Namna ya kujenga daraja jipya Ferry - Kigamboni ndani ya siku 3 tu

Mkuu wazo lako ni zuri ila hapo kama patatolewa pantoni basi pawekwe daraja la kufunga na kufunguka kama lile la London Tower Bridge nchini Uingereza ambalo litakuwa ni refu kwenda juu ili kuwe na air clearance kubwa kuruhusu meli kupita bila kizuizi au likifungwa meli zipite bila tatizo.

Endapo litajengwa daraja kama hilo ujenzi utabidi uanzie mbali ili kutafuta level pande zote za Kigamboni na Magogoni, Pia ni gharama kubwa sana na hii itakuwa ni mradi mkubwa kwetu.
Ghafama ya hilo ni kubwa sana na kuna ufinyu wa nafasi, hili litafunguka kwa pantoni ya katikati kujikata na kupisha meli halafu meli ikishapita pantoni linarudi kuunga daraja.
 
Mkuu hakuna haja ya kuweka pantoni 3. Kwa mchoro wako huo wa pantoni 3 kati ya pantoni moja na jingine kuna eneo la wazi kiusalama haitokuwa sahihi maana itaweza kuathiri stability ya chombo endapo juu kutakuwa na gari zinapita.

Hii ni kwa sababu pantoni chini litakuwa halina mzigo wowote na juu ndio kuna mzigo hapo Vertical Stability ya pantoni itakuwa dhaifu na kuhatarisha usalama.

Na kuhusu kutumia nanga(anchor) kuzuia pantoni zisisogee itakuwa ngumu, na kuhakikishia hata ukiweka nanga chombo bado kitazunguka hapo hapo (drift) kwa kuwa hapo kuna upepo na mkondo wa maji.

Kuzizuia pantoni 3 kisha meli ikitaka ipite zitoke na baadae pantoni zirudi teknolojia nyingine itabidi itumike na pantoni hazitoweza kuwa off. Lazima emergency generators ziwe zimewashwa maana nanga ili ipande na kushuka tutatumia umeme kusukuma chain.
Pantoni zinawashwa wakati wa kufanya hizo manouvres za kupisha meli tu. Pia stability italetwa na 'balast tanks' za chini ya pantoni ambazo huwa zinajazwa maji kwa kadri ya stability inavyohitaji.
 
Nakuunga mkono kwa idea yako ila hapo kama kutotumia pantoni pawekwe open and closed tower brigde.

Hilo ni eneo la mlango wa bahari na ndio njia pekee ya kuingia bandari ya Dar. Meli inapoingia au kutoka inabidi isichelewe ili tuwe na Ship Turnaround ya kutumia muda mchache pale bandari na kufanya bandari yetu iwe inafanya kazi haraka kutokana na meli kutotumia muda mrefu.
Kitendo cha pantoni kujikata ili kuruhusi meli ipite kinachukua dakika chache sana na kinafanyika well in advance kabla hata meli haijafika hivyo hakuna ucheweleshaji wowote
 
Na hizo pantoni zitaundwa kwa siku tatu tu? Na hizo "anchor" za kuzuwia mkondo wa ferry pale umeshazifikiria zitakuwaje ili zizuwie hizo pantoni zisiyumbe na kwa muda gani?

Bora ungesema zitumike pantoni bridges za kijeshi, hata hizo nazo ni za muda tu si "permanent".

Solution rahisi na sahihi ya ferry ni tunnel tu lianzie mbali. Gharama kubwa lakini litadumu miaka mingi sana ijayo.
 
We ni Engineer?
Ni kwamba zinawekwa ferry tatu (3) tu ndefu na zenye milango mirefu ya kufunguka ambapo zinagusana mwanzo hadi mwisho na hivyo kutengeneza barabara inayoelea baharini.

Na ikitokea meli inataka kupita pantoni la katikayi linajikata na kupisha meli kisha inarudi mahala pake.

Picha hapo chini ina maelezo zaidi.

View attachment 1326086

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndugu hata uende na idea ya cheap na efficient kiasi gani..HAIWEZEKANI

Kivuko cha Kigamboni ni chanzo kikubwa cha pesa kwa hawa jamaa...

Kuna mawazo mawili hapa ambayo yataweza tatua hili janga.

1. Underground tunnel - Gari zipite chini ya bahari kuruhusu traffic ya Meli bila bugudha yoyote...

2. Floating Bridge - Hii ni kama ulivyoelezea hapo juu, smart and cheap idea

Lakini hebu jiulize wale mbuzi wa pale Ferry wamekewa facilities ngapi ambazo wangeweza kuzitumia kupunguza matatizo yaliyopo sasa

1.Kero ya kutumia ticket za karatasi.

Huu upuuzi kwanza unasababisha uchafu, Pili usiombe siku una haraka zako alaf ukute hamna network...mtapanga foleni kama mnaenda kuchukua uji Bwalo la chakula.
SOLUTION: Kuna facility za kadi za malipo kwa NFC, hizi zikianza kutumika hii itabaki story

2. Misafara ya viongozi: Hapa uko haraka zako alaf kinakuja kivuko , badala ya kupanda nyie abilia zitaingia gari mbili au tatu za viongozi na kuondoka.
SOLUTION: Misafara yote isipokuwa gari za wagonjwa tu itumie daraja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hizo pantoni zitaundwa kwa siku tatu tu? Na hizo "anchor" za kuzuwia mkondo wa ferry pale umeshazifikiria zitakuwaje ili zizuwie hizo pantoni zisiyumbe na kwa muda gani?

Bora ungesema zitumike pantoni bridges za kijeshi, hata hizo nazo ni za muda tu si "permanent".

