Crimea Bridge
Member
- Oct 8, 2022
- 51
- 152
Kuna mdau alikuwa ni mteja wangu, hapa Kariakoo. Nilikua nampa mali kauli ili akauze, mara ya mwisho kabisa uyo mteja alinitapeli. Hakunilipa pesa yangu. Nikafuatilia kwa njia ya sheria na kutumia police wa pale Central ya posta Tukafanikiwa kumkamata lakini kama mnavyojua police hawahusiki na madeni na jamaa alikuwa na connection, hata ndani hakulala.
Kilichotokea tu ni kwamba police walishauri niende mahakamani au tuandikishane pale pale.
Tukaandikishana mkataba kwamba atakua ananilipa kwa awamu. Mpaka sasa hajalipa hata sumni na amekuwa mbishi sana. Ni kama aliwapa pesa wale police maana kila Nikimkumbusha deni langu anakataa anasema yeye amesha nilipa.
Nikimuuliza umenilipaje anasema alikua ananipa pesa cash kitu ambacho ni uongo.
Sasa wadau naombeni solution huyu mtu nimfanye nini? Kwanza kabisa amechangia katika kuanguka kwa biashara yangu.
Mwanzo nilifikiria kwenda mahakamani lakini najua nitapoteza pesa nyingi na wanasheria wengi ni wahuni. Pia mahakimu hawaaminiki wanaweza kula rushwa na nikapoteza haki yangu.
Wazo la pili nafikiria niende kwa mtaalam anisaidie kurejesha deni langu. Nimeshapata connection ya watalaam wanaoweza mambo hayo watu wa uhakika. Walionipa connection wao walifanikisha kurejesha pesa/mali zao.
Naombeni ushauri madhara ya kutumia mtaalam kurejesha deni na faida zake.