Nampongeza dada huyu kwa jinsi alivyochagua mume wa kumuoa na kumuacha mchumba wake wa zamani

Nampongeza dada huyu kwa jinsi alivyochagua mume wa kumuoa na kumuacha mchumba wake wa zamani

Kipolipoli ndio nini? unamaanisha mtu wa porini?
Wanawake wenye akili timamu hawapendagi masharobaro or watanashati, ila wanawake mapepe ndio wanabase kwa dizain hiyo ya wanaume.
 
Swali:

Kwanini huyu dada alifanya siri hivyo uhusiano wao? wasn't she proud of the mpori pori?

Alikuwa proud na jamaa na ndiyo maana aliolewa naye na kwa kuwa wazazi wa binti nao walikuwa wasomi walimkubali yule kijana kwa mikono miwili.Dhehebu alilokuwa anasali yule dada ambalo ni tofauti na la wazazi wake lilikuwa na complications sana hivyo kama angeweka mambo hadharani mapema na kukaa kwa muda mrefu amini angekuwa discouraged kuanzia kwa viongozi wa kidini hadi kwa wanachuo wenzake maana kwa muda ule mdada alikuwa anaonekana tofauti kidogo compared to mpolipoli Pia watu wengi wana tabia ya ku judge the book by looking its cover.Moyoni alikuwa anajua mara baada ya jamaa kumaliza chuo na kupata kazi mambo yangebadilika hasa kimavazi.
 
Hongera zao, Jambo la muhimu katika maisha ya yoyote yale ni kujitambua, mtu anatakiwa kujitathmini kuwa anapenda kuwa na mtu wa aina gani, anafurahishwa na kitu gani katika mapenzi na anategemea kuishi maisha gani katika ndoa kisha chukua hatua madhubuti for your own happiness. Kama umesema naye mara kadhaa hakuelewi wala habadiliki na wewe unaona hamshabiiani bora muachane ili kila mmoja atafute wa kufanana naye na hii ndiyo furaha ya mapenzi na ndoa kwa ujumla.
 
Mvumilivu hula mbivu...Dada alivumilia kwa "mpoli mpoli" baada ya kumuona ana mapenzi ya kweli kwake ukilinganisha na yule mtanashati ambaye hata namba ya mrembo alikuwa haikumbuki kwa kichwa sasa wanakula maisha kwa raha zao.




hadithi hii inatufundisha nini...?
 
Last edited by a moderator:
Habari wana JF,

Hii ilitokea wakati tukiwa chuoni wakati dada akiwa First year alikuwa na mchumba wake (mtanashati) ambaye alikuwa ndiyo kamaliza chuo na kupata kazi Dsm kwa hiyo alikuwa na fedha kiasi.Nilikuwa nikimsikia mdada akilalamika kwamba kijana haonyeshi kumjali kwani hampigii simu mara kwa mara ingawa yeye amekuwa akifanya hivyo.Kuna siku aliniuliza kama nimekariri kichwani namba ya mchumba wangu nikamwambia ndiyo na nikamtajia jambo lile lilitokea kumvutia sana na akasema mchumba wake hajaiweka namba yake kichwani hivyo akawa anahisi inawezekana hampendi kwa uhakika au inawezekana akawa na watu wengi anaowajali kimapenzi zaidi yake.

Alipofika mwaka wa pili kuna kaka mmoja ambaye alikuwa akisoma nae course moja alikuwa akionyesha kumjali kwa maongezi, kumsaidia kimasomo ingawa hata dada nae alikuwa kichwa darasani.Tatizo la huyu kaka alikuwa mpolipoli kwa kuwa alikuwa akitegemea boom (Government Allowance) pekee kwa kujikimu kimaisha Chuoni hivyo uvaaji wake ulikuwa hafifu hasa kwa wadada wanaopapatikia masharobaro.Upendo aliokuwa akionyesha yule kaka kwa mdada taratibu dada wa watu akaanza kuhamisha moyo wake kutoka kwa mtanashati kwenda kwa mpolipoli.

Hatimaye dada akaamua kumuacha mchumba wake waziwazi na watu wote tukajua ingawa wengine walimshangaa.Lakini akaamua kumchagua mpolipoli bila watu wengine kujua na kwa kuwa dada alikuwa ni mrembo kulinganisha na personality ya jamaa kwa muda ule hivyo hakuwashirikisha watu ktk uamuzi wake kwa kuhofia kukatishwa tamaa na watu wake wa karibuhata mimi nilikuja kujua ndoa inakaribia kufungwa baada ya yeye kunitaarifu ili nikampe company.Ndoa ilifungwa na kupendeza sana ingawa kati ya watu zaidi 100 ambao walikuwa karibu na yule dada walipata taarifa baada ya harusi ila mimi na wenzangu watano tuliwawakilisha.


Baada ya kumaliza chuo ndoa ilifungwa na mpaka sasa dada ni Afisa utumishi na mkaka ni mhadhiri wa Chuo Kikuu na baada ya kupata kazi upolipoli uliisha na utanashati ukaibuka mpaka sasa ndoa yao ina miaka kumi na wanaishi kwa raha na amani.



zp



Hii
 
Dot com generation hatupendi hadithi hadithi tunataka vitendo,,, mambo ya upori pori sijui uhadhiri peleka kijijini.. Mjini pesa tabia kijijini...

Let's me get ready for sweet 16.. Can't wait to see Gators advance to final four
 
Back
Top Bottom