Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kwa wale wenye malengo yakuja kumiliki taasisi za kifedha n.k au ulisoma 'economics & investment' au 'Finance and investment' na hujui wapi pa kuitumia taaluma yako; huu ni uwanja wako.
Lakini yeyote anaweza akafanya, ili mradi uwe tayari kuchukua 'risk' baada ya kuitathmini.
Inawezekana una mtaji mdogo, labda milioni moja n.k
Fanya yafuatayo:-
Tujadili.Lakini yeyote anaweza akafanya, ili mradi uwe tayari kuchukua 'risk' baada ya kuitathmini.
Inawezekana una mtaji mdogo, labda milioni moja n.k
Fanya yafuatayo:-
- Sajili jina la biashara i.e Equation x partnership
- Chukua milioni moja gawa kwa elfu hamsini
- Utapata 20
- Ina maana, utatakiwa utafute watu wenye mitaji midogo wanaofanya biashara ya kutoka kwa haraka; inaweza kuwa genge, mama ntilie n.k
- Tumia ujuzi wako na muda, kupata watu sahihi na ikiwezekana andikianeni makubaliano, namna ya uwekezaji na namna ya kugawana faida.
- Najua umeenda shule, weka fomula zitakazosaidia uwazi wa mapato
- Wekeza kwa kila mmoja kiasi cha fedha; na wao watakuwa wanakufanyia kazi bila wao kujua, igawa mtakuwa mnagawana faida.
- Kwa wale waaminifu unaweza ukawa unaongeza mzigo (fedha) kadiri unavyozalisha.
- Maendeleo yakiwa mazuri, endelea kuongeza idadi ya watu n.k
- Ukishakuwa na mtaji mkubwa, unaweza kubadili aina ya biashara kwa kujiondoa kwenye ushirika, na ukawa unawakopesha wao na wengineo, na wakawa wanarejesha kwa riba.
- Sajili taasisi yako kuwa taasisi ya kifedha