Namna ya kuifanya Afrika kuwa nchi moja

Namna ya kuifanya Afrika kuwa nchi moja

Je inawezekana Tanzania kuiteka Afrika na kuunda nchi moja inayotokana na Afrika ?


  • Total voters
    3

ThisisDenis

Senior Member
Joined
Apr 14, 2013
Posts
162
Reaction score
139
Ili tuweze kuiunganisha afrika sisi kama watanzania ni kuwaunganisha kua nchi moja na kuiongoza. Tumeona nchi nyingi zinapitia migogoro na migogoro hiyo siso kama watanzania ndio tunaenda kuwasaidia, ikiwemo ifuatayo:-
1. Vurugu za kampeni
2. Vurugu baada ya matokeo
3. Makundi ya kihuni yasio na kichwa wala miguu.
4. Ukosaji wa demokrasia na adabu miongoni mwa nchi.
5. Kushindwa kujisimamia wenyewe.

Kupitia changamoto hizi ambazo nchi nyingi za afrika ambazo zinajifanya zinajua sana ndio zinatumbukia kwenye matatizo hayo na sisi kama watanzania tumekua tukienda kuwasimamia, kuwasaidia na kuwakomboa na wanarudo wanakaa sawa. Tumeona nchi nyingi zimeongeza nguvu kwa kununua nchi zingine mfano wa nchi hizo ni Marekani, Urusi, United Kingdom, na Unated Arabs Emirate.


Sasa kwa nini sisi kama watanzania tusitie mbinu za kiitelijensia kuwaingiza nchi zingine kwenye migogoro na kuwanyakua mamlaka na kuwafanya wawe part ya nchi ya Tanzania na Mwisho wa siku Tanzania inakua ndio inakua Afrika lakini yenye misingi ya mswahili. ???????
 
Haiwezekani kwa kuwa
1) Tanzania yenyewe bado haijaweza haijaweza kujisimamia kikamilifu,bado tunategemea vitu vingi kutoka kwa wahisani,demokrasia imekandamizwa kwa mtutu wa bunduki hivyo inakuwa vigumu kwa raia kutoa maoni kwa uhuru kwa hofu ya kutekwa na vyombo vya dola na kuuliwa.

2) haiwezekani kwa kuwa miongoni mwa nchi hapa hapa africa zina hali bora kiuchumi, kielimu,na hata kiafya kuliko tanzania, mfano SA, botswana, Namibia,Morocco Tunisia nk, hazitakubali katu kusimamiwa na watu wasio na akili.

3) MIKAKATI, kila nchi ina road map (niyaite malengo) ambayo ndiyo yanayoifanya hiyo nchi iwe kwenye hali husika kwa wakati uliopita, wakati uliopo, na wakati ujao,( bahati mbaya tanzania yetu hatujui malengo yetu mahsusi ni yepi hasa) hivyo ni vigumu kuitawala nchi yenye mwelekeo mahsusi hata kama ipo vitani, maadui wawili wanaojuana na wanaopigania maslahi ya nchi moja ila kwa tofauti ya mitazamo wakajikuta vitani ni rahisi kwao kuungana kukupiga kwanza uwaachie nchi yao waendelee kuipigania, labda kwa round table, ila nayo inahitaji ushawishi wa hali ya juu mno amba yo tanzania hatuwezi kuwa nao kwa miaka mia kenda ijayo,hadi sasa nchi zenye ushawishi hazizidi tano duniani, Usa, China, Russia, na labda UK na France,, najichosha tu kuandika!!

KIUFUPI NI KUWA HAIWEZEKANI KABISA. Over
 
Back
Top Bottom