Namna ya kujihami na Panya Road au Makundi ya namna hiyo

Hayo ndio maamuzi ya Mwanaume sio kumpaka rangi punda ili awe pundamilia.
 
Safi sana mkuu,katika hayo masekeseke ya Kupitia orodha ya Panya Road na kuwaadabisha kiasi cha wengine kutorokea mitaani basi mmoja ya waliotoroka alikuwa mtoto wa kaka yangu alikuwa anaishi Mbagala Charambe akatoroshewa huko Morogoro ndanindani na kaka yangu maisha yakaendelea. Sasa huko alipoenda bhana akawa organizer wa kundj jipya la Panya Road nikawa naskia matukio yake tu mara kaiba pikipiki yeye na kundi lake,mara kachanachana khanga ya dada yake vipandevipande,mara yeye na wahuni wenzie wamevamia kilabu cha pombe za kienyeji na kupora nikamwambia bro huyu mtoto kama kakushinda hebu niachie mimi nimfundishe adabu,Bro akanipa baraka zote nilichofanya mimi sukuma ndinga vuup mpaka Kijijini nikamwambia dogo kuna kazi nataka tukaifanye mjini chukua na washkaji wako kama watatu hivi twende nao nikajua tu kwamba angewachagua tu wale wa kwenye cycle yake na wao nilitaka niwafinye kidogo hili wamuone dogo kama ukoma hata akija siku nyingine wasimpe kampani. Basi bhana hao mpaka Dar kuna jamaa zangu wapo pale Oysterbay police post nikawapa mchongo wote basi nilivyowafikisha tu madogo tukaenda huko nje ya mji maafande wakiwa na gwanda zao vilevile aisee walitoa kibano mpaka huruma ikaanza kuniingia hakuna rangi au mateso ambayo wale madogo hawakuacha kuyaona..Tangu siku ile dogo respect sana siku hizi yupo South naambiwa katulia huyo anauza mini supermarket huko...Sometimes wazazi wetu wa uswahilini wanachangja ongezeko la Panyaroad kwa kuwakingia kifua
 
Rafiki yangu akawapokea Kwa kusema Oyo!Oyo! oyo! Huku na Mimi nikiwa nadakia kuonyesha tupo pamoja.
Experience adimu sana hii.
===
"Nilienda kwenye tamasha hili nikiwa na Yule Yule Rafikiangu, unajua wengine tunapenda ku- socialize ukiniita sociologist hautakuwa umekosea"

"Kujichanganya kwenye jamii inakupa kitu inaitwa Interpersonal skills yaani Ujuzi wa kuchangamana na kujamiiana na watu wengine. Hii itakufanya uhitimi kozi ya kitaaolojia."

Hapo umenikumbusha album ya FID Q.
 
wahuni cku zote jichanganye nao ata kama wew sio muhuni.. wafnye kuwa rafiki ;ukikutan nao sehem za bata watembezee ata dusko au ata fegi kama uko vizuri ;iyo itafanya wakujue na pia utaishi kwa usalama mtaa huo.

Wahuni hawapo hivyo Mkuu!
Wahuni hawana tofauti na wachawi.
 

Hivyo ndivyo inatakiwa
 

Hapo watu wataangalia muktadha wa neno katika sentenai Mkuu.
 
Mtu amejenga nyumba ajabu ndani tena chumbani hana panga wala mkuki wala jambia au rungu au kwenye gari unakosaje hata panga kwenye buti au unatembea unakosaje kisu kidogo au cha kati cha kiunoni au mfukoni,

Alafu yakitokea ya kutokea atailaumu serikali.
Serikali itafanya yake lakini tayari utakuwa umepata madhara.
 

Huo ndio Uanaume!

Wao ndio wakashtaki Polisi, sio ninyi wanaume wazima bila haya mnaenda kushtaki baada ya kuonewa.
Ninyi kazi yenu kutoa taarifa polisi tuu,
 
Mara nyingi hawa watoto hua wanaharibiwa na wazazi wao wenyewe, dogo anazingua badala mzazi amuwajibishe yeye anamchekea mwisho wa siku dogo anakua nunda.
Katika ile orodha ya majina tuliyopewa ya wale panya, kuna dogo mmoja sasa hivi yupo A-level na anafanya vizuri sana darasani.
Mwanzo alikataa kabisa shule ila baada lile tukio la wenzake kuwajibishwa na wananchi wenye hasira kali nasikia yeye mwenyewe aliwalilia wazazi wake wampeleke shule.
 
Kuna jamaa yangu, aliwahi kuchezea kipigo na hawa panya road, mbele ya dem wake, mitaa ya cocobeach.. Ili nifundisha niwe na tembea na siraha muda wote...

Huko Coco Beach zamani zile walikuwa wanasubiri jioni kagiza kakiingia ndio wanaleta Fujo.
Ila wanaangalia na wakumletea Fujo.

Ukiwa na demu wako kama upo kinyonge na upo pekeako anakuja mmoja anajifanya huyo demu wako ni wake. Kisha wenzake wanakuja.

Kama hujajipanga mbona kisanga
 
Nimekuelewa sana ndugu, ila Magomeni hakukuwa na panya road nakumbuka ile siku ilikuwa ni tetesi tu
 
Huo ndio Uanaume!

Wao ndio wakashtaki Polisi, sio ninyi wanaume wazima bila haya mnaenda kushtaki baada ya kuonewa.
Ninyi kazi yenu kutoa taarifa polisi tuu,
Matukio ya mwanzo ya hawa panya kufanya mjumbe na mwenyekiti wetu alienda kulalamika kituo cha polisi, ila polisi nao walimuuliza mwenyekiti hapo mtaani kwenu kuna wanaume pia wanaishi au mtaa wote wanaishi wanawake?
Kama mtaa wote hamna wanaume ni wanawake watupu haya matukio ndio mnatakiwa mje kulalamika.
Haya majibu yalileta molari ya hali ya juu wanaume kuanza operesheni ya nyumba kwa nyumba kudaka kila panya tunae ishi nae kitaani kwetu.
 
Panyaroad wana maeneo yao wanayo yaonea
Kinondoni huwez ona upuz huu

Ova
 
wahuni cku zote jichanganye nao ata kama wew sio muhuni.. wafnye kuwa rafiki ;ukikutan nao sehem za bata watembezee ata dusko au ata fegi kama uko vizuri ;iyo itafanya wakujue na pia utaishi kwa usalama mtaa huo.
Nimeitumia sana hii mbinu kuishi na wahuni wa tandika kilimahewa bila shida yoyote, ilikuwa nikienda mtaa ambao sijulikani alafu nikataka kuwekwa mtu kati basi akitokea muhuni ata mmoja tu wa kitaa changu utasikia "oyyoo mkaushieni hyu mwanetu, huyu kichaa wetu mwache ajikatae". Mpk nahama tandika takriban miaka zaidi 7 Ya kuishi kule sikuwahi kuporwa wala kuzinguliwa na muhuni,.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…