SoC02 Namna ya kutatua matatizo yanayohusisha upatikanaji wa mazao ya chakula nchini

SoC02 Namna ya kutatua matatizo yanayohusisha upatikanaji wa mazao ya chakula nchini

Stories of Change - 2022 Competition

Tinov 1998

New Member
Joined
Aug 26, 2022
Posts
3
Reaction score
4
SoC 2022 Kilimo kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.

Kwa mda mrefu Sasa watanzania tunaendelea kukumbana na matatizo ya upungufu wa baadhi ya bidhaa Kama vile mafuta ya kupikia, Jambo ambalo hupelekea Bei kuwa kubwa na kuzua taharuki.
Aidha baadhi ya jitihada za serikali kupitia wizara ya kilimo ni pamoja na kuagiza mafuta kutoka nchi jirani.

Kulingana na taarifa kutoka wizara ya kilimo, Tani laki nne ya mafuta ya kupikia huagizwa kila mwaka kukidhi mahitaji ya Tani laki sita kwa mwaka.

Zifuatazo ni mbinu za kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya chakula nchini:

1. Kuandaa maeneo ya wazi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya chakula Kama vile alizeti na michikichi, mashamba hayo yanaweza kupewa vijana wavitunze kama sehemu ya kupunguza changamoto za ajira nchini.

2. Utoaji wa ruzuku kuhakikisha upatikanaji wa mbolea na mbegu bora (hybrid).

3. Uzalishaji wa mazao kimkakati (specialization in production), hii Ina maana kwamba kila mkoa iwe na uwezo wa kuzalisha zao moja kwa wingi kulingana na ekolojia ya sehemu hiyo, kwa mfano alizeti kwa mikoa ya singida, ngano mkoa wa manyara (basutu), korosho mikoa ya lindi na mtwara, lakini pia mazao mengine kama ziada.

3. Kuboresha mifumo ya umwagiliaji, hii itasaidia kuongeza uzalishaji hata kipindi ambacho si Cha uzalishaji (off season).

4. Kuongeza wataalamu katika idara ya uzalishaji, wataalamu wenye ujuzi wakutumia teknolojia ya kisasa ( computerized Agriculture). Hii ni pamoja na kuingia uhisani na nchini kama Israel ambao wameboresha kilimo Chao.

5. Kuboresha idara ya utafiti wa kilimo ili kupata teknolojia imara na madhubuti itakayowafikia wakulima kwa haraka.

6. Serikali kuwekeza nguvu kubwa katika kuboresha kilimo nchini, ikiwa ni pamoja na pesa, vitendea kazi (machine) na masoko.

From
Tinoboy
0688503442
0559886431
 
Upvote 2
Back
Top Bottom