Namna ya kuuaga umasikini

Namna ya kuuaga umasikini

Nakubaliana na wewe jambo Moja hapo kutafutia mafanikio nyumbani ukianza kunyanyuka kidogo kuna changamoto zake hasa ndugu na jamaa kujiona na wao ni wamiliki wa biashara yako au kazi mwisho wa siku usipokuwa makini juhudi zako zitakwama
Comment yangu naianzia kutoka hapa umeongea kitu nilichowaza mimi.

Concept ya maskini au utajiri ni ndefu sana.

Kama ukoo wako ni maskini inahitaji ushujaa wa hali ya juu sana kuwa kutajirika.

Kwa sababu ukianza kupata mafanikio utalazimika mafanikio yako yajigawe kuwasaidia ndugu zako wote ambao bado ni maskini mwisho wa siku unarudi nyuma tena badala ya kwenda mbele.

Vinginevyo inatakiwa uwafundishe mbinu iliyokufanya ufanikiwe ambayo wapo watakaokuelewa na wengine hawatokuelewa,hii strategy ikiendelezwa itakuja kuonekana impact yake kwenye kizazi chenu cha pili wakati huo mlioanzisha mshazeeka.
 
Watu wengi wanafikiri kuwa hawawezi kutafuta hela ili wawe matajiri. Kumbe hawajui kutumia hela ( hapa simaanishi uwe bahili tafadhali mana ma bahili wanaweza kujipatia ujiko hapa)
 
Una maanisha tuna matumizi mabaya ya fedha?
Watu wengi wanafikiri kuwa hawawezi kutafuta hela ili wawe matajiri. Kumbe hawajui kutumia hela ( hapa simaanishi uwe bahili tafadhali mana ma bahili wanaweza kujipatia ujiko hapa)
 
Ndio hvyo mkuu.

Utajiri unaouona kwa wafanya biashara matajiri wa kihindi na wachina hawakuanza wao bali walianzisha babu zao hao wanaendeleza gurudumu.

Mimi binafsi siwezi kujiona tajiri kama ndugu zangu hawana uhakika wa milo 3 kwa siku.

Sitajiona tajiri kama ndugu zangu hawamudu kuwalipia watoto wao ada.

Sitajiona tajiri kama ndugu zangu hawana uhakika wa pesa ya matibabu.

Sitajiona tajiri kama ndugu zangu hawana nyumba nzuri za kuishi.

Sitajiona tajiri kama ndugu zangu wa kijijini wanakosa hata pesa ya kununua chumvi na mafuta ya koroboi.

Kwa hiyo inategemea mtu anawazaje kuhusu utajiri
Mr dengue... strategy hiyo ni nzuri ila inahitaji surcrifice ya vizazi 2 kuishi maisha ya jasho
 
Zote mlizotoa sio mbinu. Mbinu zipo 3 tu.
1. Fanya kazi kwa bidii sana
2. Weka malengo na hakikisha unayatimiza
3. Kuwa na discpline ya pesa
Mimi hizo mbinu ulizotaja zote nimezitumia tangu niko shule hadi leo hii ni mtu mzima na bado sijatajirika.
Nafikiri kuna siri zingine za ziada ila sio hizi.
 
Back
Top Bottom