SoC04 Namna ya kutatua tatizo la ajira Tanzania

SoC04 Namna ya kutatua tatizo la ajira Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Apr 20, 2024
Posts
25
Reaction score
26
UTANGULIZI.
Kuna Msemo unasema kuwa "Ajira ni chache ila kazi ni nyingi". Hii inatupa tafsiri kuwa, ajira zinapatikana kwa uchache sana ila kazi (Kujiajiri)/Fursa, zipo nyingi na hii inategemea na uwezo wa mtu (Taifa) kuziona fursa hizo na kuzibadili kuwa fedha na kutengeneza ajira kutoka katika hizo fursa.
Kwa mujibu ripoti ya Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini Tanzania (REPOA) ya 2019, takribani vijana milioni moja wanahitimu kila mwaka kutoka taasisi mbalimbali za kielimu, huku idadi ya ajira zinazozalishwa kutoka serikalini na sekta binafsi ni 250,000, kwa wastani wa kila mhitimu anatumia miaka 5.5 kupata ajira.

Serikali imesema "Asilimia 12.2 ya vijana kati ya umri wa miaka 15-35, nchini Tanzania hawana ajira. Asilimia hiyo ni sawa na 1,732,509 kati ya nguvu kazi ya vijana 14,219,191 wenye uwezo wa kufanya kazi, Kwa maana ya vijana walio katika umri huo na Hawapo katika mafunzo wala hawana ulemavu inayosababisha wasijihusishe na shughuli za kiuchumi. Chanzo: Patrobasi katambi (Bungeni- February 3, 2023).

images (1).jpg

Chanzo: Google.


MAMBO YAFUATAYO YAKIFANYIWA KAZI YATAWEZA KUONDOA KABISA TATIZO SUGU LA AJIRA TANZANIA.

1.
Kutumia aridhi isiyotumika (Idle land) na kugeuza kuwa mashamba (Maeneo ya Kilimo).
Tanzania, Tumejaliwa kuwa na ardhi kubwa, ni sehemu ndogo tu inayotumika ila sehemu iliyobakia haifanyiwi kazi ipasavyo, hivyo sehemu zote zenye mapori/vichaka/Mabonde. Vinaweza kufyekwa na kuandaliwa kwa ajili ya kufanya kilimo na maeneo hayo yatakabiziwa kwa vijana waliopo mtaani na wale wanaomaliza elimu na kuingia mtaani kutafuta ajira, Hivyo watapewa hekari 1 mpaka 2 kila kijana na kuwezeshwa kwa mitaji, vyanzo vya umwagililiaji na elimu kuhusu kilimo na watalima mazao ya Chakula na Biashara ili kuweza kujimudu na hii itasaidia kupunguza janga la ajira.
*** Nitoe angalizo hapa.
- Kwa kufanikiwa katika kilimo, Tutegemee kuwa na mazao mengi sana, hivyo mipaka ya kuuza mazao nje ya nchi ifunguliwe na masoko mengine ya nje ya nchi yatafutwe ili kuhakikisha wakulima wote wanafaidika kwa kuuza mazao yao nje ya nchi kwa faida nzuri ili kuwa motisha kwa wakulima.

images.jpeg

Chanzo: Google.

2.
Serikali Kuziwezesha sekta binafsi na Kuweka mazingira/sera bora ya uwekezaji kwa mashirika toka nje ya nchi.
Taasisi zote zisizo za kiserikali, ambazo zinasua sua katika ukuaji, serikali inaweza kuzipa uwezo/mitaji katika ukuaji, Pia mazingira/sera shawishi kwa wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza, hii itasaidia kwa wao kuajiri baazi ya watu na kupunguza kwa sehemu hii changamoto ya ajira.

3. Kutoa Mitaji kwa Vijana wote wenye mawazo bunifu. (Uwezeshaji wa Tekinolojia & Ujasiliamali).
Kuna wimbi kubwa la vijana wenye mawazo ya Ujasiriama/Ubunifu. Serikali iwe na jukumu la Kuwapa mitaji au kutumia Taasisi za kifedha ili Kuwapa mitaji na kuwasaidia hatua kwa hatua katika kutekeleza mawazo yao na kuwa halisia.

