Namna ya kuondoa Tabia mbovu usiyoitaka

Asante sana asigwa kwa mada nzuri ila mara nyingi kwenye hizo affirmation una shauriwa kufanya kinyume chake kwa mfano badala ya ku sema mimi siyo mwoga unatakiwa kusema mimi ni jasiri au tafuta neno lingine lakini usirudie kutamka mwoga, punyeto pombe nk .. Kwani subconscios mind itakuwa inaskia muoga.. Muoga.. Muoga. (kwa kuwa hilo ndilo dominant hii subconscious mind haina uwezo wa kupambanua inachukuaga mambo yote kama ni real ndiyo maana ukiwa unaota unakimbiza na mashetani yenyewe inachukulia ni kweli utakuta mapigo ya moyo yanaenda mbio,jasho linakutoka nk )

Wanashauri pia unapoacha tabia flani tafuta tabia nyingine kinyume chake ya kuireplace badala ya pombe amia kwenye maziwa, fresh fruit juice, au hata soda.

Subconscious mind siku zote ni taswira (imagnation) na conscious ina controol (will) au nia. Wanasema when imagnation is stronger than will imagnation always win. Hivyo unashauriwa ubalanceshe kati ya image yako na will visiwe vinaendana kinyume. Ndiyo maana mpigaji wapunyeto hawezi fanya bila ya kuvuta taswira picha za ngono..
Hivyo nina maanisha kama unataka kuacha uraibu wowote inatakiwa ile nia ya kuacha iendane na picha mbaya ya lile jambo unalotaka kuacha au picha nzuri ya vile ambavyo unafikiri ukiacha utakuwa.. Waswahili wanasema ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.. Hivi mtu anayeita bangi au ugoro dawa au pombe juice kali. anaweza kuacha kweli? ni wazi hawezi kuacha. Hivyo njia nzuri niku itafutia jina baya na jina baya utalipata kwenye madhara ya hicho kitu unachotaka kuacha. Mtu mmoja akaita sigara cancer stick au kijiti cha kansa.. Hivi ni kwanini watu wanajua kabisa kwamba ni kivuta sigara nitapata kansa au nikinywa pombe namaliza pesa na chelewa kulala, au naharibu mwili lakini bado unaendelea kuvuta au kunywa pombe.. Ni kwa kuwa vitu vingi tunavyofanya ni kwasababu ya kupata starehe au kuepuka maumivu.. Hivyo mara nyingi watu waliobobea kwenye jambo flani inafikaga kipindi inakuwa anafanya jambo flani siyo kwasabu ya kupata tena starehe bali ni kwaajili ya kuepuka maumivu.. Sasa ikishafikia hatua hiyo unahitaji...Rudi kwenye wil na imagnation naishia hapa kwanza kwa sasa
 
Last edited by a moderator:

Natamani kujua na hiyo ya mirror technique
 
Mkuu kuna mambo unamix sana hapa, labda tuyaweke wazi kwanza.

  1. Affirmations zote hutumia formula inaitwa "AUTOSUGGESTION" au "SELF-SUGGESTION" na sio "SUGGESTION", najua kama wewe ni mtaalamu wa hii kitu utakua umenielewa, ila kifupi ni kuwa affirmations zote hutumika katika kuunda "subliminal phrases" na "internal self talk" na ndio maana ni lazima utumie nafsi ya kwanza(MIMI au I AM) katika kutengeneza phrases zako, that is to say nilichokiandika hapo sio affirmations kwa kuwa hazibebi sifa ya kuwa "AUTOSUGGESTION".
  2. Katika kuunda SUGGESTION sio lazima kukwepa kurudia neno la tabia unayotaka kuiondoa au ku replace kwa neno kinyume kwa kuwa automatically unaicommand subconcious mind yenyewe ibebe jukumu la kungeneza picha ya kile unachokitaka na sio wewe kuiundia picha kama ilivyo kwenye AUTOSUGGESTION, na ndio maana tunatumia nafsi ya pili(Wewe au YOU), hapa kama unaifahamu mirror technique utakua unanielewa vizuri sana.

Unapozungumzia kuwa imagination ndio lugha ya subconcious mind unakua umeipa ufinyu mkubwa sana wa kile unachokisema kwa kuwa subconcious mind inaelewa images tu zilizomi ksiwa na hisia(visualize), kwa hiyo hata kama utakua expert wa kucheza na "imaginations" lakini ukawa haufiki katika level ya "kuvisualize" bado subconcious mind haitakua impressed kwani itajua ni "wishfull thinking",
na kwa mfano wako wa ngono ni rahisi sana kwa mtu anaye "imagine" zinaa kuweza kupata kile anachokitaka kwa kuwa anavuka level ya "imagination" mpaka kwenye "visualization" kwa kuwa ana mix kile anachoki imagine na hisia na tofauti na principle ya "imagination" huyu anaye "visualize" zinaa huwa anapata matokeo hapo hapo bila haja ya kurudia rudia kile anachotaka kukifikia.

