Kwa namna Yanga wanafanya mambo yao naiona kesho ya Yanga ni kubwa kuliko SIMBA
NAWASILISHA.
- Wameandika katiba ambayo wanaishi nayo sasa. Eng. Hersi ataipeleka Yanga mbali
- Wanasajili wanachama online which is a good thing....upande wa SImba mambo mengi yako kimya kimya hakuna uwazi.
- Camp ya Yanga iko serious na kisiri sana compared na Simba kila mechi ya kirafiki inaonekana in which mapungufu ya TIMU kila mtu anayaona(hii inaleta maneno sana). Training Camp ya SImba ipo open yeyeote anafika na anawaona wanavyofanya mazoezi. Yanga sometime ni closed door.
- Wanaajiri professional kitu ambacho kitawavusha
- Uswahili hauwezi kuisha lakini naona Yanga kama uswahili unapungua
- Yanga watakuja kujenga Uwanja mapema ya SImba kwa sbb ya transformation wanayoenda nayo
- Simba kuendelea kugambo na Mgunda tu peke yake itatucost huko mbeleni kwenye mechi za kiume.
- Simba mafather wengi sana na huwezi kuwaondoa kwa sbb mfumo unawabeba mfano MKUDE amechoka, Onyango amechoka, Nyoni amechka, bocco amechoa. Sasa SImba ukimdhibiti Chama na PHIRI umeimaliza timu
- Jiulize kwa nini SImba hawaweki wazi mambo yao mfano Mkataba wa MO na SIMBA hauonekani
- Yanga pamoja na kuwasponsored na GSM lakini MIKATABA ya GSM vs YANGA inaonekana wazi
- Yanga kusajili wanachama online hii ni hatua kubwa mnooooo kama wanavyofanya huko duniani.
NAWASILISHA.