Namna ya kuzuia Kichechefu wakati wa Ujauzito

Ngufumu

Member
Joined
Dec 29, 2016
Posts
25
Reaction score
44
morning-sickness-pregnancy-nausea.jpg

Je unaelewa nini kuhusu Kichechefu wakati wa ujauzito/ Morning sickness?

Kichefuchu ni dalili ya kawaida ya ujauzito, hasa wakati wa kipindi cha kwanza cha mimba(miezi 3 ya mwanzo). Hali hii inaweza kukufanya uhisi kuchefuka au kuwa na kizunguzungu na kukuacha bila hamu ya kula. Ingawa ni kawaida, kichefuchefu hiki kinaweza kuwa cha Karaha sana kwa baadhi ya wanawake kwani huweza kupelekea kutapika sana na hata kulazwa hospitali.

Habari njema ni kwamba kuna mambo unayoweza kufanya ili kusaidia kupunguza dalili nyumbani na katika maisha yako ya kila siku twende pamoja jambo la 5 lutakushangaza sana👇🏽

Tuanze kwa kuangazia maana ya Kichefuchefu cha asubuhi/ Morning sickness

Ni hali ya kuhisi kama kutapika kila asubuhi, na wakati mwingine hata wakati wa mchana au usiku. Hili ni tatizo la kawaida katika ujauzito sio hatari kwa mama au mtoto aliye tumboni, lakini kinaweza kuwa cha Karaha sana kwa baadhi ya wanawake. Naam kinasababishwa na nini 👇🏽

Sababu Za Kichefucho cha asubuhi; kinasababishwa na viwango vya juu vya homoni katika mwili wa Mwanamke mwenye mimba (homoni kama estrogen na progesterone).

Hizi homoni wakati wa mimba hufanya kazi sana na huzalishwa kwa wingi ili kudumisha(ku sustain) hali ya mama mwenyewe na mtoto wake anayekua, kwa hivyo wakati hizi homoni zinongezeka, pia kuchefuka! Hutokea

Kichefuchefu cha asubuhi kwa kawaida huisha baada ya wiki 12 za ujauzito, kwa iyo usiwe na wasiwasi ikiwa chako hakijaibuka mara moja! Au Ikiwa kinaendelea kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya mimba na ikiwa kinakusababisha usumbufu mkubwa. Zungumza na daktari wako ili akupe matibabu kama dawa au mabadiliko ya mtindo wa maisha kama kuepuka harufu zinazosababisha kuchefuka (kama vile moshi wa sigara) au kula vyakula vidogo vidogo mara nyingi badala ya milo mikubwa mitatu kwa siku kama ilivyozoeleka

Ni njia zipi sasa za kutibu kichefuchefu cha asubuhi ukiwa nyumbani?
1. Kula milo midogo midogo ambayo ni rahisi kumeng'enywa.

2. Kula mara kwa mara, hasa ikiwa unahisi kichefuchefu sana.

3. Kunywa maji ya kutosha, lakini si mengi kwa wakati mmoja - inaweza kusababisha kuhara na kukufanya ujisikie vibaya! Jaribu kunywa maji kidogo kidogo wakati wa mchana (na hakikisha pia unakunywa kabla ya kulala).

4. Epuka harufu zinazosababisha kichefuchefu, kama moshi wa sigara au manukato(perfume).

5. Epuka vyakula vinavyosababisha kichefuchefu, kama vyakula vyenye mafuta mengi au vyenye viungo vingi (kama vile pilau).

6. Kula vyakula vyenye protini kwa wingi kama vile nyama nono 😋

7. Tumia virutubisho vya vitamini B6 pamoja tangawizi kabla ya kutoka kitandani asubuhi hadi dalili zako zipungue; hii itakusaidia kupunguza baadhi ya usumbufu wakati wa miezi hii ya mwanzo!

Nini chakufanya ili kupunguza kichefuchefu wakati wa mchana?
1. Kula mlo kidogo mara kwa mara.

2. Kunywa vinywaji vyenye tangawizi kama vile chai au soda ya tangawizi.

3. Hakikisha unakula polepole na kutafuna vizuri chakula kijisage vizuri ndio umeze.

4. Pata mapumziko ya kutosha kila siku, hata kama inamaanisha kupumzika wakati wa mchana unapojisikia uchovu, kula shushu.

Hitimisho:
Njia bora ya kukabiliana na kichefuchefu cha asubuhi ni kujaribu kupumzika, lakini kuna mambo machache mengine unayoweza kufanya pia. Kwa baadhi ya wanawake tangawizi huwasaidia na kichefuchefu, wakati wengine wanapenda chai ya mnanaa (mint tea). Pia, zingatia kula mlo wenye afya na wenye usawa(balanced diet) ili usisababishe matatizo mengine kama kiungulia (ambacho pia kinaweza kusababisha kichefuchefu). Ikiwa haya hayakukusaidia basi zungumza na daktari wako akupe dawa lakini kumbuka si dawa zote zinafanya kazi kwa kila mtu(usitumie dawa aliyotumia mwenzako kwa kudhani itakusaidia na ww).

Kuendelea kupata haya na mengine mengi kupitia Whatsapp status bonyeza link👇🏽kupata namba zangu.

Asante sana

© Kaka Gift(Kagift)🤗
“Let's Connect”
 
View attachment 2999351

images.jpg
 
Back
Top Bottom