mjusilizard
JF-Expert Member
- Nov 7, 2019
- 1,027
- 1,869
Wasalaam,
Watu wengi maeneo ya mijini vipato vyao ni wastani wa Tsh. 10,000 kwa siku, hii inafanya wengi wafikishe angalau Tsh. 330,000 kwa mwezi.
Kwa kipato hiki wapo wanaishi vizuri kabisa kwa familia za watu wachache na wanaishi bila kuwa na madeni. Mchanganuo rahisi ni kama huu hapa chini kwa faida ya wengi.
Kwanza kabisa hakikisha kwamba mke, mtoto na wewe msitumie zaidi Tsh. 200,000 kwa mwezi. Pia, mke na mtoto wawe na bima za afya kwa mwaka ambazo unalipia Tsh. 170000.
Wazazi wapewe Tsh. 80,000 tu, yaani, upande wa kike wapate Tsh. 40,000 na upande wa kike wapate hivyo hivyo. Kila mmoja, hasa mwanaume, awe na pocket money yake isiyozidi Tsh. 20,000 kwa mwezi.
Kama mmejenga tumieni sola tu, ila kama hamjajenga pangeni chumba kodi iwe si zaidi ya Tsh. 35,000 kwa mwezi. Inayobaki mnaweza kusevu. Ila hakikisha mama mjengo naye awe na sehemu ya kujipatia riziki ili kuziba mapengo yatakayojitokeza katikati hapo.
Mwisho kabisa, msipande magari safari fupi fupi ama kusafiri kwa daladala labda iwe ni lazima sana. Kila la heri!