Namna ya kuweza kutunza mshahara wako ukutane na wa mwezi unaofuata

Umemaliza mkuu
 
Hoja nzuri Sana hii

Hapo kwenye suluhisho ...hiyo Point no 04 watu wakiizingatia ,watafanikiwa ...Watu wakubali kuishi kawaida kabisa ..haya Mambo ya kujifanya wa kisasa ,kununua ma vitu ya gharama ,starehe ,matumizi Bila budget ,wakati unakipato constant ni mbaya Sana...Utalaumu mshahara hautoshi ..kumbe huna budget .... Tujifunze kuishi kulingana na vipato vyetu..

Utashangaa mtu kwa wakati wa lunch baada ya chakula ananunua juice ,soda, maji kwa wakati mmoja, wakati ni Unnecessary ..au Aina ya usafiri anaotumia hauko constant ..Leo kapanda daladala, kesho bolt. ,siku nyingine boda ..Yan hana mfumo maalumu .... Kuishi Bila mpangilio ndo kunafanya watu waseme Mshahara haukai. ..Sasa utakaaje wakati huna budget ..unaishi ishi tuu

Kivyovyote vile hata kama unaingiza pesa ya kawaida. Jifunze utamaduni wa ku save...life is tough kwel kweli ..
 
Hapo kwenye chakula kama utafanikiwa kununua vyakula vyote muhim ukaweka ndan kama mchele maharage unga sukar etc itakusaidia kupunguza gharama mana rejareja ni gharama zaidi.. pia kama na friji likiwepo mkamnunua viungo angalao kila wik au wik mbil nayo itasaidia kupunguza gharama..mana utaenda kununua sokon ndo bei nafuu tofaut na gengen.

Pia mkaa ukitumika kuchemshia vitu kama nyama maharage makande au hata kupikia wali..ges inakua imebak na mapishi ya vyakula visivyokaa mda mrefu jikon.

Kwenye kusuka hapo kwa budget hiyo angalao kwa mwez isizid 20,000 kwa ajil ya mama watoto kusuka.Wanawake tuna misuko mingi na yenye gharama sana tu Ila kwa mazingira hayo bibie anatakiwa awe mwelewa tu asiwe complicator kwa kutaka misuko ya kuanzia may be ya kuanzia fifty huko.

NACHOWEZA KUKUSHAURI KAMA MAMA WATOTO SIO MFANYAKAZI WA KUAJIRIWA AU KUJIAJIRI...JITAHIDI UMTAFTIE KITU KAMA BIASHARA YENYE MTAJI UTAKAOWEZA KUUMUDU KULINGANA NA UCHUMI WENU MUWE NA MALENGO YA KUINGIZA FAIDA YA ELFU KUMI TU KWA SIKU. KUNA BIASHARA NYINGI ZINATUMIA MTAJI WA CHINI YA LAKI MOJA NA MKAPATA ELFU KAMA FAIDA YENU KWA SIKU..
 
Umeongea ukweli mtupu
 
Mtoa mada umetoa mwongozo mzuri sana kwa watu wenye kipato constant! Kwa wale ma junior katika kazi mie nashauri tutafute tu kamradi angalau hata ka kuingiza dh. 5000/= net profit Aisee! Mshahara haujawahi kumtosha mfanyakazi hata Siku moja.Nahisi mshahara umelaaniwa!!! Imagine unachukua hela tat 30 unaiweka kwenye mto wa kulalia kisha kila Siku ni minus hakuna plus mwisho wa Sikh unakuta hela imeisha
Kuna jamaa yangu ananunua bahasha za khaki kisha anapaki hela kulingana na budget mfano
(1) Sokoni tsh 2000×30=60,000/=(anaipaki kwenye bahasha juu imeandikwa SOKONI
(2)Kitafunio tsh 2000×30=60,000/=(anapaki kwenye bahasha....)
(3)Michele tsh.30000/(anapaki....)
(4) usafiri 4000×30=120;000/=(anapaki....)
N.K .....Akishapaki anabaki hana hata tsh.mia mkononi kisha anaweka zile bahasha kwenye draw.ufunguo mmoja mke mwingine wa kwake na anajihakikishia ni marufuku Ku diverge fund yaani MF achomoe hela ya kitafunio kutoka bahasha ya hela sokoni !!
BAJETI YAKE INAKUWA STRAIT RELI NA TRAIN NA ANAFIKA NA INAMUEPUSHA KUKOPA KOPA MITAANI.
 
Vipi Kama Kuna dharura mfa kuumwa?
 
Vipi Kama Kuna dharura mfa kuumwa?
Jamaa akizidiwa alikuwa anamega kutoka kila account then anazidi kubana matumizi let say kama kama alikuwa ananunua mkate wa 2500 anaenda kwa buku mbili na alikuwa haingii salary advance kwa issue za kitoto labda msiba.
 
Hakika ni kweli kabisa...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Jamaa akizidiwa alikuwa anamega kutoka kila account then anazidi kubana matumizi let say kama kama alikuwa ananunua mkate wa 2500 anaenda kwa buku mbili na alikuwa haingii salary advance kwa issue za kitoto labda msiba.
Inahitaji nidhamu na kujitoa kwa hali ya juu hii,nitajaribu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…