Nyagawakelvin
Member
- Apr 8, 2021
- 8
- 34
NAMNA YA KUKOKOTOA SIKU YA KUPATA UJAUZITO NA MZUNGUKO WA HEDHI KWA URAHISI | HOW TO CAN YOU KNOW YOUR MENSTRUAL CIRCLE AND A DAY TO CONCEIVE?
Inaletwa kwenu na Kelvin Nyagawa
Kupitia somo hili dakika 5 baada ya kumaliza kusoma utakwenda kufahamu jinsi ya kuhesabu mzunguko wa hedhi kwa urahisi zaidi.
.
Kwa wastani mzunguko wa hedhi nisiku 28, Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa kuanzia siku ya kwanza mwanamke anapoanza ku bleed.
.
Kwa kawaida idadi ya siku katika mzunguko ambazo huhesabika kama ni mzunguko wa kawaida nisiku 21 hadi 35, Ambapo hapo ndipo utapata wastani wa siku 28 yaani [(21+35)-:2].
.
Ili tuseme mwanamke anamizunguko ya hedhi iliyo sawa (Regular cycles) Inabidi idadi ya siku za mizunguko ya hedhi kati ya mwezi na mwezi isitofautiane kwa zaidi ya wiki moja (siku 7).
KWA MFANO:
Kama mwezi wa kwanza aliona siku zake baada ya siku 28, Mwezi wapili akaona baada ya siku 30, Mwezi unao fwata akaona baada ya siku 35, Bado mzunguko wake upo kwenye uwiano mzuri (Regular cycle). Kwa sababu mzunguko mmoja na mwingine hauja tofautiana kwa zaidi ya siku 7.
"Usichanganye kati ya menstrual period na menstrual cycle, hivi ni vitu viwili tofauti kabisa".
Siku ya kwanza ya ku bleed ndo siku tunayoanza kuhesabu mzunguko wa hedhi (day one), Sio siku ya kumaliza ku bleed.
Kwa kawaida idadi ya siku za ku bleed ni kati ya siku 3 hadi 7, Hapa pia kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo.
NAMNA YA KUKOKOTOA SIKU YA KUPATA UJAUZITO.
Idadi ya siku kati ya ovarian cycle na menstrual cycle hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke (Mfano wapo wa siku 28, 30, 25 kama tulivyo ona mwanzo.
Idadi ya siku katika luteal phase niswa katika mizunguko yote na ni siku 14. Hapa tuelewane.
KWA MFANO:
Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28, kuipata siku ya ovulation tunachukua 28-14 tunapata 14, kwahiyo kutoka siku ya kwanza mwanamke alipo anza ku bleed ni siku ya 14 ndiyo yai linakuwa tayari kurutubishwa.
.
Kwa mwenye mzunguko wa siku 30, tunachukua 30-14 tunapata 16, kwahiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30, ovulation inauwezekano mkubwa wa kutokea siku ya 16 na sio siku ya 14 (Hapo kuwa makini).
.
Yule mwenye mzunguko wa siku 35, ovulation day ni 35-14=21, Kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35, Ovulation inanafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.
.
Sasa baada ya kuijuwa siku ya ovulation lazima uwe makini na siku zinazokaribiana na siku ya ovulation kwani ni siku za hatari pia.
KWANINI?
Mbegu za kuime zinauwezo wa kuwa hai hadi masaa 48 (2 days) tangu shahawa zimwagiwe ndani, Na yai la mwanamke linaweza kuwa hai hadi masaa 24 tangu kutolewa kwenye ovary.
Kwa hiyo kama mwanaume akijamiana na mwanamke siku mbili kabla ya yai kutolewa kwenye ovari, Mbegu inaweza kuwa hai na kutungisha mimba, endapo yai litatolewa ndani ya siku mbili zijazo.
Kadhalika kama mwanamke atatoa yai siku ya 14 kisha akajamiana ndani ya masaa 24 mbeleni, pia anaweza pata mimba kwasababu kipindi mbegu zina mwagwa zinaweza kulikuta yai bado lipo hai na kutungisha mimba.
Kwaufupi nisiku tatu tu, Ndizo hatari sana mwanamke kupata mimba, yaani, siku mbili kabla ya ovulation na ndani ya masaa 24 baada ya ovulation.
NB: Njia ya kalenda ni nzuri sana katika kupangilia uzazi, lakini ningumu kuizingatia na kufanya kazi kwa 100%, Hivyo basi unashauriwa kutumia njia zingine za muda mrefu za uzazi wa mpango kama vile vipandikizi N.K.
Imeandaliwa na kuletwa kwenu na:
Kelvin Nyagawa
Email: nyagawakelvin85@gmail.com
Phone: +255 627 00 431