(Nimetumia complex language kidogo lakini nadhani utanielewa)
 
upo deep sana asigwa simaanishi ni lazima ila inashauriwa hivyo ila kurahisisha mara moja installation ya tabia mpya kwa kuwa nature ya subconscious mind ina maneno machache mara nyingi inatumia picha na hisia (ndiyo maana huwezi ota ndoto ya maneno ila unaona picha na kama nitukio la furaha watu wengine wanacheka usingizini) sasa kwanini inashauriwa hivyo kwakuwa subconscious ikishikilia jambo huwezi kulifuta bali linakuwa overpowerd na jambo jingine kuna watu wameathirika na pombe kiasi kwamba anaporudia rudia kutaja sinywi pombe lile neno pombe tu ndiyo linalosikika kwenye akili yake hivyo anapata kiu pale anaenda kunywa tena. Kuna watu wakisema siangalii tena picha za ngono. Ndiyo mizuka inampanda kabisa kwani kwenye neno dominant kwenye akili yake ni picha za ngono embu acha kusema mimi siumwi sema mimi ni mzima tena imara kama chuma cha pua,.kuhusu limit ya subconscious subconscious ni infinity unajua imerekodi maisha yako yote kwanzia umezaliwa kila tukio ulofanya, kunaushuhuda uliwahi toka kuwa mtu mmoja aliyekuwa amechomwa sindano ya ganzi nusu kifo subconscious yake ilikuwa ikielewa kila jambo kwakuwa macho yake alikuwa hajafunga.. Pia inauwezo wa kufanya mambo trillion kwa wakati mmoja mambo ya hewa cell na tissue zote mwln kuna shuhuda za watu kujiponya hadi kansa kwa kutumia subconscious hivyo inauwezo mkubwa ila haiwezi pambanua mambo tofauti. programe zilizopo ndiyo izo izo. Inatumia imagnation na feeling kazi za inner talk na outosuggestion ni za conscious mind ila pale zinapo fanya kazi kwa pamoja na upendo ndipo visualization zinapotokea watu kama wakina galileo galilei kina newton waliweza kutumia hizi vizuri..Umetumia complex term ila nimezielewa baadhi kama hiyo ya mirror sijaelewa unajubado mm mwanafunzi na nina hitaji sana kufahamu haya mambo,,
 
Last edited by a moderator:
Umeongea mengi ningekujibu yote, ila kwa sasa nikujibu hija ya kwanza halafu nikipata muda nitakujibu ya pili na ya tatu pia(simaanishi hauko correct ila kuna vitu vingi unavyovizungumza viko theoretical sana)

Umezungumza kwa nini mtu akisema mimi sinywi pombe mara nyingi anaishia kunywa pombe sana zaidi ya mwanzo au akisema mimi sifanyi ngono anaishia kuwa mfanya ngono zaidi.

Iko hivi, jaribu kuchukua kioo ujiangalie halafu useme maneno haya kwa wiki moja mfululizo
  1. "KAMWE WEWE HUANYWI POMBE, WEWE UMESHAACHA KABISA TABIA YA KUNYWA POMBE, HONGERA SANA KWA KUACHA POMBE "
  2. "KAMWE MIMI SINYWI POMBE, MIMI NIMEACHA KABISA TABIA YA KUNYWA POMBE, NINAJIPONGEZA SANA KUACHA KUNYWA POMBE"

Kwenye kesi mbili hapo juu subconcious mind yako itaelewa kwa haraka sana command ya kwanza na kuifanyia kazi mara moja na utaacha kunywa pombe, lakini kwa kesi ya pili itakuchukua almost miezi mitatu kuacha tabia ya kunywa pombe na usipokua makini unaweza ukaendelea kuwa mnywaji wa hatari kuliko hapo mwanzoni.

kwa nini??

Kwa sababu ya social setup subconcious mind ina tabia ya kuamini kuwa inachoambiwa na mtu "mwingine" hata kama ni wewe mwenyewe ukajiita "wewe" kiko serious sana kuliko ukiiambia wewe mwenyewe kwa sababu ya tendency za watu kutojiamini na ili ikubali command ya kesi ya pili inabidi uzunguke sana kwa kutaja angle nyingi katika maisha yako ambazo unadhani ndio chanzo cha wewe kuanza tatizo hilo.

