Nampenda binti wa kitajiri ila ana kiburi, jeuri na dharau. Je, nimuoe?

Nampenda binti wa kitajiri ila ana kiburi, jeuri na dharau. Je, nimuoe?

hata hayo maisha mazuri unayoyaona kwa familia ya huyo binti ujue kuna mwanaume alipambana..!,bado una muda wa kupambana na kufika walipo na hata kuwa zaidi yao as long as hujakata tamaa,weka kwanza vigezo vya mke unayemtaka mbele kama hajafit kwenye vigezo vyako na pia nafsi yako inakupa mashaka move on mkuu, usiendeshwe na woga wa maisha na mapenzi achana na hilo jipu kama hana values unazotaka.wazee walisema kosea vyote ila usikosee kuoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Point
 
Mbona unatanguliza kufariki? Una matatizo gani? Je akifa yy akakuachia hao madogo?
emoji848.png
🙆‍♀️😬😬maisha magumu nyie
 
nataka kuoa, ila pia naagalia kama nikifariki watoto wangu watabaki kwenye hali gani ya kimaisha
Dah mkuu unaonekana hujiamini kabisa ...Stand as man ..pambana hadi dakika ya mwisho ,...huyo mwanamke ashaona udhaifu wako ndo maana anafanya chochote anajua utaenda wap? ...we unamuonyesha kumuabudu badala ya kuwa kama mwanaume ..... stay strong mkuu
 
Watoto wa kiume siku hizi ndio maana wanawake wanwatawala na kuwaingilia mamlaka yenu.

Kwanza kwa namna umeandika unaonekana wazi wewe una lack self esteem na hauna mamlaka ndani yako na katika maisha yako.

Wewe umeshaona kuwa huyo mtu ana kila possibilities za kuja kukufanya ujutie baadae.... Why unahangaika nae....?! Kazi kutujazia Ma'single mother mtaani na watoto bastards wasioelewa kosa lao ni lipi hadi kuzaliwa nje ya familia.

Huu upuuzi kwann mnauendekeza.....?!

Pesa ni zao sio za kwake?! So unataka kuishi na kuwafanya watoto wako waishi kwa mali za ukweni?!

Wewe unataka kuleta damu ya umasikini katika kizazi chako. Watoto wanafuata nyayo za baba, sasa kama baba ndie mzembe kiasi hiki?!

Kama huyo mwanamke umeshaona hizo dalili tafuta mwanamke mtakae sikilizana na kufanya mambo yenu pamoja na sio ambaye mtakuwa mnavimbiana na kushindana kuwa nani yupo juu.

Huwa nakwazika sana ninapoona matoto ya kiume yanaleta ulegelege katika uanaume no wonder wanawake wanaamua kuwabebea ujauzito wanaume nje ya ndoa sababu wanaona waliowaoa sio wanaume kamili.....

Shika njia yako, mwanamke sahihi na anaejitambua atakufuata uelekeo wako.

Mwanamke asiyekubali kuwa chini ya mwanaume huyo si mwanamke ni matatizo.

Mwanamke asie na adabu na mjeuri kiburi kwa mwanaume ndio wengi wanaishia na maisha ya kutangatanga, wawe wamesoma au hawajasoma, wawe na pesa wasiwe na pesa, kutangatanga kupo pale pale.

Wewe ndie mwanaume acha ufala...... Mwanamke kiburi asie na utii kwako atakuwa mzigo katika safari yenu ya maisha....

Mabinti wazuri wapo wengi sana, zunguka na tafuta utapata. Haujaambiwa mwanamke wako yupo mkoa gani utashangaa unakutana nae..na wewe mwanaume, ili mwanamke akubali kuwa chini yako ni lazima uwe na uelekeo wa maana sio kukalia upuuzi upuuzi tu na hauna ramani. Wanawake huwa hawatazami unapesa kiasi gani as long as u are a man and u have control over your life. Tafuta usiogope.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiburi,heshima,adabu ndio vipaumbele vyangu Hata utoke ukoo wa kina MO

ukikosa heshima,ukawa mwenye kiburi,jeuri,madharau nakuacha kweupe yani

siwezi jifunga kamba shingoni huku najiona,Mr acha kuwa mnyonge unakoelekea

ni kuja kuanza kupiga simu ukweni upewe hela za matumizi,huo ni uduanzi no.1 unaokunyemelea

kwanza mpaka saivi akili lako limeshalala,yani tayri ushajiona huwezi mpa good life mwanao "wewe kama wewe"

come on buddy kwani what is good life? asee acha hiyo cockroach stay strong,hivi wanao utawarithisha nini ase ukiwa na mawazo hayo?

Kama member 1 alivyosema huko juu,Baki nae kama unatafuta mtaji wa kutokea kimaisha ila Kama unahitaji Kuoa unataka mke Hamna kitu hapo,sasa jichanganye uone hata hicho kidogo unachokitafuta sasa hivi utakuja kukipteza.

Ukimuoa TU na ikafika mahali yakakushnda ukataka muachane,mtagawana pasu kwa pasu hadi kitanda atachukua kitanda utachukua godoro,Mahakama haitojali wewe n maskini wao wanapesa,yani utapitishwa mgawanyo wa pasu kwa pasu nakwambia.

utabaki mweupeeee peeee mwisho kama nakuona UTASUSAAAAA ETIII, ukisusa ndo umeumia zaid🤣🤣
 
Habari za uzima ndugu, nina binti mmoja nipo nae kwenye mahusiano. Huyu binti kiukweli kabisa kutoka moyoni ni binti ambaye si wife material (kwangu), ila kuna kitu huwa nakiwaza sana kichwani.

Huyu binti kwao ni watu wenye uwezo mkubwa sana kipesa, yaani wana pesa sana sana sana wameiacha familia yangu kiuchumi kwa asilimia kama 75%.

Nina kazi yangu na nina shughuli zangu zingine za kunifanya niishi mjini bila shida yeyote ile lakini kuna muda wazo kichwani linaniambia kwamba, nimuoe huyu huyu nimzalishe pia nikiwa na uhakika wa asilimia 100% watoto wataishi kwenye good-life hata kama ikitokea mungu amenichukua.

Nikiwa nawaza hivyo roho yangu inashindwa kunifanya nimuache huyu binti, ila ni binti mwenye kiburi, jeuri, dharau na mambo mengine mengi tu ila ndio nipo nae.

Naombeni ushauri wenu wa dhati ndugu zangu, ili nichukue maamuzi sahihi kabisa.
Zalisha kaa pembeni full stop
 
Kwann ukose mahaba ya ndoa kisa visenti? Tajiri bongo? Watu wanapesa bhanaa afu jeuri hizo kama za demu wako tajiri uchwara hawana
 
Wanaomtaja Mungu kwenye hili wanakupotosha. Umempenda mwenyewe, unayaona anayokuonyesha kabla hamjaenda hata fungate hivyo ni akili mkichwa.

Love is blind ila baadaye utasema I wish i followed the advises I got from JF. Aisifiye mvua imemnyea. Moyo waweza kukupeleka kwenye kisu cha mchinjaji ukidhani anakujaribu, kumbe ndo bye.
 
Back
Top Bottom