Namna ya kupika Pilau

Namna ya kupika Pilau

Napenda sana haya mapishi yako. Ila unatumiaga misamiati migeni sana kwangu.
Namba 4 "vitunguu thomu" ndio vitunguu gani.?!

Samahani kwa hiyo misamiati sikusudii kuwa confuse wengine bali tu hutokea si unajua tunatofauti kiswahili....

Kitunguu thomu ni kitunguu saumu
 
Samahani kwa hiyo misamiati sikusudii kuwa confuse wengine bali tu hutokea si unajua tunatofauti kiswahili....

Kitunguu thomu ni kitunguu saumu

Ahsante sana.
Mapishi yako sasa yamekuwa applicable sana hapo home sasa hv. Endelea hivyo hivyo,GOD will bless you.
 
Umewahi kuchanganya na njegere ama mahindi? Inapendeza zaidi...unatia hiyo mixed vegetables wakati unapamimina mchele.

Mahindi hayabadili ladha ya pilau?!
 
Mahindi hayabadili ladha ya pilau?!


Hapana kuna yale kwenye mixed vegetables pamoja na green peas na carrot yanakua sana frozen ushajua? Unaweza weka yale
 
Heshima iwe kwako.
Mahitaji

1)nyama/kuku
2)mchele kg 1
3)vitunguu maji 3 vikubwa
4)vitunguu thomu 1 kidogo
5)pilipili manga kidogo
6)uzile 1(bizari ya pilau) tbsp
7)mdalasini kijiti 5 vikubwa au kama ni wa unga 1 tbsp
8)hiliki 15
9)zabibu kavu kiasi

Namna ya kutaarisha

1)kata kata nyama/kuku then add maji saga kitunguu thomu na tangawizi tia na chumvi kiasi na uchemshe hadi viwive
2)weka mafuta robo kikombe kwenye sufuria safi weka jikoni hadi mafuta yawe moto then tia vitunguu maji ambavyo umevikatakata vikaange hadi viwe brown
3)weka mdalasini hiliki uzile zabibu na pilipili manga then changanya kwa dakika 2
4)weka soup yako pamoja na nyama/kuku kwenye mchanganyiko wako visubirie vichemke kwa dakika 5
5)add maji kulingana na mchele wako unavohitaji ili uwive vr
6)weka mchele wako then funika hadi uwe umewiza
7)then waweza kuutia kwenye oven kwa dakika 10 ili ukauke vizuri

8)pilau tayari kwa kuliwa
 
Itabidi nibadilike pilau nakula shighulini tu,ngoja nipike nione itakuwaje
Nalog off
 
Asante sana penda mapishi yako kaaa mpembaa atiiiiii[emoji14]
 
Back
Top Bottom