Mfano kama wewe ni mywaji na unataka kutengeneza affirmations kwa kutumia nafsi ya kwanza yaani MIMI itabidi ugusie na suala la marafiki, suala la kupenda starehe, suala la kipato, suala la stress, athari za kiafya na mengine mengi ambayo inawezekana ni possibilities za wewe kuwa cha pombe.
Na utajikuta unatengeneza "affrimations" nyingi mno kwa issue ndogo sana na ikibidi wakati wa kujisemea useme kwa hisia vinginevyo haitakuchukulia serious kwa kuwa always you are not serious when it comes to personal issues, kifupi unaamini sana watu wanasema nini kuliko wewe unajisemea nini. Na subconcious mind inakujua mno katika hilo

Lakini ishu hiyo hiyo ukitumia nafsi ya pili(WEWE) badala ya MIMI hata kama utatumia phrases chache na wakati wa kuzisema ukawa hauna emotion yoyote na hata kama kuna a little bit of negativity katika statement zako bado itazichukua zote na kuzifanyia kazi zote tena kwa haraka sana, kwa kuwa wanadamu daima wanajali sana wanayoambiwa na watu kuliko wanayojiambia wenyewe na wanaogopa sana wengine wanasema nini kuhusu yeye kuliko yeye anasema nini kujihusu yeye.

Na labda nikwambie tu paradox moja kuwa subconcious inaiamini sana sauti yako lakini haikuamini wewe kwa sababu hata wewe mwenyewe haujiamini, na pia haina uwezo wa ku reason kama ilivyo concious mind hiki kitu mpaka leo wanasayansi wanakishangaa
 
A Asigwa. Darasa zuri. Endelea kushusha nondo kwani majibu yako haya ni shule tosha.

Mimi tatizo langu kubwa ni procrastination. Yaani naweza kuwa na ishu muhimu na naweza kuianza vizuri tu halafu inaishia njiani. Halafu deadline ikikaribia basi naji-stress wee naimaliza kabla lakini (obviously) kazi inakuwa si kwa kiwango cha exceptional. Jambo hili huwa linanikera na kuniumiza sana. Yaani hata nikijilazimisha kabisa kabisa naishia tu kuwa stressed out. Tatizo hapa ni nini mkuu na nawezaje kuishinda tabia hii kwa kutumia techniques hizi unazofundisha?

Na procrastination hii inajitokeza hasa kwa kazi za kiofisi. Manual labour hata uniambie nipalilie eka nzima nitaimaliza kwa siku moja na nusu lakini ukiniambia niandike report au nifanye homework/project hapo ndipo kimbembe sasa yaani nitajikongoja wee na mwisho naishia kuiripua tu. Why? Na Wil power yangu pia siyo legelege kwani niliweza kuacha sigara kwa kuamua tu na huu ni mwezi wa tisa sijagusa pombe baada ya kuamua kuacha mwanzoni mwa mwaka huu. Ila hapo kwenye procrastination ndipo nimekwama. Nitashukuru sana kwa msaada wako na wajuzi wengine wa masuala haya!
 

Ku visualize ndio inakuaje mkuu naomba elimu juu ya hii kitu
 
mi naamini Mungu ndio anaweza kunifinyanga na kuondoka tabia mbaya pale ninapomwomba.nimeshafanikiwa kwa baadhi ya tabia na nyingine mbaya zitaondoka tuu kwa msaada wa Roho mtakatifu

Kweli kabisa mkuu.
 
Ku visualize ndio inakuaje mkuu naomba elimu juu ya hii kitu
Ku visualize ni kitendo cha wewe kutumiauwezo wako wa kuona jambo kwa kutumia jicho la ndani, yaani ni jumla ya picha zote na matukio kama yanavyoendelea nadni ya kichwa chako(Moyo wako) mfano nikikuambia unamfahamu simba??
Automaticaly picha ya simba inakujia kichwani.

Nikikuambianimekutana na mama yako mzazni automatically sura(picha) ya mama yako inakujia kichwani hata kama uko mbali naye.

Sasa katika kuvisualize unatengeneza picha na mazingira ya namna unavyotaka uwe na unairudia mara kwa mara katika kichwa(moyo) wako ukiwa tayari unajiona umeshafikia lile lengo unalotaka kufikia, na hapo ndipo mind yako huchukua na kukileta kile ambacho umejiambia kwa muda mrefu.

Mfano kama unataka kuacha kuvuta sigara, inabidi ujitengenezee picha kichwani ukiojiona umeshaacha kuvuta sigara kabisa(hata kama kwa sasa bado unaendelea kuvuta) mind yako itachukua picha hiyo na kuifanyia kazi na automaticaly utachukia mno uvutaji sigara na utajikuta hata unasahau ni lini ulivuta kwa mara ya mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…