kikoozi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2015
- 2,094
- 3,108
Habari za uzima ndugu, nina binti mmoja nipo nae kwenye mahusiano. Huyu binti kiukweli kabisa kutoka moyoni ni binti ambaye si wife material (kwangu), ila kuna kitu huwa nakiwaza sana kichwani.
Huyu binti kwao ni watu wenye uwezo mkubwa sana kipesa, yaani wana pesa sana sana sana wameiacha familia yangu kiuchumi kwa asilimia kama 75%.
Nina kazi yangu na nina shughuli zangu zingine za kunifanya niishi mjini bila shida yeyote ile lakini kuna muda wazo kichwani linaniambia kwamba, nimuoe huyu huyu nimzalishe pia nikiwa na uhakika wa asilimia 100% watoto wataishi kwenye good-life hata kama ikitokea mungu amenichukua.
Nikiwa nawaza hivyo roho yangu inashindwa kunifanya nimuache huyu binti, ila ni binti mwenye kiburi, jeuri, dharau na mambo mengine mengi tu ila ndio nipo naye.
Naombeni ushauri wenu wa dhati ndugu zangu, ili nichukue maamuzi sahihi kabisa.