteza pesa nyingi na wanasheria wengi ni wahuni. Pia mahakimu hawaaminiki wanaweza kula rushwa na nikapoteza haki yangu.

Wazo la pili nafikiria niende kwa mtaalam anisaidie kurejesha deni langu. Nimeshapata connection ya watalaam wanaoweza mambo hayo watu wa uhakika. Walionipa connection wao walifanikisha kurejesha pesa/mali zao.

Naombeni ushauri madhara ya kutumia mtaalam kurejesha deni na faida zake.
 
Broo watanzania walio wengi sio waaminifu katika suala la pesa

All in all pambana nae mtakapo ishia ndio hapo hapo

Yan hata akulipe kidogo kidogo sio mbaya kuliko jamaa kujitoa mshipa wa aibu kabisa kuwa alisha lipa

Sio fair kabisa

Note

Karma is real .huyo jamaa mpe muda na yeye atakuja kutapeliwa kiasi zaidi ya hicho.
 
Ni ngumu sana kukulipa pesa hizo kama makubaliano yenu yalijikita kwenye malikauli. Hata huko mahakamani hawana namna ya kumlazimisha mdaiwa akulipe pesa yote au hata robo yake. Kwa kawaida mdaiwa hakatai kuwa humdai na huahidi kulipa.

Mahakama huafuatilia tu kama amelipa angalau kidogo kidogo hata kwa miaka mingi, lakini haiwezi kulazimisha-kwa sababu hata ukimfunga ndio hatalipa kabisa.
 
Pesa ndefu iyo kafanya na ushirikina juu kuwa makini ..Hapo kariakoo umafia ni mwingi sana Kuna mambo ya ovyo haswa nguvu za giza.

Hiyo pesa ni ndefu hapa bongo uaminifu ni mdogo sana utapoteza watu sana na mtu akipanga ubishi ni forever. Kama hamjaandikishiana na kapanga tabu basi andika maumivu.
 
Yaani watanzania walio wengi kwa asilimia kubwa sio waaminifu hata kidogo kwenye inshu mbali mbali mimi nakushauri wewe mloge tu awe ndondocha kila mtu akose
Bongo hata aje mtu akuambia nigaiye 20k fasta jioni nakurudishia ujue ndo kibati hupati ng'o.
 
Back
Top Bottom