4. Kuboresha mitaala ya elimu ya awali mpaka juu, iwe ya kimataifa.
Wahitimu wa elimu ya Tanzania, wamekuwa wakipata wakati mgumu sana katika ushindani wa soko la ajira hasa kwa kazi za kimataifa kwani, mitaala yetu imekuwa inalenga soko la ndani zaidi na wachache sana wanafanikiwa kushinda ila wengi wao wanakosa Kwa sababu ya kutokukizi vigezo. Hivyo elimu ya ujuzi (Field/ Practical studies) Inatakiwa kuwa 50% na elimu ya darasani (Theoretical studies) kuwa 50% ili wanafunzi waweze kuwa na uwiano mzuri katika ujuzi na masomo.

5. Somo la Ujasiliamali & Tekinolojia lipewe kipaumbele.
Dunia inaenda Kasi sana na mifumo ya kitekinolojia Inakua kwa Kasi sana kila siku, hivyo ili kuendana na mabadiliko ya kitekinolojia basi ni vyema somo hili lipewe kipaumbele. Ujasiliamali kama; Ufundi, Ujenzi na kujitegemea, vinahitajika kupewa kipaumbele Kuanzia shule za awali mpaka juu ili kuwa na kizazi chenye kuweza kujitegemea na chenye maarifa na ujuzi wa kutosha ili kupunguza kutegemea kuajiriwa.

6. Wazazi waandae mazingira wezeshi kwa watoto wao kujitegemea/Kujiajiri.
• Wazazi kuwawekea akiba watoto wao toka wakiwa wadogo na matarajio ni kuwa wakimaliza elimu basi wataweza kuwa na fedha ambayo itawasaidia wao kuanzisha Biashara ambayo itawasaidia Kujiajiri kwani kilio cha vijana wengi ni kukosa mtaji na hii itaweza kuwa suluhu zaidi ya kusubiri Kukopeshwa. (Serikali inaweza kuweka hii kama sera).
• Wazazi wawaandae watoto wao kujifunza Kujiajiri na kujitegemea bila kutegemea ajira.

7. Serikali iweke fungu kwa budget ya kila mwaka kwa ajili ya kuwasaidia vijana (Fungu la kuwainua Vijana).
  • Hii itaenda moja kwa moja kwa kuwasaidia vijana na itakuwa inakopeshwa kwa vijana wote ambao hawana ajira, mkopo unaweza kuwa Mil 1 mpaka Mil 2 kwa kila kijana. Vigezo na Mashariti vutawekwa ili kijana kupata huo mkopo na namna ya kurejesha ili walau mkopo huo utumike Kukopeshwa wengine yaani kama vile Loans board inavyofanya.
  • Elimu pia itolewe Kwa vijana kuwa wanahitaji kujitegemea na kuondokana na dhana ya kutegemea kusaidiwa na serikali kwani mara zote haitoweza kumaliza yenyewe tatizo la ajira ila Inatakiwa kusaidiana Kati ya Wazazi, Vijana wenyewe, Taasisi Binafsi na Jamii yote kiujumla.

HITIMISHO.
Baada ya kufanya mambo hapo juu kama taifa tunaweza Kufanikiwa kupunguza kama sio kuondoa kabisa tatizo sugu la ajira na kujenga kizazi
kinachoweza kujitegemea na Kujiajiri na kuondokana na dhana ya kusubiri ajira.
- Tanzania Bora na nzuri tuitakayo inawezekana ila kwa kuondokana na fikra ndoto na kuingia katika vitendo yaani kuyafanyia kazi yale tunayojua ni sahihi badala ya Kulalamika au kubaki katika ndoto.
 
Upvote 4
Kutumia aridhi isiyotumika (Idle land) na kugeuza kuwa mashamba.
Tanzania, Tumejaliwa kuwa na ardhi kubwa, ni sehemu ndogo tu inayotumika ila sehemu iliyobakia haifanyiwi kazi ipasavyo, hivyo sehemu zote zenye mapori/vichaka/Mabonde. Vinaweza kufyekwa na kuandaliwa kwa ajili ya kufanya kilimo na maeneo hayo yatakabiziwa kwa vijana waliopo mtaani na wale wanaomaliza elimu na kuingia mtaani kutafuta ajira, Hivyo watapewa hekari 1 mpaka 2 kila kijana na kuwezeshwa kwa mitaji, vyanzo vya umwagililiaji na elimu kuhusu kilimo na watalima mazao ya Chakula na Biashara ili kuweza kujimudu na hii itasaidia kupunguza janga la ajira.
Sawa kilimo ni bonge la fursa, 'potential fursa'. Kilio chetu tu ni soko la hizo bidhaa zake.

