Uko sahihi, kwa leo naomba tuanze na somo la vitendo la kuhakikisha bidhaa yako inapatikana kwenye maduka 1000 yanayokuzunguka.
Fanya uzalishaji kutokana na mtaji wako
Piga mahesabu kwa kila unit moja unayozalisha unatakiwa uuze kiasi gani, mfano 500
Ongeza bei kidogo kwa kila unit kwa yule mwenye duka atakayekuwa anakuuzia, mfano 50
Kwa hiyo utabeba bidhaa zako kwa makubaliano kwa kutembelea hayo maduka 1000, na kuwapa bei elekezi 550, ya kwako ni 50 tu.
Hapo utafanikisha kusambaza bidhaa zako.
Kuhusu 'awareness' hilo ni somo lingine kwenye 'marketing'; unaweza kulipia tangazo kwenye vyombo vya habari, unaweza kuwatumia vijana waliosomea masoko kwa ngazi ya cheti, unaweza kutumia mitandao ya kijamii; bahati nzuri vijana wengi ni jobless, wanaweza kukusaidia katika baadhi ya kazi kwa ujira mdogo/ kamisheni.