Habari wana JF,
Hii ilitokea wakati tukiwa chuoni wakati dada akiwa First year alikuwa na mchumba wake (mtanashati) ambaye alikuwa ndiyo kamaliza chuo na kupata kazi Dsm kwa hiyo alikuwa na fedha kiasi.Nilikuwa nikimsikia mdada akilalamika kwamba kijana haonyeshi kumjali kwani hampigii simu mara kwa mara ingawa yeye amekuwa akifanya hivyo.Kuna siku aliniuliza kama nimekariri kichwani namba ya mchumba wangu nikamwambia ndiyo na nikamtajia jambo lile lilitokea kumvutia sana na akasema mchumba wake hajaiweka namba yake kichwani hivyo akawa anahisi inawezekana hampendi kwa uhakika au inawezekana akawa na watu wengi anaowajali kimapenzi zaidi yake.
Alipofika mwaka wa pili kuna kaka mmoja ambaye alikuwa akisoma nae course moja alikuwa akionyesha kumjali kwa maongezi, kumsaidia kimasomo ingawa hata dada nae alikuwa kichwa darasani.Tatizo la huyu kaka alikuwa mpolipoli kwa kuwa alikuwa akitegemea boom (Government Allowance) pekee kwa kujikimu kimaisha Chuoni hivyo uvaaji wake ulikuwa hafifu hasa kwa wadada wanaopapatikia masharobaro.Upendo aliokuwa akionyesha yule kaka kwa mdada taratibu dada wa watu akaanza kuhamisha moyo wake kutoka kwa mtanashati kwenda kwa mpolipoli.
Hatimaye dada akaamua kumuacha mchumba wake waziwazi na watu wote tukajua ingawa wengine walimshangaa.Lakini akaamua kumchagua mpolipoli bila watu wengine kujua na kwa kuwa dada alikuwa ni mrembo kulinganisha na personality ya jamaa kwa muda ule hivyo hakuwashirikisha watu ktk uamuzi wake kwa kuhofia kukatishwa tamaa na watu wake wa karibuhata mimi nilikuja kujua ndoa inakaribia kufungwa baada ya yeye kunitaarifu ili nikampe company.Ndoa ilifungwa na kupendeza sana ingawa kati ya watu zaidi 100 ambao walikuwa karibu na yule dada walipata taarifa baada ya harusi ila mimi na wenzangu watano tuliwawakilisha.
Baada ya kumaliza chuo ndoa ilifungwa na mpaka sasa dada ni Afisa utumishi na mkaka ni mhadhiri wa Chuo Kikuu na baada ya kupata kazi upolipoli uliisha na utanashati ukaibuka mpaka sasa ndoa yao ina miaka kumi na wanaishi kwa raha na amani.