Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Process yake ni ndefu ndugu...duuh maana sijui nianze vipi.
tafuta sehemu iliyo elezea kiurahisi umuwekee..
hahaha mwambie baada ya ingredients kuwa tayari atengeneze chapati ambazo akizisukuma zinakuwa nyembamba sana kama karatasi kisha akate pembetatu, halafu akaroge pembeni uji wa ngano mzito kama ule wa keki au chapati za maji hii ndio gundi ya kuungia hizo sambuza.Kwanini nitafute ya mtu mwingine, naweza kumpa mahitaji/ingredients lakin vipi nitamweleza jinsi ya kukunja sambusa.:confused2:
Kwanini nitafute ya mtu mwingine, naweza kumpa mahitaji/ingredients lakin vipi nitamweleza jinsi ya kukunja sambusa.:confused2:
Bora tutengeneze burger ama kebabs. Sambusa uvivu kweli jamani, mhh
hahaha mwambie baada ya ingredients kuwa tayari atengeneze chapati ambazo akizisukuma zinakuwa nyembamba sana kama karatasi kisha akate pembetatu, halafu akaroge pembeni uji wa ngano mzito kama ule wa keki au chapati za maji hii ndio gundi ya kuungia hizo sambuza.
Halafu jinsi ya kufunga ni kama vile anamfunga mtoto nepi. nafikiri hapo atakuelewa.
Sasa tunaomba utupe hizo ingredients maana jinsi ya kufunga nafikiri nimekusaidia au vipi MadameX
hizo chapati nyembamba azam ashakutengenezea,
msaada hapo kwenye kotmiri! hii ni kitu gani? au inajina lingine naweza kuitambua!? naomba kujulishwaMahitaji Manda ya sambusa ya tayari Kiasi zinavyouzwa Nyama ya Kusaga au kuku iliyosagwa 1/2 kg Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa 3tsp Pilipili mbichi iliyosagwa 1 tsp Pilipili manga iliyosagwa1 tsp Giligilani iliyosawagwa1 tsp Chumvi kiasi Vitunguu maji vilivyokatwa (chopped) Kikombe kimoja Karoti iliyokatwa (grated) nusu kikombe Kotmiri kiasi 2 Soup cube (optional) Mafuta ya kukaangia Gundi 3/4 kikombe unga ngano 1/4 maji changanya pamoja, ikumbukwe lazima uwe mzito hivi ili igandishe zaidi. Mataarisho Pika nyama/kuku ya kusaga kwa kutia chumvi, vitungu saumu, tangawizi, pilipili na ndimu acha ichemke mpaka ikauke. Ongeza maji ya pili ya kutosha kama vikombe 3 ili iive zaidi tia hizo soup cube kama unazo lakini sio lazima. Kabla haija kauka tia pilipili manga na giligilani. Zima moto acha kidogo ipoe tia vitunguu, karoti na kotimiri. Funga sambusa katika manda kama kawaida kwa kutumia gundi, hakikisha hakuna matundu. Pika sambusa katika mafuta ya moto hadi ziwe golden brown ondoa taya kwa kuliwa. Nafikiri hapa panatosha, nikipata picture za ukunjaji nitakuwekea, umenipata Dine
Mahitaji
Manda ya sambusa ya tayari Kiasi zinavyouzwa
Nyama ya Kusaga au kuku iliyosagwa 1/2 kg
Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa 3tsp
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 tsp
Pilipili manga iliyosagwa1 tsp
Giligilani iliyosawagwa1 tsp
Chumvi kiasi
Vitunguu maji vilivyokatwa (chopped) Kikombe kimoja
Karoti iliyokatwa (grated) nusu kikombe
Kotmiri kiasi
2 Soup cube (optional)
Mafuta ya kukaangia
Gundi
3/4 kikombe unga ngano
1/4 maji
changanya pamoja, ikumbukwe lazima uwe mzito hivi ili igandishe zaidi.
Mataarisho
Pika nyama/kuku ya kusaga kwa kutia chumvi, vitungu saumu, tangawizi, pilipili na ndimu acha ichemke mpaka ikauke. Ongeza maji ya pili ya kutosha kama vikombe 3 ili iive zaidi tia hizo soup cube kama unazo lakini sio lazima. Kabla haija kauka tia pilipili manga na giligilani. Zima moto acha kidogo ipoe tia vitunguu, karoti na kotimiri.
Funga sambusa katika manda kama kawaida kwa kutumia gundi, hakikisha hakuna matundu. Pika sambusa katika mafuta ya moto hadi ziwe golden brown ondoa taya kwa kuliwa.
Nafikiri hapa panatosha, nikipata picture za ukunjaji nitakuwekea, umenipata Dine