1. Kama ni timu inafanya mambo kwa confidentiality ya hali ya juu basi ni Simba. Mzungu mpaka anaondoka hakuna aliyekuwa na tetesi. Na hata sasa hakuna anayejua kisa hasa ni kipi hadi ameondoka.
2. Kuhusu michezo kuonekana haina madhara yoyote maana inafanyika kwa ajili ya kuwaandaa na kuwajengea kujiamini wachezaji wasiocheza mara kwa mara.
3. Kuhusu hao uliowataja kuwa umri umeenda unaweza kutuambia ni yupi mchezaji anayeingia moja kwa moja kikosi cha kwanza msimu huu?
4. Kuhusu kocha Mgunda, unafahamu kuwa Mgunda Ameshinda mechi sawa na Nabi kimataifa? Hesabu kuanzia Nabi ameanza kazi ya ukocha.
5. Ni mkataba upi wa GSM unaosema umefanyika kwa uwazi? Mikataba yote hiyo si imetajwa tu kwa mdomo bila kuonekana popote?
6. Kusajili wanachama online kisha wasiwe wanalipia ina tofauti gani na kupata wafuasi wengi kwenye kampeni ila upate kura kiduchu?
7. Yote uliyolinganisha ni upumbavu mtupu maana kila Klabu ina njia zake za kufikia mafanikio na mpaka sasa njia za Simba ndio zimeonekana bora zaidi.