Aliyekwambia Ukiwa Masikini wewe ni mdhambi ni nani?,Biblia haitambui umasikini kama dhambi,sijui upande wa Quran!
Tangu wanadamu wawepo Duniani,Hakuna mahali pamewahi nukuliwa kwamba wanadamu wote waishio duniani ni matajiri!,binafsi sijawahi kuona mahali popote,Uenda wewe mkuu umewahi kutana na hayo machapisho!
Kama utatengwa na watu wa kanisani au kanisa litakutenga kisa Umasikini unaenda kanisani kufanya Nini?,Mungu hadili na kanisa,Mungu hudili na an Individual Person anayemtafuta Kwa dhati siyo kanisa!
Unaweza ukamuabudu Mungu,ukamtii na ukamuamini hata ukiwa kwako hapo hapo!
Unataka ukifa uzikwe na Askofu au Padri Ili iweje?,yaani unatafuta hela Ili mazishi yako yaendeshwe na Askofu au Padri!?,How,Kama hii ndiyo Perception yako bado unasafari ndefu mno!
Yesu alimuamini Mungu,alimtii Mungu na kutenda Mapenzi ya Mungu;Hakuna binadamu aliyedharaulika na kupitia mateso kama Yesu,bado alikufa akazikwa na watu wa kawaida siyo Padri Wala Askofu,lakini Yesu alififufuka kama Shujaa!
Askofu atakusaidia Nini wakati naye ni mwanadamu mwenye dhambi kama wewe?,sikitika Endapo utakufa ukiwa mwenye dhambi siyo kusikitika kisa umekufa ukiwa Masikini!
Hata uwe na pesa zaidi ya Billgate aliyekwambia utawaridhisha ndugu ni nani?
Tafuta pesa zikusaidie wewe na familia yako (Mke wako na watoto wako),Siyo utafute pesa Ili ndugu wakuone wa maana!
Umasikini utakutesa Endapo unataka Utajiri ili uwababaishe watu!,