Hadi hivi sasa, wakulima sio wenye kuonesha hali nzuri za kimaisha sasa hao vijana watavutiwa vipi.

Soko linaweza kuibadili kabisa hii tasnia. Fikiria tu kama mkulima wa ufuta atakuwa na ufikiaji wa soko la dunia na akapata malipo ya mojakwamoja kutoka soko la dunia?

Kilimo kinatoa sana, mifano tu wale wazee wanaojazaga fuso za viazi vya chipsi njombe na Iringa, wanaouza miti. Wakulima hawa wamefanikiwa kwa sababu uhitaji wa soko la ndani ni mkubwa hivyo wanapata thamani halisi ya mazao yao.

Lakini kwa mazao ambayo soko la ndani halitoshi, wakulima wake wana hali ngumu na haikupaswa kuwa hivyo. Mfano mahindi.
A. Kipindi yanauzwa nje wakulima huneemeka na taifa kwa ujumla linastawi (fedha za kigeni)
B. Yasipouzwa ni mdororo tu kuanzia mkulima hadi nchi.

Sasa tujiulize kama nchi, nawe mtoa mada. Je? Yuendelee kuwasikiliza wasiolima wanapolalamika kuhusu kupanda kwa bei za chakula. Au tuitumie hiyo kama fursa ya kuwavutia wawekezaji wakubwa kwa wadogo(vijana) mara watakapoona thamani ya kilimo?

Kutoa Mitaji kwa Vijana wote wenye mawazo bunifu. (Uwezeshaji wa Tekinolojia & Ujasiliamali).
Kuna wimbi kubwa la vijana wenye mawazo ya Ujasiriama/Ubunifu. Serikali iwe na jukumu la Kuwapa mitaji au kutumia Taasisi za kifedha ili Kuwapa mitaji na kuwasaidia hatua kwa hatua katika kutekeleza mawazo yao na kuwa halisia.
Ewaah! Tumeshuhudia balozi na mashirika (mengi yakiwa ya nje) kuja kutafuta ubunifu na kuupatia fungu. Ni wakati sasa wa serikali kuweka fungu kwa ajili hiyo.

Mfano, kwa kuwa vijana wengi tu ni maafisa ubashiri tayari inaweza kufanyika kama 'national lotto' betting ya kitaifa😅. Ipoje hii?;
1. Inakuwa na michezo mingi ya ubahatishaji
2. Kanuni za ubashiri kutumika.
3. Sheria ya msingi ni, kila mtu ili ajiunge ni lazima aweke vyeti vyake na zaidi aweke mpangokazi 'bussiness plan' ya atakachofanya akishinda bahati nasibu hiyo. LAZIMA.

Kitakachotokea ni wachache watakaoweza kushinda watasimamiwa kufanya miradi yao. Na kwa kuwa ni wachache watashiriki (sharti gumu la bussiness plan) basi nafasi za ushindi zitakuwa nyingi tu.

Wale wasioshinda watakuwa wameweka mawazo yao public. Ndiyo anayetaka public funds lazima afanye public service ya kukuza akili ya public. Watasisimua watu kuboresha na kufanyia kazi mawazo hayo. Unaweza juhisi ni hasara kwa mwenye wazo lakini la. Mwenye wazo kiotomati atakuwa na hati miliki ya wazo lake na ni lazima afaidike na bidhaa zitakazozalishwa kisheria.
HITIMISHO
Baada ya kufanya mambo hapo juu kama taifa tunaweza Kufanikiwa kupunguza kama sio kuondoa kabisa tatizo sugu la ajira na kujenga kizazi
kinachoweza kujitegemea na Kujiajiri na kuondokana na dhana ya kusubiri ajira
Ahsante sana, una mawazo ya kujenga sana
 
Asanteee sana kwa uchambuzi akinufu, nimejifunza zaidi na naendelea kujifunza...

Asanteee sana kwa maoni Yako kaka
 
Back
Top Bottom