Solution rahisi na sahihi ya ferry ni tunnel tu lianzie mbali. Gharama kubwa lakini litadumu miaka mingi sana ijayo.
Assuming pantoni zimeshaundwa tayari, siku tatu zinatosha kutrain manahodha namna ya kufanya hizo manouvres. Ndio nimeshafikiria namna ya kujrnga hizo achors na zitadumu hata miaka 100.
 
Hapo ndugu hata uende na idea ya cheap na efficient kiasi gani..HAIWEZEKANI

Kivuko cha Kigamboni ni chanzo kikubwa cha pesa kwa hawa jamaa...

Kuna mawazo mawili hapa ambayo yataweza tatua hili janga.

1. Underground tunnel - Gari zipite chini ya bahari kuruhusu traffic ya Meli bila bugudha yoyote...

2. Floating Bridge - Hii ni kama ulivyoelezea hapo juu, smart and cheap idea

Lakini hebu jiulize wale mbuzi wa pale Ferry wamekewa facilities ngapi ambazo wangeweza kuzitumia kupunguza matatizo yaliyopo sasa

1.Kero ya kutumia ticket za karatasi.

Huu upuuzi kwanza unasababisha uchafu, Pili usiombe siku una haraka zako alaf ukute hamna network...mtapanga foleni kama mnaenda kuchukua uji Bwalo la chakula.
SOLUTION: Kuna facility za kadi za malipo kwa NFC, hizi zikianza kutumika hii itabaki story

2. Misafara ya viongozi: Hapa uko haraka zako alaf kinakuja kivuko , badala ya kupanda nyie abilia zitaingia gari mbili au tatu za viongozi na kuondoka.
SOLUTION: Misafara yote isipokuwa gari za wagonjwa tu itumie daraja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado magari yataendelea kulipia kama kawaida kwenye toll booth kabla ya kuvuka, hivyo mapato yao yatabaki pale pale
 
Zinakuwa anchored na kamba au minyororo pantoni la kwana na la mwisho, katikati ile milango inajikamata kwa interlocking system, engine zinakuwa OFF!
Nadhani hujui kuwa ukizima injini maji yanasomba kivuko!
 
Meli zinazokuwa anchored bandarini kwa muda wa hadi miezi miwili zikisubiri kuondoka, huwa zinawasha injini zake kwa muda wa miezi miwili? Nini maana ya 'anchoring' kwa uelewa wako?
 
Kitendo cha pantoni kujikata ili kuruhusi meli ipite kinachukua dakika chache sana na kinafanyika well in advance kabla hata meli haijafika hivyo hakuna ucheweleshaji wowote
Daraja la kufunga na kufunguka lina chukua dakika moja.
Hiyo Pantoni itachukua muda gani kufunguka.

Pili, iyo pantoni ikifunguka itaenda kukaa wapi ili isiwe kikwazo kwa meli kuingia bandarini na litatumia muda gani.

Baharini kuna sheria za uendeshaji vyombo (Rule of the road at the sea). Ukicheki hizo sheria hiki kitu kufanyika kwenye mlango wa bandari itakuwa ngumu.
 
Assuming pantoni zimeshaundwa tayari, siku tatu zinatosha kutrain manahodha namna ya kufanya hizo manouvres. Ndio nimeshafikiria namna ya kujrnga hizo achors na zitadumu hata miaka 100.
Mkuu sio kila sehemu ya bandari au bahari unatakiwa kuweka anchor. Kuna maeneo maalumu yametengwa kwa mfano Dar es Salaam Port unatakiwa uweke nanga nje karibu na kile kisiwa kinaitwa Outer Mwakatumbe.

Sababu nyingine hapo karibu na bandari pia kambi ya jeshi chini kuna uwezekano wa kuwepo underground cable, sasa kitendo cha kuangusha nanga pindi unaponyanyua unaweza kukata hizo cable.

Pia nanga kuipandisha na kushusha inaweza ikawa ni kitendo cha kupoteza muda. Labda kama kuna technology mpya imetoka.
 
Hapo ndugu hata uende na idea ya cheap na efficient kiasi gani..HAIWEZEKANI

Kivuko cha Kigamboni ni chanzo kikubwa cha pesa kwa hawa jamaa...

Kuna mawazo mawili hapa ambayo yataweza tatua hili janga.

1. Underground tunnel - Gari zipite chini ya bahari kuruhusu traffic ya Meli bila bugudha yoyote...

2. Floating Bridge - Hii ni kama ulivyoelezea hapo juu, smart and cheap idea

Lakini hebu jiulize wale mbuzi wa pale Ferry wamekewa facilities ngapi ambazo wangeweza kuzitumia kupunguza matatizo yaliyopo sasa

1.Kero ya kutumia ticket za karatasi.

Huu upuuzi kwanza unasababisha uchafu, Pili usiombe siku una haraka zako alaf ukute hamna network...mtapanga foleni kama mnaenda kuchukua uji Bwalo la chakula.
SOLUTION: Kuna facility za kadi za malipo kwa NFC, hizi zikianza kutumika hii itabaki story

2. Misafara ya viongozi: Hapa uko haraka zako alaf kinakuja kivuko , badala ya kupanda nyie abilia zitaingia gari mbili au tatu za viongozi na kuondoka.
SOLUTION: Misafara yote isipokuwa gari za wagonjwa tu itumie daraja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kigamboni ferry na Kigongo Busisi ndio vyanzo vikuu vya mapato kwa Temesa. Vivuko vyote vilivyobaki maeneo mengine ni kama wanatoa huduma kwa jamii.
 
Back
Top Bottom