Namna ya kupika mtori

Namna ya kupika mtori

sacha

Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
76
Reaction score
11
Msaada jaman...naomba kuelekezwa namna ya kuandaa mapishi ya mtori..
 
Ingredients;
Ndizi msale
Kitunguu
Karoti
Nyama
Chumvi
Supu

Mapishi;
Kwenye sufuria katia ndizi zako vipande vidogo katia karoti na vitunguu,miminia supu ifike nusu sufuria ila isifunike ndizi zote weka jikoni kwa mda wa dakika15 mara kwa mara uangalie maji yasikaukie,then pepeta zile ndizi za chini zije juu huki ukiongezea supu baada ya dakika 15 chukua mwiko bonyeza kuona kama imeiva kama ndio weka chumvi na ongeza supu ,zima jiko weka pembeni anza kuponda na kipekecho au whisker usiwe mzito sana uwe unaongezea supu uzito ni wastani.ikiwa tayari korogea nyama yako iliyoiva kama umepoa unaweza rudisha jikoni ukachemka tena.
Nb.wengine husaga na blender na mwishoni hutia kijiko kidogo cha siagi.
😀 adios!
 
Ahsante ntafanya kwa maelekezo...samahan lazima ndizi mshare...?
 
nafikiri ndizi bukoba ama ngombe kwa uchagani zinafaa zaidi. ila pia ukiweka na viazi kidogo huongeza ladha nzuri zaid.
 
nafikiri ndizi bukoba ama ngombe kwa uchagani zinafaa zaidi. ila pia ukiweka na viazi kidogo huongeza ladha nzuri zaid.

mwali ushawahi kuuweka magimbi yale madogo madogo!
uuwih mwisho wa habari!
ukiandaa na chapati za kitabu!unaweza kung'ata ulimi ujue!
 
nafikiri ndizi bukoba ama ngombe kwa uchagani zinafaa zaidi. ila pia ukiweka na viazi kidogo huongeza ladha nzuri zaid.

ni kweli hizo ndizi ni pouwa coz ni laini, vilevile waweza kuweka mafuta ya ng'ombe kwenye hiyo nyama unayochemsha kama ni mzazi,..
 
amelinem hakuna vipimo halafu kumbe mtori unatiwa karoti, new to me. thanx
 
Last edited by a moderator:
amelinem hakuna vipimo halafu kumbe mtori unatiwa karoti, new to me. thanx

si ndo mitori ya kisasa hiyo, mtori niliofundishwa mimi kama ni chakula cha mtu 1
mahitaji:
  1. ndizi 7-10 inategemea na mlaji mwenyewe(ngombe au mchare laini au bukoba)

  • magimbi yale meupe (kwetu twayaita sowe) wengine viaz mbatata vile vya chips
  • mafuta ya ng'ombe au mbuzi (ukinunua nyama unamwambia akupe na mafuta kiasi)
  • chumvi
  • K/vitunguu
  • Nyama ya ng'ombe au mbuzi kiasi ni wewe na mapenzi yako kwenye nyama
maandalizi & Mapishi

  • Osha nyama yako vizuri na uikate vipande vidogo kias kisha weka jikoni hakikisha ipo supu ya kutosha

  • menya ndizi zako kisha zikate ndogondogo (mm nlifundishwa kukata kwa urefu (siku nikikata ntakuonesha picha uone)
  • menya magimbi yako hayo au viazi mbatata (kwa hayo magimbi kata kwa wembamba kama crips coz ni magumu tofauti na ndizi huchelewa kuiva) kwa viaz mbatata kata mara mbili/tatu kutegemea na size ya kiaz
  • osha vizuri ndiz zako, kwa ndizi bukoba au ngombe zichemshe kidogo kisha umwage maji coz zina ukakasi(utomvu) sana, na magimbi fanya hivyo hivyo ila kwa viaz mbatata haina shida au mchare laini
  • panga magimbi yatangulie then ndizi juu,wakat huo nyama imeshachemka sana tu chukua yale mafuta coz hayawez kuyeyuka yote, changanya huko kwenye ndizi na zile nyama kama hazikuiva sana ili zimalizie huko kwenye ndizi,.tia chumvi kias, katia huko na kitunguu chako tia supu kias na funikia,(tulikua tunapikia kwenye chungu na tunafunika na jani la mgomba) wewe waweza tumia sufuria na ukafunika hata kwa mfuko nia ni kuzuia mvuke
  • baada ya muda kama 20mnts unaweza kuchungulia kama ukizichek kwa mwiko kama tayari epua na songa kwanza kikilainika endelea kusonga ukitia supu polepole mpaka uwe na uzito wa wastani,si mwepes au mzito sana.
  • baada ya hapo Mtori tayari...unakua na ladha ya asili maana hauwekwi makorokoro.. mi ndo najua hivi mamy...ukisaga mtori bwana unateleza sana yaan unakua laini hadi too muuch so hata ukila huwi na cha kutafunatafuna zaid ya nyama...
 
Hebu tupeni recipe za chapati za kitabu.... ameline, King'asti mnahitajika.

thanks,hizo chapati za kitabu bado sijazipata kwa kweli labda kama kuna jina tofaut na ninalolijua mim,. ila kama ni zile za kawaida haina shida, muhimu ni kujua hizo chapati za kitabu ni kitu gani..?
 
thanks,hizo chapati za kitabu bado sijazipata kwa kweli labda kama kuna jina tofaut na ninalolijua mim,. ila kama ni zile za kawaida haina shida, muhimu ni kujua hizo chapati za kitabu ni kitu gani..?

Ni zile chapati zinazofanya layers, yaani zinajichambua zenyewe, laini...hasa huwa ni zile zilizopikwa na samli na ufundi wa kukanda.
 
Chapati ukizikanda vizuri usiku halafu uzifunike mpaka asubuhi ndo upike zinakuwa laini ajabu. mahitaji watakujuza.
 
Back
Top Bottom