Namna ya kujenga daraja jipya Ferry - Kigamboni ndani ya siku 3 tu

Ghafama ya hilo ni kubwa sana na kuna ufinyu wa nafasi, hili litafunguka kwa pantoni ya katikati kujikata na kupisha meli halafu meli ikishapita pantoni linarudi kuunga daraja.
 
Pantoni zinawashwa wakati wa kufanya hizo manouvres za kupisha meli tu. Pia stability italetwa na 'balast tanks' za chini ya pantoni ambazo huwa zinajazwa maji kwa kadri ya stability inavyohitaji.
 
Kitendo cha pantoni kujikata ili kuruhusi meli ipite kinachukua dakika chache sana na kinafanyika well in advance kabla hata meli haijafika hivyo hakuna ucheweleshaji wowote
 
Na hizo pantoni zitaundwa kwa siku tatu tu? Na hizo "anchor" za kuzuwia mkondo wa ferry pale umeshazifikiria zitakuwaje ili zizuwie hizo pantoni zisiyumbe na kwa muda gani?

Bora ungesema zitumike pantoni bridges za kijeshi, hata hizo nazo ni za muda tu si "permanent".

Solution rahisi na sahihi ya ferry ni tunnel tu lianzie mbali. Gharama kubwa lakini litadumu miaka mingi sana ijayo.
 
We ni Engineer?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndugu hata uende na idea ya cheap na efficient kiasi gani..HAIWEZEKANI

Kivuko cha Kigamboni ni chanzo kikubwa cha pesa kwa hawa jamaa...

Kuna mawazo mawili hapa ambayo yataweza tatua hili janga.

1. Underground tunnel - Gari zipite chini ya bahari kuruhusu traffic ya Meli bila bugudha yoyote...

2. Floating Bridge - Hii ni kama ulivyoelezea hapo juu, smart and cheap idea

Lakini hebu jiulize wale mbuzi wa pale Ferry wamekewa facilities ngapi ambazo wangeweza kuzitumia kupunguza matatizo yaliyopo sasa

1.Kero ya kutumia ticket za karatasi.

Huu upuuzi kwanza unasababisha uchafu, Pili usiombe siku una haraka zako alaf ukute hamna network...mtapanga foleni kama mnaenda kuchukua uji Bwalo la chakula.
SOLUTION: Kuna facility za kadi za malipo kwa NFC, hizi zikianza kutumika hii itabaki story

2. Misafara ya viongozi: Hapa uko haraka zako alaf kinakuja kivuko , badala ya kupanda nyie abilia zitaingia gari mbili au tatu za viongozi na kuondoka.
SOLUTION: Misafara yote isipokuwa gari za wagonjwa tu itumie daraja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Assuming pantoni zimeshaundwa tayari, siku tatu zinatosha kutrain manahodha namna ya kufanya hizo manouvres. Ndio nimeshafikiria namna ya kujrnga hizo achors na zitadumu hata miaka 100.
 
Bado magari yataendelea kulipia kama kawaida kwenye toll booth kabla ya kuvuka, hivyo mapato yao yatabaki pale pale
 
Zinakuwa anchored na kamba au minyororo pantoni la kwana na la mwisho, katikati ile milango inajikamata kwa interlocking system, engine zinakuwa OFF!
Nadhani hujui kuwa ukizima injini maji yanasomba kivuko!
 
Nadhani hujui kuwa ukizima injini maji yanasomba kivuko!
Meli zinazokuwa anchored bandarini kwa muda wa hadi miezi miwili zikisubiri kuondoka, huwa zinawasha injini zake kwa muda wa miezi miwili? Nini maana ya 'anchoring' kwa uelewa wako?
 
Kitendo cha pantoni kujikata ili kuruhusi meli ipite kinachukua dakika chache sana na kinafanyika well in advance kabla hata meli haijafika hivyo hakuna ucheweleshaji wowote
Daraja la kufunga na kufunguka lina chukua dakika moja.
Hiyo Pantoni itachukua muda gani kufunguka.

Pili, iyo pantoni ikifunguka itaenda kukaa wapi ili isiwe kikwazo kwa meli kuingia bandarini na litatumia muda gani.

Baharini kuna sheria za uendeshaji vyombo (Rule of the road at the sea). Ukicheki hizo sheria hiki kitu kufanyika kwenye mlango wa bandari itakuwa ngumu.
 
Assuming pantoni zimeshaundwa tayari, siku tatu zinatosha kutrain manahodha namna ya kufanya hizo manouvres. Ndio nimeshafikiria namna ya kujrnga hizo achors na zitadumu hata miaka 100.
Mkuu sio kila sehemu ya bandari au bahari unatakiwa kuweka anchor. Kuna maeneo maalumu yametengwa kwa mfano Dar es Salaam Port unatakiwa uweke nanga nje karibu na kile kisiwa kinaitwa Outer Mwakatumbe.

Sababu nyingine hapo karibu na bandari pia kambi ya jeshi chini kuna uwezekano wa kuwepo underground cable, sasa kitendo cha kuangusha nanga pindi unaponyanyua unaweza kukata hizo cable.

Pia nanga kuipandisha na kushusha inaweza ikawa ni kitendo cha kupoteza muda. Labda kama kuna technology mpya imetoka.
 
Kigamboni ferry na Kigongo Busisi ndio vyanzo vikuu vya mapato kwa Temesa. Vivuko vyote vilivyobaki maeneo mengine ni kama wanatoa huduma kwa jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…